Skip to main content

Posts

Showing posts from April 7, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Mbunge Ghati Chomete Awaombea Maji Wananchi wa Kata za Bisumwa,Nyankanga na Bukabwa Wilaya ya Butiama

Na Shomari Binda-Musoma  MBUNGE wa viti maalum mkoa wa Mara Ghati Chomete amewaombea upatikanaji wa maji wananchi wa Kata za Bisumwa,Nyankanga na Bukabwa zilizopo Wilaya ya Butiama. Maombi ya mbunge huyo ameyatoa leo April 8 bungeni katika kikao cha kwanza cha mkutano wa 19 wa bunge la bajeti alipokuwa akiuliza swali la nyongeza kwenye Wizara ya Maji. Kabla ya kuuliza swali hilo mbunge huyo ameishukuru serikali kwa kutekeleza miradi mbalimbali ya maji ili kuwezesha wananchi kupata maji kwenye maeneo yao. Amesema miradi hiyo imewezesha kumtua mama ndoo kichwani na kumshukuru Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha nyingi kwaajili ya miradi hiyo. " Mheshimiwa Naibu Spika nashukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza kwenye Wizara ya Maji. " Kwanza naidhukuru serikali kwa utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maji kwa mkoa wa Mara,swali langu ni lini wananchi wa Kata za Bisumwa,Nyankanga na Bukabwa wilayani Butiama watafikishiwa huduma ya maji?",ameuliza Akiji...

Happy Birthday George Marato

GMTV inakutakia George Marato, heri njema na baraka tele katika siku yako ya kuzaliwa! Hongera kwa kufikia hatua nyingine ya maisha. Uendelee kuwa na afya njema, furaha, na mafanikio katika kila unachofanya. Siku hii iwe ya kipekee kwako, ikujaze matumaini mapya na kumbukumbu nzuri zisizosahaulika.

Balozi Dkt Nchimbi Akutana wa Askofu wa Jimbo la Mbinga

 Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, akizungumza jambo na Askofu John Chrisostom Ndimbo wa Jimbo Katoliki la Mbinga, walipokutana Uwanja wa Ndege wa Songea, mkoani Ruvuma, Jumatatu tarehe 7 Aprili 2025.

Femata Yampongeza Igp Mstaafu Siro Kuteuliwa Kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Sitamico

 Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini   FEMATA Mr .Yusuph Kazi anatoa pongezi kwa  Mwenyekiti wa bodi ya STAMICO aliyemaliza muda wake  Major General ISAMUHYO kwa kazi kubwa aliyoifanya kwa kipindi chote ambacho ameongoza tangu kupewa nafsi hiyo.  Aidha nachukua nafasi hii kumpongeza  Mh Balozi SIMON NYAKORO SIRRO (IGP mtaafu ) kwa kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa bodi ya  Madini Tanzania yaani STAMICO.   Tuna imani na wewe kubwa na Mwenyezi Mungu akutangulia katika majukumu yako mapya.Madini ni maisha na Madini  ni utajiri.

Balozi Nchimbi Afunga Kazi Ruvuma

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, amehitimisha ziara yake ya siku tano mkoani Ruvuma, akisisitiza kuwa CCM itaendelea kuwa chama cha wanachama, kwa ajili ya kuwatumikia wananchi wote na kuwa mtetezi wa wanyonge. Balozi Nchimbi amesema kwamba katika kuendeleza nafasi yake kama taasisi imara inayohusika na uongozi wa nchi, CCM hakina budi kuendeleza misingi ya sera zake zinazolenga kubadilisha hali za maisha ya watu, kuendana na mahitaji ya nyakati, na kuzingatia maslahi ya taifa. Dkt. Nchimbi aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na wanaCCM na wananchi wa mji wa Songea, waliokusanyika kumpokea alipofika kufungua mradi wa kitega uchumi wa Tawi la CCM la Mshangano mjini Songea, Jumapili tarehe 6 Aprili 2025, ikiwa ni siku ya tano tangu alipoanza ziara hiyo tarehe 2 Aprili 2025. Katika ziara hiyo aliyoanzia katika Wilaya ya Tunduru, Namtumbo, Nyasa, na hatimaye Songea mjini, Balozi Nchimbi alitoa pongezi kwa Serikali ya CCM, inayoongozwa na Rais wa...

Michuano ya Afcon na Chan Itaendeleza Michezo na Utalii Nchini - Majaliwa

_▪️Aridhishwa na kasi na ubora wa ukarabati_ WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema uamuzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Ali Mwinyi wa kuridhia Mashindano ya AFCON na CHAN kufanyika nchini utasaidia kwa kiasi kikubwa kuendeleza na kukuza sekta ya michezo na utalii nchini.  Akizungumza baada kukagua ukarabati na ujenzi wa Viwanja vya Amani, Maisara na Mao Zedong Zanzibar leo Aprili 7, 2025, Mheshimiwa Majaliwa amesema Watanzania watapata fursa ya kuendeleza michezo na kuhamasisha wachezaji kufanya mazoezi zaidi ili wapate sifa za kucheza michuano hiyo. “ujio wa wageni wakati wa michuano utahitaji malazi, chakula na usafiri  hivyo waliowekeza kwenye hoteli na vyombo vya usafiri watapata faida kubwa na kujiingizia kipato, hii ni fursa nzuri ambayo Marais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan na Dkt. Hussein Ali Mwinyi wametuletea kwa sababu timu zinakuja na watu wengi.” Aidha Mheshimiwa Majaliwa amesema ameridhishwa n...

Bunge la Mwisho Kabla ya Uchaguzi Mkuu Kuanza Kesho Aprili 8

 

Kirigini Ampongeza Rais Dkt.Mwinyi Kusimamia Misingi Ya Uongozi qa Hayati Rais Abeid Amani Karume

Na Shomari Binda-Musoma  RAIS wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dkt.Hussen Ally Mwinyi amepongezwa kwa kusimamia misingi ya uongozi uliofanywa na Hayati Rais wa Kwanza wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Sheikh Abeid Aman Karume. Pongezi hizo zimetolewa na kada wa Chama cha Mapinduzi( CCM) na Mjumbe wa zamani wa (NEC) Paul Herman Kirigini. Akizungumza kwa njia ya simu na GMTV leo aprili 7 katika kumbukizi ya miaka 53 tangu kifo cha Hayati Karume amesema moja ya misingi hiyo ni kuwaletea maendeleo wananchj wa Zanzibar. Amesema tangu serikali ya awamu ya 8 ya Dkt.Mwinyi iingie madarakani yameshuhudiwa mabadiliko makubwa ya kimaendeleo kwenye visiwa vya Zanzibar. Kirigini amesema moja ya kumbukumbu ya hutuba za Hayati Shekh Abed Aman Karume ni vijana kujiandaa kuja kuwaongoza wananchi na kuwaletea maendeleo wananchi jambo linalofanywa vyema na Rais Dkt.Mwinyi. Amesema ujenzi wa skuli kwa ajili ya maendeleo ya elimu zimekuwa zikijengwa na kushuhudiwa ufunguzi wake mara kwa mara. Kirig...