Skip to main content

Posts

Showing posts from January 21, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Waziri Mavunde kuwachukulia hatua maafisa madini wanaosababisha migogoro

Dodoma | Januari 22, 2026 Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde, amesema Serikali haitasita kuwachukulia hatua kali Maafisa Madini Wakazi wa Mikoa ambao ofisi zao zitabainika kuhusika au kusababisha migogoro katika shughuli za uchimbaji wa madini, akisisitiza ulazima wa kuzingatia kikamilifu Sheria na Kanuni za Madini katika utekelezaji wa majukumu yao. Mhe. Mavunde ametoa kauli hiyo leo jijini Dodoma wakati wa ufunguzi  kikao cha Menejimenti cha Tume ya Madini kilichowakutanisha Wakurugenzi, Mameneja na Maafisa Madini Wakazi wa Mikoa, kilicholenga kufanya tathmini ya utekelezaji wa majukumu ya Tume kwa kipindi cha robo ya pili ya mwaka, pamoja na kuweka mikakati ya kukabiliana na changamoto zinazojitokeza katika Sekta ya Madini. Kikao hicho kimehudhuriwa pia na Naibu Waziri wa Madini, Mhe. Dkt. Steven Kiruswa; Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Msafiri Mbibo; Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Dkt. Janet Lekashingo; Kamishna wa Tume ya Madini, Mhandisi Theonestina Mwasha, pamoja n...

Tanzania Yafungua Ukurasa Mpya wa Kiuchumi

📍 SEKTA YA FEDHA YAKUA, YAONDOLEWA KWENYE ORODHA YA MATAIFA HATARISHI Na Mashaka  Mhando, Tanga SEEIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetangaza mafanikio makubwa katika sekta ya fedha, huku rasilimali za kibenki zikipaa hadi kufikia shilingi trilioni 71.8 na nchi kuondolewa rasmi katika orodha ya mataifa yenye vihatarishi vya kifedha ( Grey List ) duniani. Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Laurent Deogratius kwa niaba ya Waziri wa Fedha Balozi Khamis Mussa Omar , wakati akifungua Maadhimisho ya Tano ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa yaliyofanyika katika Viwanja vya Usagara, jijini Tanga, Januari 21, 2026. Akizungumza mbele ya mamia ya wananchi na wadau wa fedha, Naibu Waziri amesema kuondolewa kwa Tanzania kwenye orodha ya nchi hatarishi (High-Risk List) na Umoja wa Ulaya (EU) ni ushindi mkubwa utakaofungua milango ya uwekezaji na kurahisisha miamala ya kimataifa kuanzia Januari 29, 2026. Takwimu zinaonesha kuwa sekta ya kibenki imeendelea kuimarika kwa ...

Kapalata aiomba Serikali kuchukua hatua za mapema kuiokoa miji inayozonguka migodi

*• Aekeza kuwa miji mingi duniani kudorora na kufa kiuchumi baada ya migodi kufungwa* *• Ataka viwanda, ajira na miundombinu ianzishwe sambamba na uwekezaji wa madini* *• Waziri Mavunde apongeza ushauri wa kitaalamu na mtazamo wa muda mrefu* *DODOMA* Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Mheshimiwa Neto Paul Kapalata, ameitaka Serikali kuweka Sera na miongozo madhubuti itakayohakikisha utoaji wa leseni kubwa za uchimbaji madini unaambatana moja kwa moja na wajibu wa kuendeleza miji inayozunguka migodi, ili miji hiyo iendelee kuwa na uhai wa kiuchumi na kijamii hata baada ya rasilimali za madini kuisha. Akizungumza wakati wa kikao cha Kamati hiyo, Mheshimiwa Kapalata amesema uzoefu wa kimataifa unaonesha kuwa utegemezi wa miji mingi kwenye uchumi wa madini pekee umesababisha kudorora kwa shughuli za kijamii na kiuchumi mara tu miradi ya uchimbaji inapofikia tamati, jambo linaloacha athari kubwa kwa wananchi na Serikali. “Miji mingi duniani imekosa uendelevu baada ya ...

Waziri wa Ulinzi na Jkt Akutana na Kaimu Balozi wa Marekani Tanzania

Waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga Taifa Mhe.Dkt.Rhimo Nyansaho (mb) , tarehe 21 januari 2026, jijini Dodoma amekutana na kufanya mazungumzo na kaimu Balozi wa Marekani nchini, Mhe Balozi Andrew Lentz  Pamoja na masuala mengine viongozi hao wamejadili kuendeleza uhusiano wa kidiplomasia uliopo baina ya mataifa hayo mawili . Aidha viongozi wawili Tanzania na Marekani walijadili masuala yahusuyo ulinzi na usalama pamoja na uchumi ambao nchi hizo zimekuwa zikishirikiana. Dkt.Nyansaho ameishukuru serikali ya Marekani na Balozi Lentz kwa kufika na kumuona na serikali ya Marekani kuendeleza ushirikiano na serikali ya Tanzania wakati wote tangu kuanzishwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya mataifa hayo ambao umekuwa na faida kwa maslahi mapana kwa wananchi wa pande zote mbili  Naye kaimu Balozi wa Marekani Nchini Mhe.Balozi Andrew Lentz ameipongeza serikali ya Tanzania kwa kuendelea kudumisha uhusiano wake na serikali ya Marekani. 

Waziri Mkuu Aongoza Mkutano Kazi Wa Mawaziri, Manaibu Mawaziri

WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba, ameongoza mkutano kazi wa Mawaziri, Makatibu Wakuu na Viongozi Waandamizi wa Serikali uliofanyika leo Januari 21, 2026, katika Ukumbi wa Kambarage, Hazina, jijini Dodoma.  Katika mkutano huo, viongozi hao wamejadili utekelezaji wa masuala mbalimbali ya Serikali yanayolenga uwekezaji kwenye sekta ya umma na binafsi katika kuchochea maendeleo ya nchini.