▪️Ni cha Kampuni ya Madini ya Shenghe ambacho ujenzi wake umeanza ▪️Madin ya mchanga mzito kutoka nchi mbalimbali Afrika kuchakatwa Pangani,Tanga ▪️Waziri Mavunde apongeza hatua ya kuifanya Tanzania kitovu cha uongezaji thamani madini Afrika ▪️Awataka wawekezaji kukamilisha ujenzi wa kiwanda mapema ▪️Rais Samia apongezwa kwa mazingira rafiki ya uwekezaji Chengdu,China Kampuni ya Shenghe Resources ya China imeanza ujenzi wa kiwanda kikubwa cha kuchakata madini madini ya mchanga mzito wa baharini (𝙃𝙚𝙖𝙫𝙮 𝙈𝙞𝙣𝙚𝙧𝙖𝙡 𝙎𝙖𝙣𝙙𝙨) katika eneo la Tajiri,Wilaya ya Pangani Mkoani Tanga ambapo kampuni hii inatekeleza mradi mkubwa wa uchimbaji wa madini tembo. Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Shenghe Ndg. Xie Bing wakati wa ziara ya Waziri wa Madini Mh. Anthony Mavunde kutembelea na kujionea shughuli mbalimbali za uongezaji thamani madini zinazofanywa kampuni hiyo. Akizungumza katika ziara hiyo Ndg. Bing amesema kwa Bara la Afrika wana miradi ya madin...
Marato tv - Sauti ya Jamii