Skip to main content

Posts

Showing posts from April 13, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

JWTZ na Jeshi la India kushirikiana na mataifa tisa ya Afrika kukabiliana na matishio bahari ya hindi

  Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mh dkt Stergomena Lawrence Tax amezindua zoezi la Pamoja la ulinzi wa Bahari maarufu kama ‘AIKEYME’ lenye lengo la kukabiliana na matishio mbalimbali ya uhalifu baharini katika ukanda wa Bahari ya hindi. Akizungumza wakati wa kuzindua zoezi hilo aprili 13  mwaka 2025 katika bandari ya Dar es saam, baada ya kupokea meli vita moja kutoka nchini India ambayo imekuja maalum kwa ajili ya zoezi hilo linalohusisha nchi nyingine tisa za afrika, Mh, Stergomena Tax,amesema kuwa kumekuwa na matishio mbalimbali ya kiusalama baharini kama vile usafirishaji haramu wa madawa za kulevya,ugaidi,usafirishaji haramu wa bianadamu na uvuvi haramu. Kwa sababu hiyo amesema  kwa kushirikiana kwa Pamoja katika mazoezi hayo kutasaidia kuleta tija katika kushughulikia maswala hayo Pamoja na kuongeza ushirikiano na ujuzi katika ya nchi na nchi. Waziri huyo wa ulinzi na jeshi la kujenga taifa,amesema kuwa uwepo wa mazoezi hayo ni moja ya matokeo ya jitiha...

JWTZ lasaidia huduma tiba na afya Jamhuri ya Afrika ya kati

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania limechangia huduma tiba na afya kwenye hospitali ya Jiji la Berberati iliyoko nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati tarehe 14 Aprili mwaka 2025. Akizungumza mara baada ya uchangiaji wa huduma hizo kwa niaba ya Kamanda Kikosi cha Nane cha Ulinzi wa Amani nchini humo Luteni Kanali Theophil Nguruwe, Mkuu wa Operesheni na Utendaji Kivita wa Kikosi hicho Maj Mkangara Mzuma amesema kuwa JWTZ limefanya hivyo ikiwa ni moja ya kuimarisha amani nchini humo. " Siku zote JWTZ linathamini maisha ya watu na linawajibika na kuhakikisha wananchi wanaishi kwa amani na utulivu"alisema Maj Mzuma. Naye Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo, Daktari Sanzema Komoto amelishukuru JWTZ na uongozi wa Kikosi Cha Nane Cha Ulinzi wa Amani nchini humo kwa moyo wao wa kujitolea ili kurudisha amani kwa wananchi wake. "Tangu JWTZ lianze ulinzi wa amani nchini kwetu, limekuwa msaada mkubwa kwenye kusaidia huduma za afya na wananchi wetu wamefaidika sana" alisema Daktari ...

Rais mstaafu Jakaya Kikwete awasilisha ujumbe wa Rais Samia kwa Rais wa Guinea

  Rais Mstaafu wa Tanzania na Mjumbe Maalum wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, amewasilisha Ujumbe Maalum ambao ulipokewa na Waziri wa Nchi katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Guinea ya Ikweta, Mhe. Simeon Oyono Esono Angue, kwa niaba ya Rais wa nchi hiyo, Mhe. Teodoro Obiang Nguema Mbasogo. Uwasilishaji wa ujumbe huo ulifanyika katika ofisi ya Wizara ya Mambo ya Nje jijini Malabo tarehe 13 Aprili 2025. Katika tukio hilo, Mhe. Kikwete pia alitoa salamu za Rais Samia, akisisitiza umuhimu wa nchi za Afrika kuimarisha ushirikiano, mshikamano, na umoja ili kukabiliana kwa pamoja na changamoto zinazokabili Bara la Afrika na dunia kwa ujumla.

Tamasha la kuombea Uchaguzi Mkuu kufanyika mikoa 26

  Tamasha la kuombea Uchaguzi Mkuu litakalofanyika katika mikoa 26 linatarajiwa Kuanza Jijini Dar-es-Salaam Juni 21, 2025 Akizungumza na waandishi wa Habari April 12, Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion , Alex Msama amesema tamasha hilo halitakuwa na kiingilio ili kila mtanzania aweze kushiriki kwenye kuliombea taifa huku maandilizi yakiwa yanaendele vizuri Msama ameongeza kuwa tamasha litaanzia katika mkoa wa Dar es salaam na kwenda mikoa mingine na limehusisha Wachungaji, Maskofu wa mikoa mbalimbali katika kuhakikisha wanaombea amani kulekea uchaguzi Mkuu. Aidha amesema waimbaji mbalimbali wakubwa kutoka nje ya nchi na Ndani ya nchi watakuwepo kwenye tamasha la Kuombea Uchaguzi Mkuu Mwaka huu Wa 2025.

Sanaa ni uchumi - Majaliwa

  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali imejidhatiti kuendelea kukuza na kuimarisha sanaa nchini ikiwa ni moja ya sekta rasmi ya kiuchumi. Ametoa kauli hiyo leo Jumapili (Aprili 13, 2025) katika Kongamano la Chama cha Wafawidhi wa Matukio Tanzania, linalofanyika Olasiti Garden, Mkoani Arusha. Ambapo amesema fani ya ushereheshaji ni uchumi. Amesema kuwa kwa kutambua umuhimu huo, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan aliridhia kaunzisha Mfuko wa Utamaduni na Sanaa ambao unakopesha hadi shilingi Milioni 100 kwa wasanii wakiwemo washereheshaji ili waweze kujiimarisha kimitaji na vitendea kazi. “Pia kupitia maboresho ya Sheria ya Hakimiliki na Hakishiriki ya mwaka 1999 yaliyofanyika mwaka 2022, Serikali imeanzishwa tozo ya hakimiliki (copyright levy) ambapo asilimia 60 ya makusanyo inakuja kwenu moja kwa moja na asilimia nyingine 10 inakuja kwenu kupitia Mfuko” Katika hatua nyingine, Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa Serikali inatarajia kujenga Ukumbi wa Kimataifa ya Sanaa na Michezo ‘Art...
  Waziri nchi ofisi. ya waziri mkuu,kazi,ajira na wenye ulemavu mh Ridhwani Kikwete,ameshiriki marathon ya Hisani iliyoandaliwa na Lions Club kuchangia fedha kwa ajili ya Uchunguzi na Tiba kutibu Uono Tanzania. Michango hiyo inakwenda kutumiwa kusaidia kufanya uchunguzi na kutibu Changamoto zinazotokana na magonjwa ya Macho.  Hii sio mara ya kwanza kwa Taasisi hii ya Lion’s Club kuchangisha pesa kwa ajili ya kusaidia wenye uhitaji. Wamekuwa wakisaidia tiba Nchini na rufaa za Nje ya Nchi pamoja na kusaidia programu mbalimbali za serikali kwa wenye uhitaji maalum ikiwemo watu wenye Ualbino, na Wenye shida ya Kuona kwa kutoa vifaa kama Fimbo Nyeupe na mashine za Braile.

Waziri Mavunde azindua kiwanda cha uzalishaji vilipuzi - Kisarawe,Pwani

  ▪️Kiwanda kuzalisha tani 22,000 za baruti na vilipuzi milioni 15 kwa mwaka ▪️Ni matokeo ya kazi ya Rais Samia mazingira kuvutia uwekezaji ▪️ Zaidi ya ajira 300 za moja kwa moja na 1000 zisizo za moja kwa moja kuzalishwa *KISARAWE,PWANI* Serikali inaendelea na utekelezaji wa mkakati wake wa kuhakikisha Tanzania inakuwa kitovu cha uzalishaji wa bidhaa zinazotumika migodini na kupunguza uagizaji wa bidhaa hizo kutoka nje ya nchi. Hayo yamesemwa leo tarehe 13 Aprili, 2025 na Waziri wa Madini, *Mh.Anthony Mavunde (Mb)* alipotembelea na kuzindua kiwanda cha uzalishaji wa baruti na vilipuzi cha Solar Nitrochemicals Limited kilichopo Wilayani Kisarawe. "Mh. Rais wetu *Dkt. Samia S. Hassan* anafanya kazi kubwa ya kufungua fursa na kuweka mazingira mazuri yanayovutia uwekezaji nchini. Matokeo ya kazi hiyo ni pamoja na ujenzi wa kiwanda hiki cha kuzalisha bidhaa hizi ambazo ni muhimu sana kwenye uchimbaji wa madini. "Kama Serikali, tutaendelea kuwalinda wawekezaji wetu na kuwawekea ma...