*▪️Asisitiza Serikali itaendelea kuwawezesha wawekezaji wazawa* *▪️Aeleza mpango wa Serikali wa kukabiliana na ugonjwa wa Malaria nchini* Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameitaka Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) ihakilishe inatoa kandarasi za ujenzi na ukarabati wa barabara kwa wakandarasi wenye uwezo wa kujenga kwa viwango vinavyoendana na thamani ya fedha. Ameyasema hayo leo (Alhamisi, Februari 13, 2025) wakati akijibu swali la Mbunge wa Kinondoni, Abbasi Tarimba aliyehoji kwanini Serikali isianze kutumia vikosi kazi vya Manispaa au TARURA badala ya wakandarasi binafsi katika ukarabati wa barabara zilizoharibika, katika kipindi cha maswali kwa Waziri Mkuu, bungeni jijini Dodoma. “Tunaitaka TARURA iwasimamie wakandarasi binafsi wanapopewa kazi, wawe na uwezo wa kujenga barabara za kudumu kwa mujibu wa viwango vilivyopo ili barabara ziweze kutumika kwa muda mrefu. ” Amesema kuwa awali mfumo wa ujenzi wa barabara za vijijini uliokuwa unaruhusu Halmashauri kukarabati ba...
Marato tv - Sauti ya Jamii