Serikali ya Tanzania imesema hakuna sheria iliyokiukwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam ilipoamua kusikiliza kesi ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu kwa njia ya mtandao. Hayo yameelezwa Ijumaa Bungeni mjini Dodoma na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Hamza Johari, wakati wa mjadala wa bajeti ya Wizara ya Katiba na Sheria kwa mwaka 2025/26. “Ukifuatilia kilichotokea tarehe 24, Procedures (taratibu) zile zilikuwa properly lollowed (zimefuatwa inavyotakiwa), sasa huyu mtu anayetokea anayesema kuna uvunjifu wa sheria, sheria ipi sheria si ndiyo hii?,” alihoji Johari na kuongeza: “hii ndiyo sheria, na mimi ninayezungumza hapa ndiye Mwanasheria Mkuu wa Serikali.” Akifafanua zaidi, Johari alisema Mahakama inaweza kuendesha kesi kwa njia ya mtandao iwapo imeona kuna tishio lolote baada ya kufanya tathmini. “Mahakama itaassess (tathmini) mazingira yaliyopo siku hiyo na kuona kwamba tuisikilizeje shauri hili na hasa kama kuna mazing...