Skip to main content

Posts

Showing posts from October 16, 2024

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Comoro yatafuta fursa za ushirikiano na miji ya Tanzania

Balozi wa Tanzania nchini Comoro,Saidi Yakubu,amekutana na Rais wa Umoja wa Mameya Nchini Comoro,Nassuf Ahmed Abdallah ambaye amemueleza kuwa wangependa kuona ushirikiano wa miji ya Comoro na Tanzania. Mheshimiwa Abdallah ambaye pia Meya wa Mji wa Domoni uliopo katika Kisiwa cha Anjouan amesema ushirikiano huo wa miji ya Comoro na Tanzania utafungua fursa za kiuchumi kwa kuwa tayari kuna uhusiano mkubwa wa kijamii na kihistoria baina ya raia wa nchi hizo mbili na kuongeza kuwa kwa upande wa Domoni wangependa kuwa na ushirikiano na Manispaa ya Mji wa Mtwara ambao tayari wamewahi kufanya ziara huko siku za nyuma. Kwa upande wake,Balozi Yakubu alimhakikishia kuwa ombi hilo atalifikisha Tanzania ili lifanyiwe kazi na kusifu ushirikiano anaoupata kutoka kwa Mameya wa Miji mbali mbali anapoitembelea na kuongeza kuwa uhusiano wa miji utasaidia pia kuongeza ushirikiano wa kidiplomasia uliopo baina ya nchi hizo mbili.

Zaidi ya wakulima mia mbili Kagera wanufaika na elimu ya mbinu bora za kilimo cha Umwagiliaji

NA MWANDISHI WETU;NIRC KAGERA Serikali ina mpango wa kujenga soko la kisasa la ndizi  Mkoani Kagera ili kuwasaidia wakulima Mkoani humo kupata bei nzuri ya mazao yao. Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa Kilimo David Silinde wakati wa kuhitimisha Maonesho ya wiki ya chakula duniani yaliyofanyika kitaifa mkoani kagera.  Silinde pia amewataka washiriki wote wa maonyesho hayo kuzingatia mambo waliyojifunza ili kuboresha uzalishaji na hivyo kuwa na uhakika wa chakula na lishe kwa jamii. Awali Naibu Waziri Silinde ametembelea mabanda ya washiriki wa maonyesho hayo likiwemo banda la Tume ya Taifa ya Umwagiliaji  na na kusifu hatua zinazochukuliwa katika utekelezaji wa miradi. Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Uendeshaji kutoka Tume  ya Taifa ya Umwagiliaji Salome Njau, amesema kuwa maonyesho hayo yamekuwa na mafanikio makubwa kwa upande wa Tume hiyo.  Salome amesema kuwa wameweza kuhudumia wakulima zaidi ya 200 na kutoa elimu ya  mbinu bora za kilimo ...

Waziri mkuu amwakilisha Rais Dkt.Samia maziko ya Baba wa Katibu mkuu kiongozi

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa leo Oktoba  16, 2024 amemwakilisha Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika maziko ya Mzee Jeremiah Kusiluka ambaye ni Baba mzazi wa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka yaliyofanyika katika kijiji cha Madihani, Makete mkoani Njombe. Akitoa salamu za Mheshimiwa Rais Dkt. Samia, Waziri Mkuu amesema  Mheshimiwa Rais Dkt. Samia ametoa wito kwa wanafamilia, ndugu na waombolezaji wawe watulivu katika kipindi hiki kigumu za msiba huo na waendelee kumuombea marehemu Mzee Jeremiah ili Mwenyezi Mungu amlaze mahali pema peponi.  Aidha, Mheshimiwa Majaliwa ametoa wito kwa wanafamilia, ndugu na waombolezaji kuyaenzi mema yote aliyoyafanya marehemu kipindi cha uhai wake. “Tuenzi yale yote mema aliyoyafanya mzee wetu Jeremiah wakati wa uhai wake, tukifanya hivyo tutakuwa tumetenda haki. ” Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amesema kuwa Makamu wa Rais Dkt. Philip Isdor Mpango na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Huss...

Wizara ya madini kurejesha minada ya ndani na kimataifa madini ya vito

●Itafanyika ndani ya nchi na nje ya nchi ●Itaendeshwa na Tume ya Madini kushirikiana na Soko la Bidhaa Tanzania ●Marekebisho ya Sheria na Kanuni yakamilika ⚫️ Ni utekelezaji wa Rais Samia kukuza biashara ya Tanzanite *Dodoma* Serikali kupitia Wizara ya Madini inarudisha minada ya ndani ya madini ya vito itakayofanyika katika maeneo ya uzalishaji hususan Mirerani, Mahenge, Tunduru, Dar es salaam, Arusha na Tanga na kimataifa itafanyika mji wa Bangkok na Jaipur nchini Thailand. Hayo yamesemwa leo Oktoba 16, 2024 na Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde wakati akijibu hoja mbalimbali zilizoibuliwa na wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Nishati na Madini jijini Dodoma.  Waziri Mavunde amesema kuwa baada ya taratibu za marekebisho ya kisheria kukamilika juu ya uendeshaji wa minada hiyo wanatarajia ndani ya muda mfupi ujao kuanza taraibu za kuweka miundombinu ya kuanza minada ya ndani. Waziri Mavunde amefafanua kuwa, uendeshaji wa maonesho na minada ya kimataifa nchini ni fursa muhim...

Serikali yaweka mkazo kukuza tasnia ya ufugaji wa kuku

📌 Vijana Wahimizwa Kujiajiri Kupitia Ufugaji Kuku 📌 Dkt. Biteko Atoa Maagizo kwa Wizara ya Mifugo Kukuza Tasnia ya ufugaji wa Kuku 📌 Watanzania Wahimizwa Kufuga Kibiashara sio Kitamaduni 📌 Mkutano wa Kwanza wa Tasnia ya Kuku na ndege wafugwao Kusini mwa Afrika Wafanyika Tanzania Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa ujio wa Mkutano wa Jukwaa la Tasnia ya Kuku na ndege wafugwao kwa Nchi za Kusini mwa Afrika unadhihirisha  namna Tanzania chini ya uongozi wa Rais Mhe. Dkt.  Samia ilivyokuwa na mahusiano mazuri ambayo yamefungua milango katika sekta mbalimbali ikiwemo ya tasnia ya kuku na ndege wafugwao. Amesema hayo leo Oktoba 16, 2024 jijini Dar es salaam wakati akimwakilisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Isdory Mpango katika ufunguzi wa mkutano huo. Ametaja faida za ufugaji kuku na ndege wafugwao kuwa ni pamoja na kuchangia usalama wa chakula na kuongeza ...

Rais Mwinyi:Smz imeweka kipaumbele cha maendeleo ya jamii

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi, amesema Serikali imeweka kipaumbele kwenye maendeleo ya jamii endelevu, ikiwemo ujenzi wa nyumba za bei nafuu na kuhakikisha upatikanaji wa huduma muhimu za maji safi, usafi wa mazingira, na umeme. Rais Dk. Mwinyi ameyasema hayo katika Hoteli ya Melia, Kiwengwa, Mkoa wa Kaskazini Unguja, kwenye mkutano wa mwaka wa pamoja kati ya Umoja wa Afrika na Jumuiya za Taasisi zinazojishughulisha na mikopo ya nyumba kutoka nchi za Umoja wa Afrika (AUHF). Aidha, Rais Dk. Mwinyi ameongeza kuwa Serikali imepiga hatua kubwa za kukabiliana na mahitaji ya makazi ya watu wanaoongezeka siku hadi siku, kwa kuzingatia uwezo wa kumudu gharama za nyumba na makaazi endelevu. Rais Dk. Mwinyi amezisihi taasisi hizo kutoa mikopo nafuu ili wananchi waweze kumudu gharama za nyumba kwa urahisi. Ameeleza kuwa Serikali, kupitia Shirika la Nyumba la Zanzibar (ZHC), imeweka mipango kadhaa ya kuinua upatikanaji wa nyumba za bei nafuu, ha...