Skip to main content

Posts

Showing posts from September 30, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Kura zote Butinzya tumpigie Dkt Samia - Dkt.Biteko

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Bukombe kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Doto Mashaka Biteko amewahimiza wananchi wa Kata ya Butinzya, Wilayani Bukombe kumpigia kura mgombea wa Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM)Dkt. Samia Suluhu Hassan ili aendelee kuongoza na kusimamia miradi ya maendele iliyokwishaanzishwa na hivyo kuwaletea maendeleo. Dkt. Biteko amesema hayo Septemba 30, 2025 wakati wa mkutano wa kampeni katika Kata ya Butinzya wilayani Bukombe mkoani Geita ikiwa ni sehemu Kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani utakaofanyika Oktoba 29, mwaka huu. Amesema wananchi wanalo jukumu la kujotokeza kwa wingi kupiga kura na watakapopiga kura maana yake ni kutimiza wajibu wao kidemokrasia ambao utawawezesha kutimiziwa mahitaji yao kwa kujengewa miradi ya maji, umeme, barabara, hospitali na shule. Amesema katika miaka mitano iliyopita wananchi hao wakishiriki katika kutekeleza miradi ya maendeleo iliyolenga kutatua changamoto za Bukombe na sasa jukumu lililo...

Kura Zote Butinzya Tumpigie Dkt. Samia - Dkt. Biteko

Dkt.Nchimbi Awahimiza Wana Ilala Kumpigia Kura za Kishindo Dkt.Samia

Mgombea Mwenza wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Emmanuel  John Nchimbi akiwasalimia na kuzungumza na Wananchi wa Ilala-Machinga Complex leo Oktoba 01, 2025 akiendelea na mikutano yake ya kampeni kwa Mkoa wa Dar es Salaam. Mara baada ya kuwasalimia Wananchi hao,Dkt.Nchimbi pia alipata nafasi ya kumnadi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Ilala Ndugu Mussa Azzan Zungu pamoja na Madiwani . Pamoja na hayo Dkt.Nchimbi amewahamiza Wananchi hao kujitokeza kwa wingi ifikapo Oktoba 29,2025 na kumpigia kura za kutosha Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM),Dkt.Samia Suluhu Hassan,Wabunge na Mdiwani na hatimae kuibuka na ushindi wa Kishindo. Dkt. Nchimbi anahitimisha kampeni zake leo kwa mkoa wa Dar es Salaam akifikisha mkoa wa 15 tangu kuzinduliwa kwa kampeni hizo Agosti 28,2025 jijini Dar na kuelekea mikoa mingine kusaka kura za ushindi wa kishindo kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Ccm Yaja na Suluhisho la Kudumu la Maji Ilala na Segerea

MGOMBEA Mwenza wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, amesema chama hicho kikipewa ridhaa ya kuongoza katika kipindi cha miaka mitano ijayo, kitahakikisha changamoto ya maji katika Wilaya ya Ilala na Jimbo la Segerea inabaki kuwa historia. Amesema azma ya CCM ni kuanzisha mradi mkubwa wa uzalishaji na usambazaji maji kwa maeneo hayo, sambamba na kupanua mtandao wa mabomba ili kufikisha huduma kila sehemu.  Aidha, mabomba yaliyoharibika au kukatika chini ya ardhi yatafukuliwa na kuwekwa mapya ili kuboresha upatikanaji wa maji safi na salama. Dk. Nchimbi ameongeza kuwa Serikali ya CCM itajenga tanki kubwa la maji kwa ajili ya Jimbo la Segerea, ambapo kwa sasa lina ujazo wa mita za mraba 273 pekee, lakini litaboreshwa na kuongezwa mara nne hadi kufikia ujazo wa mita za mraba 845 milioni. Akizungumza katika mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika Jimbo la Segerea, Wilaya ya Ilala mkoani Dar es Salaam, Dk. Nchimbi alisema hatua hiyo inalenga kutatua...

Dkt Nchimbi "Uzalishaji Maji 'ilala' Kufikia Lita Milioni 845" Ahimiza Wananchi Kutiki Ifikapo Oktoba 29

Mgombea mwenza wa kiti cha Urais kupitia CCM, Balozi Dkt Emmanuel Nchimbi amesema kwamba Serikali ijayo ya Dkt. Samia Suluhu Hassan imenuia kwa dhati kuongeza uzalishaji wa Maji katika Wilaya ya Ilala kutoka ujazo wa lita takribani Milioni 273 hadi kufikia ujazo wa lita milioni 845. Dkt Nchimbi ametoa kauli hiyo leo Septemba 30, 2025 Jijini Dar es Salaam katika Jimbo la Ukonga, Wilaya ya Ilala katika mwendelezo wa mikutano ya Kampeni za Urais kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29 mwaka huu. "Nataka niwaambie ndugu zangu wana Ilala, hiyo ndio ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya 2025-2030 ilivyojipanga kuondoa changamoto ya maji kwa Wakazi wa Ilala na Vitongoji vyake katika majimbo ya Ukonga na Segerea, ambapo Ongezeko hilo ni zaidi ya mara nne, kwa hiyo niwaombe tuendelee kuiunga mkono CCM ili iweze kutimiza ahadi zake kwa wananchi" amesema Dkt Nchimbi.