Skip to main content

Posts

Showing posts from August 15, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

NAIBU KATIBU MKUU CCM BARA AGGREY MWANRI AWA MGENI RASMI MKUTANO WA HADHARA UBUNGO Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Ndugu Aggrey Mwanri (MCC), leo Agosti 15, 2026, amekuwa Mgeni Rasmi katika Mkutano wa Hadhara wa Jimbo la Ubungo, ulioandaliwa na Mbunge wa Jimbo hilo, Prof. Kitila Mkumbo, ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji. Kabla ya kushiriki mkutano huo, Ndugu Mwanri alipokewa katika Ofisi za CCM Mkoa wa Dar es Salaam na Sekretarieti ya CCM Mkoa, chini ya Katibu wa CCM Mkoa, Ndugu Mkandawire. Aidha, alipokea taarifa fupi kuhusu utendaji wa Chama katika Mkoa huo na kuwashukuru viongozi wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam kwa usimamizi mzuri wa Chama na Serikali. Akizungumza katika mkutano huo, Ndugu Mwanri amesisitiza umuhimu wa Wabunge, Madiwani pamoja na Wenyeviti wa Serikali za Mitaa kufanya mikutano ya hadhara mara kwa mara ili kuwapa wananchi mrejesho kuhusu utekelezaji wa ahadi zilizotolewa na CCM wakati wa Uchaguzi. Aidha, amewasihi wananchi kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, akieleza kuwa Serikali imeendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika Mkoa wa Dar es Salaam na maeneo mengine nchini. Kwa upande wake, Prof. Kitila Mkumbo aliwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM mbele ya wananchi wa Jimbo la Ubungo, akieleza hatua zilizochukuliwa katika kuboresha miundombinu, hususan sekta ya barabara. Prof. Kitila amesema ataendelea kushirikiana na Chama Cha Mapinduzi na Serikali katika kuhakikisha wananchi wa Ubungo wanaendelea kupata huduma na maendeleo yanayostahili. KAZI NA UTU, TUNASONGA MB

  Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Ndugu Aggrey Mwanri (MCC), leo Agosti 15, 2026, amekuwa Mgeni Rasmi katika Mkutano wa Hadhara wa Jimbo la Ubungo, ulioandaliwa na Mbunge wa Jimbo hilo, Prof. Kitila Mkumbo, ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji. Kabla ya kushiriki mkutano huo, Ndugu Mwanri alipokewa katika Ofisi za CCM Mkoa wa Dar es Salaam na Sekretarieti ya CCM Mkoa, chini ya Katibu wa CCM Mkoa, Ndugu Mkandawire. Aidha, alipokea taarifa fupi kuhusu utendaji wa Chama katika Mkoa huo na kuwashukuru viongozi wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam kwa usimamizi mzuri wa Chama na Serikali. Akizungumza katika mkutano huo, Ndugu Mwanri amesisitiza umuhimu wa Wabunge, Madiwani pamoja na Wenyeviti wa Serikali za Mitaa kufanya mikutano ya hadhara mara kwa mara ili kuwapa wananchi mrejesho kuhusu utekelezaji wa ahadi zilizotolewa na CCM wakati wa Uchaguzi. Aidha, amewasihi wananchi kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. S...

MOTO MKUBWA WATEKETEZA MADUKA NA NYUMBA BARABARA 12 JIJINI TANGA.

Na Mwanamkuu Mwandoro, Tanga. Moto mkubwa  uliozuka majira ya saa mbili usiku umeteketeza maduka 11 na nyumba 2 eneo la standi ya daladala Barabara 12 jijini Tanga. Akizungumza baada ya tukio hilo mmiliki wa nyumba Mzee Hamisi Abdallah amesema moto huo umesababisha hasara kubwa kwani hawaja wafanikiwa kuokoa kitu chochote zaidi ya roho zao. Aidha Hamisi pia ameiomba serikali kumuangalia Kwa hicho la tatu kwani tukio hilo limemridisha nyuma kiuchumi na kwamba hilo ndilo lilikiwa tegemeo kubwa kwake. Kwa Upande wake mmiliki wa maduka mawili ambaye pia ni muhanga wa moto huo Godias Anthony Kimath amesema mpaka sasa ameshaukaribisha umasikini wakasi na hivyo anajipanga namna ya kusimama tena kwani mali zinatafutwa. "Nilikuja Tanga nikiwa Sina kitu hivyo basi Sina budi kumshukuru mungu Kwa tukio  hili na kikubwa ni kujipanga na kuangalia namna gani nitasimama tena japo hasara ni Kubwa sana kwani sijaokoa kitu chochote,"alisema Kimath

MUWASA YAWAOMBA RADHI WATEJA KUTOKANA NA ADHA YA KUKOSEKANA KWA MAJI MANISPAA YA MUSOMA.

  Na Mwandishi wetu Jovina Massano. Mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira Musoma (MUWASA) Mkoani Mara yawaomba radhi wateja wake kutokana na hitilafu ya mitambo ya kusukuma maji iliyopo kwenye chanzo Cha maji Bukanga hali iliyopelekea upatikanaji hafifu wa maji katika baadhi ya maeneo. Hayo yameelezwa na kaimu mkuu wa kitengo cha mawasiliano na uhusiano kwa Umma Chausiku Joseph mara baada ya kupokea taarifa ya malalamiko ya wateja wa maji wa maeneo ya Buhare,Rwamlimi,Mtakuja,Kwangwa,Kigera,Songe,majengo,Kariakoo,Zanziba,na Kijiji cha Nyabange. Chausiku amesema kuwa Mamlaka inaendelea kufanya jitihada kubwa kuhakikisha huduma inajerea kupitia wataalam ambao wanaendelea kufanya marekebisho na maboresho ya mitambo hiyo. Ameongeza kuwa hivi sasa timu ya wataalam wa MUWASA inaendelea na ufuatiliaji katika maeneo mbalimbali ili kuweza kuimarisha huduma kwa wateja. "Ndani ya siku kadhaa zilizopita kulikuwa na changamoto ya huduma ya maji kutokana na hitilafu ya mitambo ya kusukuma...

MUWASA YAWAOMBA RADHI WATEJA KUTOKANA NA ADHA YA KUKOSEKANA KWA MAJI MANISPAA YA MUSOMA.

Na  Mwandishi wetu Jovina Massano. Mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira Musoma (MUWASA) Mkoani Mara yawaomba radhi wateja wake kutokana na hitilafu ya mitambo ya kusukuma maji iliyopo kwenye chanzo Cha maji Bukanga hali iliyopelekea upatikanaji hafifu wa maji katika baadhi ya maeneo. Hayo yameelezwa  na kaimu mkuu wa kitengo cha mawasiliano na uhusiano kwa Umma Chausiku Joseph mara baada ya kupokea taarifa ya malalamiko ya wateja wa maji wa maeneo ya Buhare,Rwamlimi,Mtakuja,Kwangwa,Kigera,Songe,majengo,Kariakoo,Zanziba,na Kijiji cha Nyabange. Chausiku amesema kuwa Mamlaka inaendelea kufanya jitihada kubwa kuhakikisha huduma inajerea kupitia wataalam ambao wanaendelea kufanya marekebisho na maboresho ya mitambo hiyo. Ameongeza kuwa hivi sasa timu ya wataalam wa  MUWASA inaendelea na ufuatiliaji katika maeneo mbalimbali ili kuweza kuimarisha huduma kwa wateja. "Ndani ya siku kadhaa zilizopita kulikuwa na changamoto ya huduma ya maji kutokana na hitilafu ya mitambo ya k...

SEKTA YA MADINI YAVUTIA UWEKEZAJI WA TRILIONI 9 NDANI YA MIAKA MINNE

▪️Mikataba ya Msingi 14 ya Madini Yasainiwa ▪️Serikali yasaini Mkataba wa Bilioni 265 na Kampuni ya Henan Yudi Mining ya Mradi wa Graphite Morogoro ▪️Tanzania yawa kivutio kikubwa cha uwekezaji sekta ya Madini Afrika ▪️Rais Samia apongezwa kwa mazingira wezeshi ya uwekezaji 📍MOROGORO:  Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde, amesema ndani ya kipindi cha Miaka Minne, (4) Sekta ya Madini imevutia uwekezaji wa Shilingi trilioni 9, hatua inayoiweka Tanzania kuwa kivutio cha uwekezaji wa Madini Barani Afrika. Amesema hayo leoAgosti 15, 2026, Mkoani Morogoro wakati wa hafla ya utiaji saini wa Mikataba ya Ubia wa Uchimbaji wa Madini ya Kinywe baina ya Serikali na Kampuni ya Henan Yudi Mining na kuongeza kuwa, hadi sasa tayari jumla ya mikataba ya Msingi 14 imekwisha sainiwa. Amesema kuwa mradi huo una mashapo yaliyothibitishwa ya takribani tani milioni 104.28 za kinywe, na unatarajiwa kuwekeza takribani Dola milioni 100 (Shilingi bilioni 265) huku uzalishaji wa kiwango kamili ukilenga k...