Skip to main content

Posts

Showing posts from November 3, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

NDEJEMBI: URITHI WA HAYATI SITTA UWE MWONGOZO WA UONGOZI BORA

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi, amewataka viongozi nchini kuenzi na kuendeleza urithi wa aliyekuwa Spika wa Bunge, Hayati Samuel John Sitta, kwa kuzingatia misingi ya uadilifu, uwajibikaji, uzalendo na utumishi uliotanguliza maslahi ya Taifa. Amesema uongozi wa Hayati Sitta unapaswa kuwa somo kwa viongozi wa sasa na vizazi vijavyo katika kujenga taasisi imara, kulinda misingi ya demokrasia na kuhakikisha dhamana wanazopewa zinatumika kwa manufaa ya wananchi. Ndejembi ametoa wito huo Novemba 3, 2026, katika Ukumbi wa Bunge jijini Dodoma, alipomwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika kumbukizi ya miaka 10 ya kifo cha Hayati Sitta na uzinduzi wa kitabu kinachoelezea maisha yake na safari ya uongozi. Amesema Hayati Sitta alikuwa kiongozi aliyeweka mbele maslahi ya Taifa, akasimamia heshima na hadhi ya Bunge pamoja na kuzingatia taratibu, kanuni na misingi ya uwajibikaji katika utekelezaji wa majuk...

MBUNGE WAITARA ASIKITISHWA NA WIZI WA KUTISHA KATIKA MIRADI ILIYOKAGULIWA NA CAG

  Mbunge wa Jimbo la Tarime Vijijini, Mhe. Mwita Waitara, amesema amesikitishwa na wizi na matumizi yasiyo sahihi ya fedha za umma zilizobainishwa katika baadhi ya miradi na taasisi za Serikali kupitia ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), akitaka watendaji waliohusika kuwajibishwa. Akichangia taarifa za Kamati za Bunge kuhusu ripoti za CAG, Novemba 3, 2026, jijini Dodoma, Waitara amesema ukaguzi huo umebainisha changamoto mbalimbali ikiwemo matumizi ya fedha yasiyozingatia taratibu, mapungufu katika mikataba na manunuzi, pamoja na malipo yanayohitaji ufafanuzi kutoka kwa watendaji waliopewa dhamana ya kusimamia rasilimali za umma. Amesema miongoni mwa maeneo yanayohitaji ufuatiliaji ni Mlimani City, ambako kuna hoja zinazohusu usimamizi wa mapato, ulipaji wa kodi na utekelezaji wa mikataba, akitaka Serikali kuweka wazi namna eneo hilo linavyosimamiwa na kuhakikisha mapato yanayostahili yanakusanywa kwa mujibu wa sheria. “Ukiangalia Mlimani City, kuna masw...

BALOZI LEILA BHANJI AAINISHA HATUA NNE ZA KUWAWEZESHA WANAWAKE UKANDA WA MAZIWA MAKUU

 Na Mwandishi Maalum, Dar es Salaam, Novemba 3, 2026 Balozi Leila Bhanji, Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi, Uwajibikaji na Mahusiano wa Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT), ameainisha hatua nne madhubuti za kuwawezesha wanawake, wakati Tanzania ikiandaa Mkutano wa Wabunge Wanawake wa Mabunge ya Ukanda wa Maziwa Makuu unaofanyika Novemba 2 hadi 5, 2026, katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam. Akizungumza wakati wa kikao cha Sura ya 36 ya Ajenda ya Wanawake, Amani na Usalama, Balozi Bhanji alisema dhamira ya uongozi wa wanawake lazima itoke kwenye ahadi za maneno na hotuba za adabu na kuwa vitendo halisi. Alipinga mtazamo unaowaonyesha wanawake kama wahanga tu wa migogoro. Alisema kwa muda mrefu dunia imekuwa ikiwaonyesha wanawake kama wahanga tu wa vita, lakini huo sio sisi ni nani. Wanawake si wahanga. Wanawake ni wajenzi wa amani, ni wasuluhishi, ni waamuzi na ni walinzi wa kweli wa maliasili. Balozi Bhanji aliangazia uhu...

AMBASSADOR LEILA BHANJI OUTLINES FOUR STEPS TO EMPOWER WOMEN IN GREAT LAKES REGION

 By Special Correspondent, Dar es Salaam Ambassador Leila Bhanji, Director of the Department of Management, Accountability, and Relations for the Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT), has outlined four concrete steps to empower women, as Tanzania hosts the Conference of Women Parliamentarians of the Great Lakes Region Parliaments from November 2 to 5, 2026, at the Julius Nyerere International Convention Centre in Dar es Salaam. Speaking during the session on Chapter 36 of the Women, Peace and Security Agenda, Ambassador Bhanji said the commitment to women's leadership must move beyond mere promises and polite speeches and become concrete action. She challenged the narrative that paints women only as victims of conflict. She said for a long time, the world has painted women as mere victims of conflict, but that is not who we are. Women are not victims. Women are peace builders, mediators, decision makers and the true guardians and protectors of natural resources. Ambassado...

WAITARA AITAKA SERIKALI KUHARAKISHA UTOAJI WA VIFAA TIBA VITUO VYA AFYA TARIME

MBUNGE wa Jimbo la Tarime Vijijini, Mheshimiwa Mwita Waitara, amehoji Serikali kuhusu hatua na muda wa kupeleka vifaa tiba katika vituo vya afya vilivyokamilika kujengwa katika maeneo ya vijijini ya Mtaa, Umera, Magoma na Yuyahanja, ili wananchi waanze kunufaika na huduma za afya katika maeneo yao. Akizungumza Bungeni wakati wa kipindi cha maswali na majibu Leo Novemba 3,2026, Mheshimiwa Waitara amesema kukamilika kwa ujenzi wa majengo ya vituo vya afya pekee hakutoshi kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora, bali kunahitajika pia vifaa tiba na wataalamu wa afya watakaowezesha utoaji wa huduma hizo. Amesisitiza kuwa wananchi wamekuwa wakisubiri kwa hamu vituo hivyo kuanza kutoa huduma, hivyo ni muhimu Serikali kuhakikisha vifaa tiba vinapelekwa kwa wakati ili majengo hayo yaweze kutumika kwa lengo lililokusudiwa. Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Afya Dkt.Florence Samizi amesema Serikali inatambua umuhimu wa hatua hiyo, akieleza kuwa baada ya kukamilika kwa ujenzi wa vituo vya afya...

ETHIOPIA YAKAMILISHA MOJA YA MIFUMO MIKUBWA ZAIDI YA UMEME WA MAJI BARANI AFRIKA

Nchi ya Ethiopia imeweka historia katika sekta ya nishati barani Afrika kupitia mradi mkubwa wa kuzalisha umeme kwa kutumia nguvu ya maji unaojulikana kama Grand Ethiopian Renaissance Dam (GERD). Mradi huo umejengwa katika Mto Blue Nile, nchini Ethiopia, ukiwa na uwezo wa kuzalisha umeme wa hadi megawati 5,150 (MW), na kuufanya kuwa mradi mkubwa zaidi wa umeme wa maji barani Afrika kwa uwezo wa uzalishaji. Bwawa hilo lina urefu wa takribani mita 1,800 na kimo cha mita 170, huku likiwa na uwezo wa kuhifadhi maji kiasi cha takribani mita za ujazo bilioni 74. Kupitia mradi huo, Ethiopia inalenga kuongeza upatikanaji wa umeme kwa wananchi wake, kukuza shughuli za kiuchumi na kuuza nishati hiyo kwa nchi nyingine za Afrika. Mradi huu pia una umuhimu mkubwa katika maendeleo ya miundombinu ya nishati barani Afrika, hasa katika kipindi ambacho nchi nyingi zinaendelea kutafuta vyanzo vya uhakika vya umeme vinavyotokana na nishati jadidifu. Hata hivyo, ujenzi wa bwawa hilo umekuwa ukizua mijadala...

TANZANIA, UAE VOW CLOSER COORDINATION IN GENEVA-BASED UN BODIES

 By Prosper Makene  The Deputy Permanent Representative of the United Republic of Tanzania to the United Nations Office in Geneva, Ambassador Dr. Hoyce Temu, held a bilateral meeting with the Deputy Permanent Representative of the United Arab Emirates (UAE), Ms. Shahad Matar, earlier today. The meeting, which took place at the UAE Mission in Geneva, was held in a warm and cordial atmosphere reflecting the excellent and growing bilateral relations between Tanzania and the UAE. Central to their discussion was the strengthening of multilateral cooperation between the two countries in Geneva. Both Ambassadors underscored the importance of continued collaboration and mutual support within the various international organizations and mechanisms based in Geneva, including the UN Human Rights Council, and other humanitarian and development bodies. A key agenda item was the upcoming Universal Periodic Review (UPR) session. Ambassador Dr. Temu briefed her counterpart on Tanzania's prepar...