Na.Angela Sebastian KATIBU tawala wa mkoa wa Kagera Steven Ndaki amewaagiza wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya mkoani humo kuhakikisha wanaanda maadhimisho ya juma la elimu maalum katika Maeneo yao ili kuwezesha wananchi kupata uelewa kwa yanayofanywa na idara hiyo. Hayo yamebainishwa katika taarifa iliyosomwa na katibu tawala msaidi idara ya uchumi na biasharea Isaya Tendega kwa niaba ya katibu tawala,wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku mbili kwa maafisa elimu wa elimu maalum na wakuu wa shule zinazotoa elimu maalum mkoani humo yalifofanyika jana katika shule ya sekondari Omumwani . Amesema kuwa licha ya kwamba mkoa utafanya maadhimisho ya juma hilo lakini pia kila Halmashauri lazima inatakiwa kufanya madhimisho katika maeneo yake lengo likiwa ni kuwezesha wananchi waudhulie na kupata elimu ya kutosha juu ya idara ya elimu maalum na watu wazima sambamba na majukumu yake na faida zake. “Tunatakiwa kuendelea kuadhimisha juma la elimu ya watu wazima kwa k...
Marato tv - Sauti ya Jamii