Na Bwanku M Bwanku. Leo Januari 27, 2025 Taifa letu linasherehekea miaka 65 toka kuzaliwa kwa Rais wa sasa wa Awamu ya 6 wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, anayehudumu kwa mara ya kwanza kwenye nyadhifa ya juu kabisa nchini toka achukue mikoba hiyo Machi 19, 2021 baada ya kifo cha aliyekuwa Rais wa Awamu ya 5 Hayati John Pombe Magufuli. Kwa wasiyemfahamu sana, Rais Samia, ndiye Mwanamke wa kwanza katika historia ya Tanzania kushika nafasi ya Urais wa Tanzania baada ya pia kuwa Mwanamke wa kwanza kushika nafasi ya Makamu wa Rais mwaka 2015 hadi 2021, nafasi kuu za juu kabisa katika Taifa letu. Rais Samia Suluhu Hassan alizaliwa Januari 27, 1960 katika Kijiji cha Kizimkazi kilichopo Jimbo la Makunduchi, Wilaya ya Kusini, Mkoa wa Kusini Unguja Visiwani Zanzibar, kabla ya kuanza masomo yake ya Msingi katika shule mbalimbali ikiwemo Shule ya Msingi Chwaka kuanzia mwaka 1966 hadi 1968, kisha Ziwani mwaka 1970 na baadae Shule ya Msingi Mahonda mwaka 1972. Baadae...
Marato tv - Sauti ya Jamii