Skip to main content

Posts

Showing posts from November 26, 2024

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ashiriki katika zoezi la Uchaguzi wa Serikali za Mitaa

  Rais Dkt.Samia, amepiga kura katika Kituo cha Kitongoji cha Sokoine, Kijiji cha Chamwino Dodoma, akiungana na mamilioni ya Watanzania kwenye maeneo mbalimbali ya nchi kutumia haki yake ya Kikatiba siku ya leo Novemba 27, 2024 kupiga kura ya kuchagua viongozi wa Serikali za Mitaa.

Wananchi Wachagua Viongozi wa Serikali za Mitaa-Dkt. Biteko

📌 *DKT. Biteko apongeza Wananchi Kujitokeza kwa wingi* 📌*Awahimiza kujitokeza kuwachagua viongozi* Watanzania katika maeneo mbalimbali ya nchi wamejitokeza kupiga kura kwa ajili ya kuwachagua viongozi wao ngazi ya Serikali za Mitaa. Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko ametimiza haki yake ya Kikatiba katika Kata ya Bulangwa, Wilayani Bukombe, Geita kisha akawashukuru wananchi kwa kujitokeza kwa wingi kupiga kura. Dkt. Biteko amesema hayo leo Novemba 27, 2024 mara baada ya kupiga kura katika kituo cha kupiga kura cha Shule ya Msingi Bulangwa wilayani Bukombe mkoani Geita. “ Zoezi la kupiga kura linaendelea vizuri na wananchi wamejitokeza kwa wingi nawapongeza kwa hilo. Uchaguzi wa mwaka huu umekuwa tofauti kwa sababu ya hamasa kubwa ya kushiriki,” amesema Dkt. Biteko. Amesisitiza “ Ninaomba watu wote waliojiandikisha watumie haki yao ya kikatiba kwa kujitokeza kwa wingi na kwenda kupiga kura,” Kampeni za uchaguzi wa Serikali za Mitaa zilizinduliwa Novemba 20, ...

Waziri Mkuu apiga Kura Kijijini Kwake Nandagala

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Novemba 27, 2024 ameshiriki katika zoezi la upigaji kura kuchagua viongozi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji, kwenye kituo cha Shule ya Msingi Nandagala, Ruangwa, Lindi Novemba 27, 2024. Akizungumza baada ya kupiga kura ambapo aliongozana na Mkewe Marry Majaliwa, Waziri Mkuu amewapongeza wakazi wa eneo hilo kujitokeza kwa wingi kuchangua viongozi katika uchaguzi huo unaofanyika nchi nzima. “Wananchi wamejitokeza kwa wingi, tayari mimi na familia yangu tumepata nafasi ya kumchagua kiongozi ambaye tunaamini atatuletea maendeleo kwenye kijiji chetu”.

Ccm Kwangwa B Yawanadi Wagombea wake kwa Kishindo

Na Ada Shadrack,Musoma. MGOMBEA nafasi ya mwenyekiti mtaa wa Kwangwa B' kata ya Kwangwa Manispaa ya Musoma Maxmilian Kunju kwa tiketi ya CCM amewahaidi wananchi kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo tatizo la uhaba wa maji linalowakabili wakazi wa mtaa huo. Awali eneo hili kulikuwa na changamoto ya ukosefu wa maji safi na salama lakin tulivyoingia  madarakani mwaka 2019 tuliamua kupunguza bugudha hiyo akina mama mlikuwa mkienda  kuchota maji kwenye visima "amesema Kunju. Aidha aidha mbali na changamoto hiyo kunju alisema baadhi ya miundombinu ya barabara zilikuwa ni njia za ng'ombe, na  mashamba lakini kwa sasa uongozi wa chama hicho mkoani Mara umetengeneza barabara na kuleta maji safi na salama kupitia mabomba.

Jitokezeni Kupiga Kura-Majaliwa

*_Asisitiza kuwachagua wagombea wa CCM_* WAZIRI MKUU na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Kassim Majaliwa amewahimiza Wana-Liwale na Watanzania kwa ujumla kujitokeza kwa wingi kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 27, 2024 nchi nzima na kuwachagua wagombea wote wa Chama cha Mapinduzi. Amesema hayo leo (Jumanne, Novemba 26, 2024) wakati alipofunga kampeni za uchaguzi wa Serikali za Mitaa zilizofanyika katika viwanja vya ujenzi, Liwale Mkoani Lindi. Amesema kwa kufanya hivyo ni kutimiza haki ya msingi katika kuwachagua viongozi watakaowatumikia katika kipindi cha miaka mitano “Huu ni wakati muhimu wa kufanya uchaguzi wa viongozi bora ambao wataleta maendeleo ya kweli, nendeni mkachague viongozi waliowekwa na CCM” Amesema kuwa CCM inaamini kwa kuwachagua viongozi wa chama hicho itawawezesha kuwa na viongozi wa kipekee, wanaojali na wanaohakikisha kuwa uwajibikaji na maendeleo vinapatikana kwa kila mwananchi.  “Hivyo basi, t...

Rhobi Samwelly Ahawahimiza Wananchi Serengeti Kuwachagua Viongozi wa CCM November 27, 2024

  Fresha Kinasa, Mara.  MJUMBE wa Baraza Kuu la UWT Taifa Mkoa wa Mara  Ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Siasa Mkoa huo Rhobi Samwelly amewahimiza Wananchi wa Wilaya ya Serengeti kuhakikisha wanatekeleza wajibu wao  bila  kufanya makosa  kwa kuwapigia kura Wagombea wa Chama cha Mapinduzi katika uchaguzi wa serikali za mitaa Novemba 27, 2024.  Ameyasema hayo Novemba 26, 2024 wakati wa kuhitimishwa kwa kampeni za kuwanadi wagombea wa nafasi za Uenyekiti wa Vitongoji vya kata ya Stendi Kuu  zilizofanyika katika Kitongoji cha Bomani Wilayani humo.     Amesema, maendeleo ya kweli yanafanywa na chama Cha Mapinduzi kupitia Viongozi wake wakitekeleza ilani ya chama hicho ambayo  inagusa kila sekta. Hivyo  Wananchi watimize wajibu wao wa Kuwachagua Viongozi wa chama hicho kusudi waendelee  kuleta  maendeleo katika maeneo yao.  "Kesho tunapiga kura mjitokeze kwa wingi sana, niwaombe Wananchi wote  msifanye makos...

Mpc yahimiza Waandishi wa Habari kupewa Ushirikiano Wakati wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa

Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mwanza(MPC)imehimiza Waandishi wa Habari Kupewa Ushirikiano wakati wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Novemba 27 Mwaka huu. Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa Mpc Edwin Soko katika Taarifa yake kwa Umma. ‘’Mpc imetoa rai kwa wadau wa uchaguzi mkoa wa mwanza kuwapa ushirikiano wa kutosha waandishi wa habari wote watakaokuwa kwenye mbalimbali wakitekeleza majukumu yao,Kwa kuwa Waandishi wa habari wana wajibu wa kikatiba wa kutafuta,kuchakata na kutoa taarifa kwa umma kupitia ibara ya 18 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania’’ilieleza Taarifa ya Soko. Mwenyekiti huyo wa Mpc ameeleza matarajio yake kuwa wadau wote wa uchaguzi watatoa ushirikiano wa kutosha kwa waandishi wa Habari huku akilikumbusha Jeshi la polisi kuendelea kuwalinda raia wote wakiwemo wanahabari wanapotimiza majukumu yao. Aidha amewataka waandishi wa habari kuvaa Press Jackets(Vizibao)ili waweze kutambuliwa kwa urahisi na wadau watakapokuwa wanatekeleza majukumu yao 

Geita Msiniangushe, Msiiangushe Ccm-Dkt. Biteko

*📌Awahimiza Wananchi Kupiga Kura Kesho, Kuchagua CCM* *📌 Awapongeza kwa Kampeni za Zakistaarabu* *📌 Ataka Siasa Ziwe Daraja la Kuunganisha na Kushindanisha Mawazo* Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa ambaye pia ni Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewataka wananchi wa Geita kujitokeza wa wingi kesho na kuchagua wagombea wa CCM. Amewahimiza wananchi hao kuendelea kumuunga mkono yeye na CCM ili kutoa fursa ya kuendeleza jitihada za maendeleo “Nimekuja hapa kuwaambia msiniangushe wala kuiangusha CCM kwa kuwa miradi na juhudi zote zinazoendelea zinalenga kuleta maendeleo kwenu,”  Dkt. Biteko amesema hayo leo Novemba 26, 2024 wakati akifunga Kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa Mkoa wa Geita zilizofanyika katika Uwanja wa Mwenge, Uyovu, wilayani Bukombe. Ameongeza kuwa kampeni za 2024 zimekuwa za kistaarabu huku akiwashukuru wanachama wa CCM kwa kuendeleza kauli mbiu ya Rais Samia ya kujenga Taifa moja la k...

Tumewaletea Majembe Msifanye Makos-Majaliwa

*_Asema CCM ni Chama Imara_ WAZIRI MKUU na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Kassim Majaliwa amewataka Wana-Liwale kuwachagua wagombea wote wa Chama cha Mapinduzi kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa kuwa Chama hicho kimechagua majembe. Amesema kuwa kama ilivyo kwa uimara wa Chama cha Mapinduzi (CCM) chini ya uongozi imara wa mwenyekiti wake, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kilichagua wagombea wazuri wenye uwezo wa kusimamia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ili kuwaletea Watanzania maendeleo. Amesema hayo leo (Jumanne, Novemba 26, 2024) wakati alipofunga kampeni za uchaguzi wa Serikali za Mitaa zilizofanyika katika viwanja vya ujenzi, Liwale Mkoani Lindi. “Tunawaleta hawa viongozi wapigieni kura ili wakasimamie na kuendeleza yaliyomo kwenye ilani, hawa wanaweza na ndio maana tumewaleta mbele yenu, viongozi hawa ni muhimu kwasababu watawaunganisha na viongozi wa Serikali, Sina Mashaka na Wagombea wetu” Amesema kuwa kupitia utekelezaji wa Ila...