Skip to main content

Posts

Showing posts from October 28, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Mgombea Ubunge wa Ccm Jimbo la Bukoba Mjini Amwaga Shukrani kwa Wananchi

Na Angela Sebastian ;Bukoba  Mgombea Ubunge wa jimbo la Bukoba mjini kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mhandisi Johnston Mutasingwa amewashukuru wananchi wa jimbo hilo, kwa ushirikiano na mapokezi makubwa waliompatia tangu kuanza kwa kampeni za kunadi Ilani ya chama hicho na kuomba ridhaa. Adha amewashauri wajitokeze kwa wingi kesho kutekeleza haki yao ya kidemokrasia kwa kupiga kura na kuchagua viongozi wa CCM kuanzia ngazi ya Taifa hadi kata ili waweze kushirikiana kuwaletea maendeleo.  Mutasingwa ameeleza hayo leo wakati akihitimisha kampeni zake katika viwanja vya Shule ya Msingi Kashai ndani ya Manispaa ya Bukoba ambapo amesema kesho ni siku muhimu kwa Taifa letu hivyo, akawaomba wananchi kumuamini na kumtuma kwa kumpigia kura za kutosha Rais Dk.Samia Suluhu Hassan,yeye kwa nafasi ya ubunge na madiwani kwasababu ndiyo chaguo sahii la kutatua kero zao. "Nawaomba mjitokezeni kwa wingi kesho mpige kura kwa amani, utulivu na mchague viongozi wa CCM tutumeni kwas...

Uwekaji Michango Kwa Wakati Kutapunguza Kero ya Mafao Sekta Binafsi

Na Mwandishi wetu Jovina Massano Musoma. UWASILISHAJI michango kwa wakati utaondoa na kupunguza kero ya malipo kwa waajiriwa wa sekta binafsi pindi wanapoacha kazi au kustaafu. Hayo yamesemwa na meneja wa shirika la mfuko wa hifadhi ya Jamii *(NSSF)* mkoa wa Mara Maneno Mpogole katika hafla fupi ya kuwashukuru wateja kwa ushirikiano wanaoutoa kwa mfuko katika nyanja mbalimbali. Ameainisha nyanja hizo kuwa ni pamoja na kujiandikisha,kulipa michango, kununua au kutumia bidhaa zitolewazo na mfuko ambazo ni nyumba,viwanja,daraja la Mwalimu Nyerere ikiwemo kupanga katika majengo yanayomilikiwa na NSSF yaliyopo katika maeneo mbalimbali hapa nchini. Mpogole amewahimiza waajiri kuendelea kuwasilisha michango yao kwa wakati kupitia mfumo wa kidigitali ili kuepusha usumbufu kwa wanachama watakaostaafu au kuachishwa kazi kwa kulipwa kwa wakati na kuondoa kero ya malipo kwa wakati. "Kulingana na kasi ya ukuaji wa teknolijia duniani kwa sasa  *NSSF* imeweza kurahisisha huduma zake ambapo waaji...

Act Wazalendo Yaahidi Kutatua Kero ya Ukosefu wa Choo Ofisi ya Kata na Uhaba wa Vifaa Tiba Kata ya Kamnyonge

Na Mwandishi wetu Jovina Massano. MGOMBEA udiwani Kata ya Kamnyonge Jimbo la Musoma mjini mkoani Mara Ladislaus Kutara ameahidi kuboresha miundombinu ya choo na upatikanaji wa huduma bora za kijamii Kata ya Kamnyonge. Ameyasema hayo wakati akihitimisha  kampeni Oktoba 27,2025 na kunadi sera za Chama hicho katika eneo la wazi la Biafra. Amesema Kata hiyo inakabiliwa na changamoto nyingi za huduma bora za kijamii ikiwemo afya na Miundombinu ya barabara na ukosefu wa huduma ya choo ofisi ya  mtendaji wa Kata hiyo. "Uboreshaji wa miundombinu ya choo utasaidia upatikanaji wa huduma za mahitaji ya nyumbani karibu kwa wakazi wa Kata hiyo", amesema Ladislaus. Ameongeza kuwa uwepo wa choo katika ofisi ya mtendaji wa Kata kutapelekea ufanisi kiutendaji. Kwa Upande wa huduma za Afya amesema ataishauri serikali kuhakikisha upatikanaji  wa vifaa tiba hasa madawa ili kuondoa adha ya uhaba wa vifaa tiba kwa wahitaji pindi wanapofika katika Zahanati hiyo.  Aidha ameeleza kuwa atawas...

Uchaguzi Mkuu wa 2025 ni Halali” – Mwanasheria Mkuu wa Serikali

Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Hamza S. Johari amesema kuwa, Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani 2025 unaotarajiwa kufanyika tarehe 29 Oktoba, 2025 ni halali kwakuwa umefuata misingi ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Sheria za Uchaguzi. Mwanasheria Mkuu wa Serikali ameyasema hayo katika Mkutano na Vyombo vya Habari uliofanyika Ofisini kwake Mtumba Jijini Dodoma, tarehe 28 Oktoba, 2025. Akizungumza katika mkutano huo Mhe. Johari amesema kuwa Uchaguzi Mkuu wa 2025 ni kwa mujibu wa masharti yaliyowekwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977. Aidha, Mwanasheria Mkuu wa Serikali ameeleza kuwa, ni haki ya kila Mtanzania aliyetimiza umri wa miaka 18 kushiriki katika Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani kama ilivyoainishwa katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.  *“Ibara ya 5(1) ya Katiba yetu inatoa haki kwa kila raia wa Tanzania aliyetimiza umri wa miaka kumi na minane kupiga kura katika uchaguzi unaofanywa Tanzania na Wananchi....

Edwin Soko asema CCM Yawa Kinara wa Kusikilizwa na Wapiga Kura

Mwandishi wa habari  Mwandamizi na mtetezi wa Haki za binadamu Edwin Soko amesema kuelekea kwenye uchaguzi mkuu October 29,2025 , Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeendelea kudhihirisha kuwa ndicho chama kinachosikilizwa zaidi na wapiga kura nchini. Amesema  hii ni kutokana na misingi yake ya muda mrefu ya uongozi, sera thabiti na mtandao mpana wa kisiasa unaogusa wananchi  kuanzia shina hadi Taifa kwa ujumla   Akizungumza na waandishi na waandishi wa habari  leo October 28,2025   amefanya uchambuzi wa mwenendo wa kampeni za wagombea wa vyama mbalimbali kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu.   "Wananchi waelewe kwamba  takwimu na tafiti mbalimbali za kisiasa zimeonyesha kuwa, licha ya kuwepo kwa vyama vingine vya upinzani vinavyoimarika, CCM bado kinaongoza kwa ushawishi mkubwa katika mijadala ya kisiasa, majukwaani, na hata katika majadiliano ya wananchi mitaani"alisema Soko Aidha  ameongeza kuwa, Nguvu ya Historia  ni mtaji kwa C...

𝗪𝗔𝗧𝗔𝗡𝗭𝗔𝗡𝗜𝗔 𝗪𝗔𝗠𝗘𝗥𝗜𝗗𝗛𝗜𝗞𝗔 𝗡𝗔 𝗨𝗧𝗘𝗡𝗗𝗔𝗝𝗜 𝗞𝗔𝗭𝗜 𝗪𝗔 𝗗𝗞𝗧. 𝗦𝗔𝗠𝗜𝗔 - 𝗗𝗞𝗧. 𝗡𝗖𝗛𝗜𝗠𝗕𝗜

-𝘼𝙢𝙨𝙝𝙪𝙠𝙪𝙧𝙪 𝘿𝙠𝙩. 𝙎𝙖𝙢𝙞𝙖 𝙠𝙬𝙖 𝙠𝙪𝙚𝙣𝙙𝙚𝙡𝙚𝙖 𝙠𝙪𝙢𝙪𝙖𝙢𝙞𝙣𝙞 𝙣𝙖 𝙠𝙪𝙢𝙩𝙚𝙪𝙖 𝙠𝙪𝙬𝙖 𝙈𝙜𝙤𝙢𝙗𝙚𝙖 𝙈𝙬𝙚𝙣𝙯𝙖. "Nakushukuru sana Mgombea Urais wa Tanzania kupitia chama chetu cha CCM kwa imani yako kubwa kwangu kwa kunipendekeza kuwa msaidizi wako mkuu, miaka minne iliyopita uliniteua kuwa Balozi wa Tanzania nchini Misiri, badae ukanipendekeza  kupitia vikao vya Halmshauri Kuu ya CCM Taifa kuwa Katibu Mkuu wa CCM na sasa umeniamini katika nafasi ya Mgombea Mwenza" "..ndani ya miaka minne umeonesha imani yako kwangu kwa kunipa nafasi muhimu ndani ya Taifa letu na ndani ya CCM.." "..nakuhakikishia kuwa imani uliyoonesha, namna pekee ninayoweza kuilipa ni kukusaidia kwa nguvu, akili, maarifa na uaminifu ili ndoto na maono yako na utekelezaji wa ilani yetu ya CCM (2025/30) ufanyike kwa mafanikio makubwa katika miaka mitano ijayo." "Watanzania katika sehemu zote tulizopita wameridhika na utekelezaji wako wa ilani ya uchaguzi ...

Msama: Asilimia 70 Ya Wapiga Kura Wako Tayari Kumchagua Dkt. Samia

Kada wa Chama cha Mapinduzi na Mkurugenzi wa Msama Promotion Ndugu Alex Msama amesema kuwa kwa takwimu zilizopo, Mgombea Urais kupitia CCM Dkt Samia Suluhu Hassan atashinda Uchaguzi wa kesho kwa kishindo kikubwa. Msama amesema hayo kutokanana na takwimu zilizotolewa jana na Katibu Mwenezi wa Chama hicho Ndugu. Kenani Kihongosi kuwa Watanzania Milioni 25 walifuatilia kwa karibu sana Kampeni za Mgombea Urais kupitia CCM Dkt Samia Suluhu Hassan. Msama ameongeza kuwa na Watanzania wengine zaidi ya Milioni 5 wamefuatilia Kampeni hizo bila kufika kwenye mikutano, hivyo kufanya jumla ya wafuatiliaji wa Dkt. Samia kufikia Milioni 30. Msama amemaliza kwa kusema kuwa kwa takwimu kama hizo basi Dkt. Samia atashinda Uchaguzi Mkuu kwa kishindo kikubwa na atavunja rekodi kuwa Rais aliyechaguliwa kwa kura nyingi kuliko yeyote yule.