Skip to main content

Posts

Showing posts from July 2, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

ASIA ABDALLAH AWAHIMIZA WANACHAMA KUSHIKAMANA, KUEPUKA MAJUNGU NA MIGAWANYIKO

 MJUMBE wa Baraza Kuu la Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) kutoka Mkoa wa Dodoma, Asia Abdallah, amewataka wanachama wa Umoja wa Leo Yetu Kesho Yetu kudumisha mshikamano, uaminifu na ushirikiano, huku akisisitiza kuepuka majungu, ubinafsi na migawanyiko inayoweza kudhoofisha maendeleo ya umoja huo. Akizungumza katika uzinduzi wa umoja huo uliofanyika jijini Dodoma, Asia Abdallah, ambaye pia aliwahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa, amesema mafanikio ya umoja huo yanategemea zaidi mshikamano wa wanachama na utayari wa kufanya kazi kwa pamoja bila kuingiza tofauti za kisiasa, kikabila au kidini. Amebainisha kuwa taasisi za kifedha na mabenki zina nafasi kubwa ya kusaidia vikundi vya kijamii na kiuchumi kukua, lakini akasema mafanikio hayo hayawezi kupatikana iwapo kutakuwa na migogoro ya ndani. “Tunayo kazi ya pamoja na taasisi za kifedha ili kuviinua vikundi hivi. Nasihi muwe kitu kimoja, epukeni majungu, ubinafsi na migawanyiko. Umoja wa kweli unaosimama bila maslahi bina...

AGNES MARWA AIOMBA SERIKALI KUHARAKISHA MIKOPO YA VIZIMBA, AKAZIA BANDARI YA KIRONGWE NA BARABARA YA RORYA

 Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mara, Mhe. Agnes Marwa, amemwomba Waziri Mkuu kuagiza kutolewa kwa haraka mikopo ya programu ya VIZIMBA kwa vikundi vinane vya Wilaya ya Rorya vilivyokamilisha taratibu zote za kupata fedha hizo, akisema hatua hiyo itawawezesha wananchi kujiajiri, kuongeza uzalishaji na kupunguza umaskini. Akizungumza mbele ya Waziri Mkuu katika mkutano wa hadhara uliofanyika wilayani Rorya, Mhe. Marwa amesema vikundi hivyo vimekidhi vigezo vinavyohitajika, hivyo vinasubiri tu fedha ziweze kutolewa ili vianze kutekeleza shughuli za maendeleo na kuinua uchumi wa wananchi. Mbali na suala la mikopo, Mhe. Marwa ameiomba Serikali kuharakisha uboreshaji wa Bandari ya Kirongwe, akieleza kuwa Rorya ni wilaya inayopakana na Kenya, hivyo bandari hiyo ina nafasi muhimu katika kukuza biashara za mipakani, kuongeza fursa za ajira na kuchochea ukuaji wa uchumi wa wananchi wa eneo hilo. Aidha, amemshukuru Rais Samia na Serikali kwa kuendelea kupeleka fedha nyingi za utekelezaji wa ...

CHEGE AIOMBA SERIKALI KUTATUA KERO ZA MAJI, UMEME NA BARABARA RORYA

 Mbunge wa Rorya, Jafari Chege, ameiomba Serikali kuharakisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Mamlaka ya Mji Mdogo Shirati, akieleza kuwa wananchi bado wanakabiliwa na changamoto za maji, umeme, barabara na ukosefu wa soko la kisasa. Akizungumzia huduma ya maji, Chege amesema licha ya uwekezaji uliofanyika, wananchi wengi wa Shirati bado hawapati maji safi na salama kwa uhakika.  Amesema akina mama na wananchi wengine wanaendelea kutumia muda mwingi kutafuta maji, hivyo kuiomba Serikali kueleza changamoto zinazokwamisha upatikanaji wa huduma hiyo na kuhakikisha mradi wa maji unakamilika ili wananchi wanufaike. Kuhusu umeme, amesema huduma hiyo ni muhimu katika kukuza biashara, viwanda vidogo na shughuli nyingine za kiuchumi, hivyo ameomba Serikali kuendelea kuboresha upatikanaji wa umeme wa uhakika ili kuongeza kasi ya maendeleo katika eneo hilo. Aidha, Mbunge huyo ameomba Serikali kuharakisha ujenzi wa barabara za lami zilizoahidiwa, akisema miundombinu hiyo itarahi...

MWAMKO WA ULIPAJI KODI KWA HIARI, CHACHU YA MWELEKEO WA KUJITEGEMEA KIBAJETI KWA ASILIMIA 74.2

 NA: DK. REUBENI LUMBAGALA Waasisi wa taifa letu walipambana na wakoloni ili kujinasua kutoka kwenye makucha ya kutawaliwa na kuamuliwa nini cha kufanya ili hali uwezo wa kufanya hivyo tulikuwa nao. Disemba 09, 1961, tukapata uhuru kamili wa kisiasa lakini tukiwa hoi kiuchumi, hivyo kuwa na wajibu wa kujenga uchumi imara wa kutufanyia tuheshimike kwa wengine. Wenye wajibu wa kujenga uchumi ni wananchi wenyewe wa nchi husika. Mathalani, kwa Tanzania, ni sisi Watanzania wenyewe ambao tunawajibika kuijenga nchi yetu kisiasa, kiuchumi na kijamii. Ni hivi: Hatuna mjomba wala shangazi wa kuja kuijenga Tanzania yetu. Ni sisi Watanzania wenyewe ndiyo wahusika wa kuijenga nchi yetu, kuhakikisha tunatatua changamoto zilizopo na kukuza ustawi wetu kwa maendeleo endelevu. Kazi kubwa ya kujenga uchumi imara na uboreshaji wa huduma za kijamii, inategemea sana uwepo wa raslimali fedha za kufanikisha utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.  Swali linakuja, tunapata wapi fedha za kuteke...

WATANZANIA SASA KUJIPIMA UTI WAKIWA NYUMBANI

 …..Ni kwa kutumia kipimo cha Checkfor UTI Test Na Mwandishi Wetu Tanzania imeendelea kupiga hatua katika sekta ya afya ambapo kipimo kipya cha UTI kinachomwezesha mtu kujipima akiwa nyumbani na kugundua kuwa amepata maambukizi ya ugonjwa huo kimeanza kutumika hapa nchini. Kipimo hicho kinachojulikana kama Checkfor UTI Test kimekuwa nyenzo muhimu kwani maambukizi ya njia ya mkojo, yanayojulikana zaidi kama UTI, ni miongoni mwa changamoto za kiafya zinazowakumba watu wengi katika jamii. Hayo yalisemwa jana jijini Dar es Salaam na daktari Dk Eshton Nkala wakati akizungumzia kipimo hicho kipya cha aina yake kuanza kutumika nchini. Alisema mara nyingi, maambukizi haya huanza kwa dalili ambazo zinaweza kuonekana kuwa ndogo, ikiwemo kukojoa mara kwa mara, maumivu au muwasho wakati wa kukojoa, maumivu ya chini ya tumbo, mkojo kubadilika rangi au kuwa na harufu isiyo ya kawaida. Alisema changamoto kubwa katika udhibiti wa UTI ni kuchelewa kutambua dalili na kuchelewa kufika katika vituo v...

NEW IPU SECRETARY GENERAL TAKES OFFICE AS EXECUTIVE COMMITTEE CONCLUDES 300TH SESSION

By Prosper Makene The IPU Executive Committee held its 300th session in Geneva, Switzerland, on 29-30 June 2026, under IPU President Dr. Tulia Ackson. The constitutional meeting coincided with International Day of Parliamentarism, observed annually on 30 June to mark the founding of the IPU. Delegates reviewed preparations for the 153rd IPU Assembly scheduled for October in Arusha, Tanzania. They also discussed the upcoming election of a new President to replace Dr. Ackson. The session featured the formal handover of the Secretary General’s office. Mr. Martin Chungong passed the “keys” of leadership to Ambassador Anda Filip, elected in April in Istanbul. Her four-year term began on 1 July 2026. Ambassador Filip is the 10th Secretary General, the first woman, and the first from Eastern Europe to lead the IPU Secretariat. The Parliament of Tanzania congratulated Ambassador Filip and pledged continued cooperation with the IPU.

BALOZI FILIP AANZA KAZI RASMI

 Na Prosper Makene Wajumbe wa Kamati ya Uongozi ya IPU wamehitimisha kikao chao cha 300 jijini Geneva, Uswizi, tarehe 29-30 Juni 2026, chini ya uongozi wa Dkt. Tulia Ackson, Rais wa IPU. Kikao hicho cha Kikatiba kimeambatana na Maadhimisho ya Siku ya Mabunge Duniani, tarehe 30 Juni, ambayo ndiyo tarehe ya kuanzishwa kwa IPU.  Katika ajenda, Kamati ilijadili maandalizi ya Mkutano Mkuu wa 153 wa IPU utakaofanyika Oktoba jijini Arusha, Tanzania, pamoja na uchaguzi wa Rais mpya atakayemrithi Dkt. Ackson. Vilevile, kikao kilishuhudia makabidhiano ya Ofisi ya Katibu Mkuu. Bw. Martin Chungong alimkabidhi Balozi Anda Filip “funguo” ya uongozi, kufuatia uchaguzi wake Aprili jijini Istanbul. Balozi Filip alichukua wadhifa rasmi tarehe 1 Julai 2026.  Yeye ni Katibu Mkuu wa 10, Mwanamke wa kwanza, na Mtu wa kwanza kutoka Ulaya Mashariki kuongoza Sekretarieti ya IPU kwa kipindi cha miaka minne. Bunge la Tanzania linampongeza Balozi Filip na linaahidi kuendelea kuimarisha ushirikiano n...

WAZIRI MKUU AKAGUA DARAJA LA NYATHOROGO, AIPONGEZA TARURA KWA MRADI WA SHILINGI MILIONI 729.2

 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, amekagua Daraja la Mto Nyathorogo lililopo Kijiji cha Nyathorogo, Kata ya Nyathorogo, wilayani Rorya mkoani Mara, linalounganisha wilaya za Rorya na Tarime katika ziara yake ya kikazi mkoani humo leo Julai 2, 2026. Akipokea taarifa ya utekelezaji wa mradi huo, Meneja wa TARURA Wilaya ya Rorya, Mhandisi Elifadhili Moses, amesema ujenzi wa daraja hilo umegharimu shilingi milioni 729.2, ambapo ulianza Agosti 1, 2025 na kukamilika Februari 28, 2026. Mhandisi Moses ameeleza kuwa daraja hilo limejengwa kwa teknolojia ya mawe, hatua iliyosaidia kupunguza gharama za ujenzi kwa zaidi ya asilimia 50 ikilinganishwa na usanifu wa awali. Ameongeza kuwa Serikali tayari imetenga fedha katika mwaka wa 2026/2027 kwa ajili ya ujenzi wa kingo za kulinda daraja hilo dhidi ya mmomonyoko wa maji. Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo la Rorya, Jafari Chege, amesema kukamilika kwa daraja hilo kumemaliza changamoto ya muda mrefu ya wananchi...

PRESIDENT CHAPO ARRIVES FOR A THREE-DAY WORKING VISIT

The President of the Republic of Mozambique, H.E. Daniel Francisco Chapo, has arrived in the United Republic of Tanzania to commence a three-day working visit from 2 to 4 July 2026. Upon his arrival at Julius Nyerere International Airport in Dar es Salaam, H.E. President Chapo was received by the Minister for Foreign Affairs and East African Cooperation, H.E. Ambassador Dr. Mahmoud Thabit Kombo (MP), who was accompanied by other senior Government officials. During his visit, H.E. President Chapo will hold official talks with his host, the President of the United Republic of Tanzania, H.E. Dr. Samia Suluhu Hassan, at the State House in Dar es Salaam. He will also officiate the opening of the 50th Dar es Salaam International Trade Fair (DITF), pay a courtesy call to Mama Maria Nyerere, and lay the foundation stone for the construction of the Embassy of the Republic of Mozambique in Dar es Salaam. It is noteworthy that this marks H.E. President Chapo's third visit to Tanzania since as...