Skip to main content

Posts

Showing posts from February 19, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Oparesheni Ya Kuwadhibiti Fisi Simiyu Yaonesha Mafanikio Makubwa

📍 Zaidi ya Fisi 16 wavunwa. Na Mwandishi wetu, Simiyu. Oparesheni maalumu ya kuwadhibiti wanyamapori wakali na waharibifu aina ya fisi waliokuwa wanaleta taharuki na madhara Kwa jamii inayoendelea Mkoani Simiyu imeonesha mafanikio makubwa baada ya fisi 16 kuvunwa ikiwa ni hatua muhimu iliyochukuliwa na Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii ya kuhakikisha usalama na utulivu Kwa wananchi vinarejea. Hayo yamesemwa leo Februari 19, 2025 na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Kenani Kihongosi alipokuwa akiongea na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari. Mhe. Kihongosi amesema kufuatia changamoto hiyo,  Serikali ilichukua jukumu kubwa la kuhakikisha inalinda wananchi wake ikiwemo kuanzisha oparesheni maalumu inayohusisha Jeshi la Uhifadhi Kwa Taasisi za TAWA, TANAPA na TFS Kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi pamoja na wananchi, oparesheni inayotajwa kuanza  Januari 25, 2025. "Tarehe 20/12/2024 baada ya fisi kuvamia wananchi Serikali ilichukua hatua kubwa ya kushirikisha vyombo ...

Waziri Ridhiwani Kikwete Aitaka Cma Kuwa Taasisi Ya Kimkakati Kutatua Migogoro Ya Kazi

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Ridhiwani Kikwete, ameitaka   Tume ya Usuluhishi na Uamuzi kuwaTaasisi ya kimkakati katika utatuzi wa migogoro ya kikazi nchini ikiwa na lengo la kuchochea ukuaji wa kiuchumi na kuhakikisha mahala pa kazi panakuwa na amani ili kuwafanya  wafanyakazi na waajiri watumie muda mwingi kufanya uzalishaji Wenye Tija. Ameyasema hayo wakati akifungua kikao kazi cha Tathmini ya Utendaji Kazi na mafunzo kwa watumishi wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi Tanzania bara, kilichofanyika Leo tarehe 19 Februari, 2025 Mkoani Morogoro. Aidha, Mhe. Kikwete ameitaka Tume hiyo kushughulikia migogoro kwa haraka, ufanisi na weledi ili kuweza kutimiza matarajio ya wadaawa na wadau ambao wengi wao ni wawekezaji, hivyo kusaidia kukuza Uchumi wa nchi. "Serikali iliongeza bajeti ya Tume kiasi cha zaidi ya Shilingi Milioni mia tisa (900,000,000+) bila shaka mmeona ongezeko hilo limeleta mabadiliko siyo tu kwenye maslahi ya wafany...

Rcc Mkoa Wa Kagera Kutenga Maeneo Kwa Ajili Ya Vikosi Vya Jwtz

  Na Angela Sebastian;Bukoba Kikao cha ushauri cha mkoa wa Kagera kimeridhia kutenga maeneo maalum (viteule) katika mipaka yote ya mkoa huo na kumilikisha vikosi vya jeshi la ulinzi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) ili kuimalisha usalama wa nchi na kupambana na wahamiaji haramu. Mkuu wa mkoa huo Hajati Fatma Mwassa ameeleza hayo leo wakati akifunga kikao cha RCC kilichofanyika Manispaa ya Bukoba mkoani humo kikiwa na agenda mbili kupitia na kuridhia bajeti ya mwaka 2025/2026 pamoja na kuwasilishwa mapendekezo ya kujenga uwanja mpya wa ndege wa mkoa wa Kagera. Anasema wameridhia kwa pamoja kuongeza viteule maeneo ya mipaka ya mkoa huo mazungumzo tayali yameanza na wakuu wa Wilayani zote saba pia kule kwenye ngazi za vijiji ili maeneo yote ambayo ni ya kimkakati kwenye ngazi zile yanakatwa na kumilikishwa kwa jeshi letu la ulizi la wananchi kulinda nchi yetu. "Kikao hiki tumekubaliana kwamba kupitia kamati za usalama ngazi zote kudhibiti uhamiaji haramu wawe wanatoka nje ya nchi au nd...

Uingereza Yavutiwa Na Mkakati Wa Tanzania Kuongeza Thamani Madini Nchini

▪️Yatenga Trilioni 3 kwa ajili ya miradi vya kuongeza thamani madini ▪️Viwanda vya uongezaji thamani madini kupewa kipaumbele ▪️Waziri Mavunde asisitiza madini kuongezwa thamani ndani ya nchi ▪️Serikali yatenga eneo maalum Kahama-Shinyanga 📍 Dar es salaam Waziri wa Uingereza anayeshughulikia masuala ya Afrika *Mh.Lord Collins* amevutiwa na mpango wa nchi ya Tanzania kuandaa mkakati maalum wa uongezaji thamani madini nchini Tanzania na kuahidi kwamba Uingereza itatoa ushirikiano katika kusaidia eneo la uongezaji thamani madini hayo ndani ya nchi. Hayo yamesemwa leo wakati wa kikao kati ya Mh. Lord Collins na Waziri wa Madini Mh. Anthony Mavunde kilichofanyika leo Jijini Dar es salaam. “Tanzania na Uingereza zina ushirikiano wa muda mrefu katika maeneo mengi ya kiuchumi ikiwemo sekta ya Madini. Nimevutiwa na mkakati wa Tanzania wa kuongeza thamani ndani ya nchi, mkakati ambao Uingereza tunauunga mkono na tupo tayari kuwezesha utekelezaji wake kupitia Mradi wa “*Manufacturing Africa*“ am...

Waziri Mkuu Amesema Ubunifu wa Rais Samia Umewanufaisha Watanzania Zaidi ya Millioni Moja

  _Asema kampeni hiyo ya  Mama Samia legal aid ni ubunifu wa Rais Dkt. Samia ili kuwasaidia Watanzania wasio na uwezo kupata huduma za kisheria bure._ WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema kuwa Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia ni ubunifu wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan uliolenga kuongeza wigo wa upatikanaji haki kwa wananchi wasio na uwezo wa kumudu gharama za huduma za kisheria. Amesema kuwa kupitia kampeni hiyo ambayo inatolewa bure mpaka sasa imefanikiwa kuwafikia zaidi ya wananchi milioni moja wakiwemo wanawake 681,326 na wanaume 691,773 katika mikoa 19 nchini. Amesema hayo leo Jumatano (Februari 19, 2025) wakati alipozindua kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia katika mkoa wa Lindi, kwenye viwanja vya Madini, Ruangwa Mkoani Lindi. “Mheshimiwa Dkt. Samia alijifunza shida, kero na changamoto wanazopata watanzania na hasa wale ambao hawana uwezo wa kulipia gharama za huduma za kisheria, aliguswa na akaamua kuanzisha kampeni hii na kuika...

Balozi Dkt Nchimbi Amesema Kamwe Ccm Haiwezi Kuwavumilia Wanaokiuka Kanuni

Dodoma  Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, ameonya vikali wanachama wanaotafuta uteuzi wa udiwani, uwakilishi na ubunge kwa njia zisizo halali, akisisitiza kuwa chama hakitasita kuwaengua wale watakaokiuka Katiba, Kanuni na maadili ya CCM kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2025. Akizungumza jijini Dodoma wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa makatibu wa matawi na kata kutoka Wilaya ya Dodoma, Balozi Nchimbi alisema baadhi ya wanachama wameanza kampeni kabla ya muda rasmi kwa kutumia mbinu kama kuanzisha mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs), kufadhili matukio ya kijamii kama kumbukumbu za misiba na sherehe za ndoa, pamoja na kushinikiza vikao vya chama kuwapitisha bila kupingwa. “Tayari tumeshuhudia baadhi ya wabunge na madiwani wakitafuta mbinu za kuhakikisha wanapitishwa bila kupingwa. Wengine wanahamasisha matamko ya vikao, huku baadhi wakihudhuria matukio yenye lengo la kujitambulisha mapema kwa wapiga kura. Wapo wanaowapa posho wahudhuriaji wa miku...