Na Mwandishi Wetu, Dodoma Mbunge wa Jimbo la Njombe Mjini, Mhe. Deo Mwanyika, ameishauri serikali kutokuwa na haraka kutoa vibali kwa wawekezaji wa sekta ya misitu wasiowekeza katika kuongeza thamani ya mazao ya misitu mkoani Njombe. Akichangia Hotuba ya Waziri Mkuu bungeni jijini Dodoma, Mhe. Mwanyika aliipongeza serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika jimbo hilo, ikiwemo sekta za elimu, afya, maji, barabara, na umeme vijijini. Katika sekta ya maji, Mbunge huyo alibainisha kuwa miradi ya Ijunilo na Livingstone tayari imekamilika na inaendelea kutoa huduma ya maji kwa wakazi wa Mji wa Njombe, hali iliyosaidia kupunguza mgao wa maji. Aidha, miradi ya Hagafilo na ya majitaka inaendelea na itakapokamilika, inatarajiwa kuongeza upatikanaji wa maji kwa wakazi wa mji huo. Kuhusu umeme, alisema vijiji vyote katika jimbo lake tayari vimeunganishwa na huduma hiyo, na kwa sasa juhudi zinaelekezwa katika vitongoji. Alito...
Marato tv - Sauti ya Jamii