Skip to main content

Posts

Showing posts from May 6, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Dodoma Yapongezwa Kupeleka Walimu 40 Korea Kusini

Na Mwandishi Wetu, Dodoma Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI, Profesa Riziki Shemdoe, ameipongeza Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kwa kuandaa mpango wa kuwapeleka walimu 40 kwenda kusoma Korea Kusini, akieleza kuwa ni hatua muhimu ya kuimarisha ubora wa elimu nchini. Akizungumza katika Mkutano wa Wadau wa Elimu Mkoa wa Dodoma uliofanyika katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini hapa, Waziri Shemdoe alisema mpango huo unaendana na juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuboresha sekta ya elimu nchini. “Mpango huu unaonyesha dhamira ya kweli ya kuboresha elimu kupitia uwekezaji kwa walimu. Serikali itaendelea kuunga mkono juhudi kama hizi,” alisema Profesa Shemdoe. Mkutano huo uliandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule, kwa lengo la kuhamasisha walimu, wanafunzi na watendaji wa halmashauri kuongeza juhudi katika kuboresha ufaulu wa elimu mkoani humo. Akizungumza katika mkutano huo, Senyamule alisema mafanikio y...

Temesa Wampokea Bosi Mpya

Na Josephat Lazaro  Watumishi wa Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) wamempokea rasmi Mtendaji Mkuu mpya wa TEMESA Bwana Kheri Mahimbali, ambaye ameteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan.  Akizungumza mara baada ya kuwasili katika ofisi za Makao Makuu ya TEMESA, Bw. Mahimbali amewashukuru watumishi kwa mapokezi mazuri na ya heshima waliyompatia na kuwaahidi  kushirikiana nao kwa karibu wakati wote katika kutekeleza majukumu ya taasisi kwa ufanisi pamoja na kuzingatia uboreshaji wa maslahi ya watumishi ili kuongeza tija na ari ya utendaji kazi.  Bw. Mahimbali amemshukuru Mhe. Rais kwa uteuzi huo na kuahidi kutekeleza maagizo yote kwa weledi na ufanisi ili kuhakikisha anafikia matarajio ya maboresho ya TEMESA na utoaji Huduma Bora.

Makonda Mgeni Rasmi Kikao kazi cha Maafisa Habari Njombe

Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Paul Makonda, anatarajiwa  kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa Kikao Kazi cha 21 cha Maafisa Habari, Mawasiliano, Itifaki na Uhusiano Serikalini Mei 7, 2026 mkoani Njombe. Kikao kazi hicho cha mwaka,  kimewakutanisha zaidi ya Maafisa Habari 300 kutoka taasisi mbalimbali za Serikali kote nchini kwa lengo la  kuwanoa na kuwajengea uwezo maafisa hao kusimamia na kuzifikisha kwa ufanisi taarifa za Serikali kwa umma. Kupitia kikao kazi hicho washiriki watapata mafunzo na kufanya mijadala mizito ikiwemo ya uandishi wa kisasa wa taarifa kwa umma, mbinu za kuandika makala zenye mvuto magazetini pamoja na kanuni muhimu za itifaki katika shughuli za kitaifa. Aidha, watapata fursa ya kujifunza kuhusu matumizi sahihi ya picha za viongozi, utaratibu wa utajo rasmi na suala la mwonekano wa mavazi katika mikutano ya kitaifa na kimataifa Katika hatua ya kuimarisha  ya Serikali hadi ngazi za chini, was...

Mbunge wa Kasulu Vijijini Aipongeza Serikali kutoka Billioni 1.5 Miradi ya Maji Kasulu Vijijini

MBUNGE wa Jimbo la Kasulu Vijijini Edibilly Kazala ameipongeza Serikali kupitia wizara ya Maji Kwa  kutenga shilingi bilioni 1.5 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maji katika vijiji mbalimbali, hatua inayolenga kupunguza changamoto ya muda mrefu ya upatikanaji wa maji safi na salama. Akizungumza Bungeni leo Mei 6, 2026 jijini Dodoma wakati akichangia Bajeti ya Wizara ya Maji kwa mwaka wa fedha 2026/2027, Mbunge wa Kasulu Vijijini, Mhe. Edibilly Kazara ameishukuru  Serikali kupitia Wizara ya Maji kwa uamuzi wake wa kutenga kiasi cha shilingi bilioni 1.5 kwa ajili ya miradi ya maji katika Jimbo la Kasulu Vijijini.  Hii ni hatua kubwa ya matumaini kwa wananchi wangu.” amesema  Ameongeza kuwa fedha hizo zitatumika kutekeleza miradi katika vijiji vya Chekenya, Kablangiri, Muziwe, Nyakitonto, Malalo, Kazage, Makere, Nyangwa, Karimungoma, Rusesa pamoja na Kitye, sambamba na mradi wa Kizima unaotarajiwa kuchimbwa katika kijiji cha Chambugwe. “Hakika hii ni hatua muhimu i...

Ghati Chomete Aitaka Serikali Kuharakisha Fedha Kukamilisha Miradi ya Maji Mkoa wa Mara

  MBUNGE wa Viti Maalum Mkoa wa Mara, Mhe. Ghati Zephania Chomete, ameiomba Serikali kuharakisha utoaji wa fedha ili kukamilisha miradi ya maji mkoani Mara, akisema ucheleweshaji wa miradi hiyo unaendelea kuwaumiza wananchi, hasa wanawake wanaobeba mzigo wa kutafuta maji kila siku. Akichangia Bajeti ya Wizara ya Maji kwa mwaka wa fedha 2026/27 bungeni Dodoma leo Mei 6, 2026, Mhe. Chomete  amepongeza uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, akieleza kuwa dhamira yake ya “kumtua mwanamke ndoo kichwani” inaendelea kuonekana kwa vitendo.  Mhe. Chomete amesema licha ya Mkoa wa Mara kunufaika na miradi 77 ya maji yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 265 pamoja na miradi sita mipya, changamoto kubwa imebaki kuwa kutokukamilika kwa miradi hiyo kwa wakati. “Mhe. Waziri Aweso,wananchi wanahitaji majibu ya lini miradi hii itakamilika. Mradi wa maji wa Mji wa Isenye uliosainiwa tangu mwaka 2020 kwa zaidi ya shilingi bilioni 38 hadi sasa uko takribani asilimia 15 tu. Hii siyo h...

Chege aitaka Serikali kuharakisha miradi ya maji Mara

MBUNGE wa Rorya, Mhe. Jafari Wambura Chege, ameibana Serikali kuongeza kasi ya utekelezaji wa miradi ya maji katika Mkoa wa Mara, akieleza kuwa ni kinaya kwa mkoa huo uliobarikiwa na rasilimali kubwa ya maji kuendelea kukumbwa na uhaba mkubwa wa huduma hiyo muhimu. Akichangia Bajeti ya Wizara ya Maji leo Mei 6, 2026, Bungeni Jijini Dodoma, Mhe. Chege amesema Takwimu zinaonesha Mara ni miongoni mwa mikoa ya mwisho kwa upatikanaji wa maji safi na salama, licha ya kuzungukwa na maji ya Ziwa Victoria kwa zaidi ya asilimia 70. “Mheshimiwa Waziri, huu ni mkoa unaozungukwa na maji kwa zaidi ya asilimia 70, lakini wananchi wake bado wanateseka kutafuta maji. Hili halikubaliki,” amesisitiza Amesema miradi mingi ya maji iliyoanzishwa imekwama na kushindwa kutoa huduma, hali inayosababisha malalamiko makubwa kwa wananchi, huku fedha nyingi zikiwa tayari zimetumika. “Fedha zimetumika, lakini miradi mingi imesimama. Tunakuomba ufanye ziara maalum ukague na kuchukua hatua,” ameeleza. Mbunge huyo pia...

Makamu wa Rais Dkt Nchimbi amwakilisha Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika mazishi ya Askofu Shauri

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mazishi ya aliyekuwa Askofu wa Pili wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Ruvuma na Katibu Mkuu Mstaafu wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) Marehemu Askofu Stanford Shauri. Mazishi hayo yamefanyika katika Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Ruvuma, Liuli Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma. Akitoa salamu za rambirambi kwa niaba ya Rais. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais amesema Serikali inatambua mchango mkubwa aliyoutoa Askofu Shauri katika hapa nchini, akiwa ametumikia Serikali za Mitaa kwa zaidi ya miaka 12 pamoja na kuwa katibu mkuu wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) kwa zaidi ya miaka 10. Aidha, Makamu wa Rais amesema Marehemu Askofu Shauri amekuwa na mchango mkubwa katika maendeleo ya jamii pamoja na kuendeleza na kuikuza imani ya kikristo nchini. Amesema ni dhamira ya Serikali kuendeleza yale ambayo Marehemu...

Wanafunzi Wajifunza Uendeshaji wa Bunge Dodoma

NAIBU Waziri wa Elimu na Teknolojia ya Habari, Wanu Hafidh Ameir, amekutana na kuzungumza na wanafunzi wa Shule ya Chemuchemu jijini Dodoma waliotembelea Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa lengo la kujifunza namna chombo hicho kinavyofanya kazi. Katika ziara hiyo ya kielimu, wanafunzi walipata fursa ya kusikiliza maelezo kuhusu shughuli za Bunge, huku wakihamasishwa kujituma katika masomo yao ili kuwa viongozi bora wa baadaye.  Baada ya mazungumzo hayo, Naibu Waziri alipiga picha ya pamoja na wanafunzi hao kuadhimisha kumbukumbu ya ziara yao. Awali, Afisa Mwandamizi wa Elimu kwa Umma wa Bunge, Waziri Kizingiti, alitoa maelekezo kwa wageni hao kuhusu taratibu za Bunge na namna ya kufuatilia vikao kwa utulivu na nidhamu. Wakiwa ndani ya Ukumbi wa Msekwa, wanafunzi hao walipata elimu ya kina kuhusu mwenendo wa Bunge, sambamba na fursa ya kuuliza maswali mbalimbali ili kuongeza uelewa wao.  Aidha, walihudhuria kipindi cha maswali na majibu ndani ya ukumbi mkubwa wa Bunge...

Makamu wa Rais Dkt.Nchimbi Amwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan katika Mazishi ya Askofu Shauri

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mazishi ya aliyekuwa Askofu wa Pili wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Ruvuma na Katibu Mkuu Mstaafu wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) Marehemu Askofu Stanford Shauri. Mazishi hayo yamefanyika katika Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Ruvuma, Liuli Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma.   Akitoa salamu za rambirambi kwa niaba ya Rais. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais amesema Serikali inatambua mchango mkubwa aliyoutoa Askofu Shauri katika hapa nchini, akiwa ametumikia Serikali za Mitaa kwa zaidi ya miaka 12 pamoja na kuwa katibu mkuu wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) kwa zaidi ya miaka 10. Aidha, Makamu wa Rais amesema Marehemu Askofu Shauri amekuwa na mchango mkubwa katika maendeleo ya jamii pamoja na kuendeleza na kuikuza imani ya kikristo nchini.     Amesema ni dhamira ya Serikali kuendeleza ...

Rais Samia Awaapisha Viongozi wateule, Asisitiza Uadilifu na Utumishi wa Umma

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, leo amewaapisha viongozi mbalimbali walioteuliwa katika hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino, mkoani Dodoma, akiwataka kutanguliza maslahi ya wananchi na kufanya kazi kwa uadilifu, nidhamu na matokeo. Miongoni mwa walioapishwa ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Mahusiano), Evaline Wilbard Munisi, ambaye Rais amesema uteuzi wake umetokana na sifa, uwezo na uzoefu wake katika masuala ya umma. "Evaline ni Katibu Mkuu wa chama cha upinzani cha NCCR-Mageuzi; lakini nimeangalia wasifu wake, nikaona ana sifa za kuingia ndani ya Serikali na kutusaidia," amesema Rais Samia, akisisitiza umuhimu wa kuweka mbele maslahi ya Taifa bila kujali tofauti za kisiasa. Rais amemtaka Dkt. Munisi kushirikiana kwa karibu na viongozi na watendaji wa Ofisi ya Waziri Mkuu kusimamia haki na stahiki za wafanyakazi, pamoja na kuimarisha juhudi za kutafuta fursa za ajira, hususan kwa vijana ndani na nje ya nchi. Aidha, Rais Samia...