Skip to main content

Posts

Showing posts from September 26, 2024

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Rais samia azindua soko la madini ya vito na dhahabu tunduru

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amezindua Soko la Madini ya Vito na Dhahabu Wilayani Tunduru ikiwa ni moja ya shughuli alizofanya akiwa katika ziara ya kikazi ya siku 6 Mkoani Ruvuma. "Kwa dhati kabisa, napenda kuipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru kwa utekelezaji wa Sera ya kushirikiana na sekta binafsi yaani Public Private Partnership kwa vitendo ambapo Serikali imeweka fedha kiasi na kiasi kingine kimechangiwa na wafanyabiashara wa madini waliopo hapa  Wilayani Tunduru" "Ni dhahiri kwamba ujenzi wa soko hili kubwa na la kisasa utarahisisha biashara ya madini Wilayani hapa na kuongeza ufanisi katika ukusanyaji maduhuli ya Serikali sambamba na kudhibiti udanganyifu na utoroshaji wa madini", alibainisha Mhe. Rais. Aidha, Rais Samia ameonesha wazi kufurahishwa na ushirikiano huo wa Halmashauri na Sekta binafsi na kusisitiza kwamba Sera ya PPP ikitelezwa kwa vitendo ni chachu ya maendeleo ya wananchi katika Wilaya zote nchini. Pi...

Mtandao wa kutokomeza ndoa za utotoni Tecmn wafanya ziara shinyanga

Na Elizabeth Cornely,SHINYANGA Wadau kutoka mashirika ya Kutokomeza Ndoa za Utotoni Tanzania(TECMN), umetembelea kituo kinachofanya kazi ya kuokoa, kulea na kuwaendeleza watoto wa kike ambao wamekumbwa na madhila ya ukatili na kukatisha masomo kwa mimba na ndoa za utotoni kilichopo katika Kata ya Chibe wilaya ya Shinyanga mkoani Shinyanga. Wadau kutoka katika mashirika hayo zaidi 80 wamewakilishwa na machache kutoka Msichana Initiative, Medea, Plan International, My Lagacy, Binti Makini Foundation na Theatre Arts Feminist Group, ikiwa ni sehemu ya ziara yao wanayoifanya katika mikoa minne ya Mara, Shinyanga, Tabora na Dodoma. Mratibu wa Mtandao huo, Lilian Kimati, anasema wameamua kutembelea kituo hicho ili kusikiliza na kushuhudia maisha wanayoishi mabinti hao waliokumbwa na madhila ya ukatili na kuona namna ya kutoa mchango wao. Mlezi wa kituo hicho kinachojulikana kama Agape Knolwedge Open School, anasema kwa mwaka anapokea wasichana zaidi ya 50 waliopata mimba za utotoni na wale ...

Rais Samia aondoa giza jimbo la prof.Muhongo

Na Shomari Binda-Musoma MKUU wa Wilaya ya Musoma Juma Chikoka amemshukuru Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuling'arisha jimbo la Musoma vijijini kwa mwanga wa taa za barabarani. Shukrani hizo amezitoa jana septemba 25 mara baada ya kukitembelea usiku Kijiji cha Suguti kilichopo kwenye jimbo hilo. Amesema kufungwa na kuwashwa taa za barabarani kumewezesha wananchi kuendelea kufanya shughuli zao za kiuchumi hadi usiku. Amesema Rais Dkt.Samia ameendelea kufanya kazi kubwa katika kuhakikisha wananchi mjini na vijijini wanafanya shughuli za kiuchumi mchana na usiku kwa usalama. Chikoka amesema wananchi wa Kata na Kijiji cha Suguti wameonyesha furaha kwa kupata mwanga wa taa barabarani na kufanya biashara hadi usiku. Mkuu huyo wa Wilaya amesema hilo ni jambo kubwa lililofanywa na Rais Dkt.Samia na sio la kuacha kushukuru. " Hapa sio daraja la Tanzanite jijini Dar es salam bali ni Kijiji cha Suguti jimbo la Musoma vijijini limeng'aa na kuwaka. " Sasa wananchi wanafanya shug...

Serikali yakubali ombi la mbunge Mathayo kupandisha hadhi chuo cha veta musoma

 Na Shomari Binda-Musoma SERIKALI kupitia Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia imekubali ombi la mbunge wa jimbo la Musoma mjini Vedastus Mathayo kupandisha chuo cha ufundi Veta Musoma. Ombi la mbunge Mathayo alilitoa bungeni alipouliza swali ni lini Waziri wa Wizara hiyo angefika Musoma na kukitembelea chuo hicho kwaajili ya kukiona chuo hicho na kuona uhitaji wake ili kukipandisha hadhi. Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Juma Omary Kipanga kwa niaba ya Waziri wa Wizara hiyo Profesa Adolf Mkenda leo septemba 26 amekitembelea chuo hicho. Akizungumza chuoni hapo Naibu Waziri huyo amesema wametekeleza ombi la mbunge Mathayo ya kufika chuoni hapo na kupata taarifa juu ya chuo hicho. Amesema taarifa imeeleza mahitaji yanayohitajika kuwepo chuoni hapo ili kukipandisha hadhi na kutoa maelekezo ili yaweze kutekelezwa. Kipanga amesema moja ya mahitaji ni kuongezwa kwa kozi kutoka 9 na kufikia 10 pamoja na kuongezwa kwa madarasa,mabweni,eneo la kupata chakula,jiko pamoja na kalak...

Mradi wa utafiti wa simba chachu ya utalii serengeti

Taarifa za kisayansi  zinazotokana na Mradi wa muda mrefu wa Utafiti  wa SIMBA SERENGETI unaoratibiwa na Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI) kupitia  Kituo cha Utafiti wa Wanyamapori Serengeti, zimekua chachu katika uhifadhi  na kivutio   cha Utalii  ndani ya hifadhi  ya  Taifa  Serengeti. Mradi huu wa SIMBA SERENGETI unafuatilia   idadi, tabia na mienendo ya makundi ya simba kwa zaidi ya miaka 50, ambapo kwa sasa yapo makundi 20 yenye jumla ya simba takribani 300 yanayofuatiliwa. Aidha, Katika mradi  wa SIMBA  SERENGETI utambulisho hufanyika  kwa kila Simba kuandaliwa kadi maalumu  (Lion  identification  card) kwa kutumia alama/madoa ya Kipekee  kwenye  uso eneo la ndevu (Whisker spots) na  alama nyinginezo za asili.Utambulisho huu husaidia kumfuatilia simba mmoja mmoja ndani ya kundi. Aidha matumizi ya teknolojia  yanarahisisha utafiti wa simba ambapo  kwa...

Rais Samia amesema lazima jitihada za kukabiliana na tembo ziendelee

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema Serikali imeendelea na mikakati mbalimbali ya kukabiliana na wanyamapori tembo katika Halmashauri za Wilaya ya Namtumbo na Tunduru Mkoani Ruvuma lengo ikiwa ni kuzuia wasiingie kwenye makazi ya watu. Ameyasema hayo leo Septemba 26, 2027 alipokuwa akizungumza na wananchi katika uwanja wa CCM Tunduma Mkoani Ruvuma. “Kwa upande wa wanyama tembo Serikali tumeanza kuchukua hatua, kwanza tumeweza kuongeza askari ambao wako katika maeneo mbalimbali lakini pia kuna askari wa vijiji wanaosaidiana na askari hawa kuhakikisha tembo hawaingii kwenye makazi ya watu” amesisitiza Rais Samia. Ameongeza kuwa Serikali imeweka magari ya doria katika Wilaya ya Namtumbo na Tunduru na yanafanya kazi kubwa ya kukabiliana na tembo. Aidha, amesema Serikali imeweka ndege nyuki “drones” kwa ajili ya kufukuza makundi ya tembo ikiwa ni hatua za awali lakini Serikali itaendelea na jitihada nyingine za kukabiliana na tembo, lengo iki...

Waziri Mkuu afungua Mjadala juu ya mifumo jumuishi ya kifedha nchini Marekani

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametoa wito kwa wadau wa maendeleo washirikiane kikamilifu na nchi zinazoendelea katika kusaidia utekelezaji wa mifumo jumuishi ya kifedha. Ametoa wito huo jana (Septemba 25, 2024) wakati akifungua mjadala kuhusu  miaka 15 ya  mafanikio katika masuala ya Mfumo Jumuishi wa Fedha kwa Maendeleo kwenye mkutano ulioitishwa na Malkia wa Uholanzi, Mhe. Maxima ambaye ni mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika Huduma Jumuishi za Fedha, Jijini New York, Marekani Amesema kuwa uchumi jumuishi ni muhimu hasa katika utekelezaji wa mpango endelevu wa maendeleo na ufanikishaji wa ajenda 2030.  “Huduma jumuishi za kifedha ni kiungo muhimu cha ukuaji wa uchumi, kupunguza umasikini na kuleta maendeleo ya jamii kwa ujumla.” Aidha, Mheshimiwa Majaliwa amempongeza Malkia Maxima kwa juhudi zake ambazo zimewezesha ongezeko kubwa la ufikiaji wa huduma za kifedha duniani, huku zaidi ya asilimia 50 ya watu wakiwa wamefikiwa na mpango huo katika kipind...

Jeshi la polisi mkoani mwanza lamkamata mmiliki wa Mtumbwi"BUBU"kwa kusababisha

 Jeshi la polisi mkoani mwanza linawashikilia watu watatu kwa tuhuma za kusafirisha abiria kwa kutumia mtumbwi bubu uliopata ajali na kusababisha vifo vya watu wawili na majeruhi 29. Wanaoshikiliwa na Jeshi hilo ni mmiliki wa mtumbwi huo Amon Lutabanzibwa,Nahodha wa Mtumbwi Robert kabota na Msimamizi wa Mtumbwi Salum Shaban wote wakazi wa Jijini Mwanza.  Kamanda wa polisi mkoa wa mwanza,Naibu kamishna wa polisi Wilbroad Mutafungwa amesema kuwa watuhumiwa hao wanaendelea kuhojiwa kuhusiana na tukio hilo baada ya Mtumbwi uliopinduka na kuzama kubainika kutokuwa na usajili wa kubeba abiria kutoka shirika la uwakala wa meli Tanzania(TASAC)  Ajali hiyo ilitokea septemba 25 mwaka huu majira ya saa kumi na moja za jioni katika mwalo wa bwiru wilayani ilemela wakati mtumbwi MV SEA FALCON wenye namba za usajili TMZ 012212 Ukisafirisha abiria na mizigo kutoka mwalo wa kirumba kwenda kisiwa cha Goziba kilichoko kwenye ziwa Victoria wilayani Muleba Mkoani Kagera.  Waathirika ...

Rais Dkt Samia atoa onyo kwa wananchi wanaochoma misitu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameonya wananchi kuacha tabia ya kuchoma misitu bali wailinde na kuihifadhi. Ameyasema hayo leo Septemba 26, 2024 katika Wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma alipokuwa akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara. "Acheni kuchoma misitu moto,  na kama ni lazima uchome moto shamba linda moto usitapakae kwenda kuharibu maeneo mengine ya misitu yaliyohifadhiwa" amesisitiza Rais Samia. Amesema wananchi wanapochoma misitu moto inaharibu misitu pamoja na miundombinu ya barabara hivyo inarudisha nyuma maendeleo. Kuhusu changamoto ya tembo iliyowasilishwa na Mbunge wa Jimbo la Namtumbo, Mhe. Vita Kawawa, Rais Samia amesema changamoto hiyo inaendelea kupatiwa  ufumbuzi na Wizara ya Maliasili na Utalii chini ya Waziri Mhe. Balozi, Dkt. Pindi Chana. J