Mkuu wa Wilaya ya Chato, Louis Peter Bura, amewataka wananchi kuacha tabia ya kusubiri umeme ukatike ndipo wakalalamike, bali washikamane na TANESCO kulinda miundombinu ya umeme kama mali yao. Bura ametoa wito huo leo Septemba 29, 2026, mara baada ya kutembelea banda la TANESCO katika Maonesho ya 9 ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea Geita. "Elimu ni muhimu. Mwananchi akiona nguzo imeegama, waya umeanguka, au mtu anachimba karibu na nguzo, atoe taarifa mapema. Kulinda miundombinu ya umeme ni kulinda maendeleo yetu," alisema Bura. Amepongeza hatua ya TANESCO ya kidijitali ya kutumia vikundi vya mawasiliano vya WhatsApp na mifumo ya teknolojia ya mawasiliano ya kikanda. Amesema sasa mwananchi hahitaji kupanda daladala kufika ofisini, anawasilisha kero yake kwenye kundi na inatatuliwa haraka. "Tangu kuanzishwa kwa makundi haya, malalamiko yamepungua kwa kiasi kikubwa. Hii ndiyo TANESCO tunayoitaka," alisema. Katika angle nyingine, Bura ameunganisha suala la umeme na ...
Marato tv - Sauti ya Jamii