Skip to main content

Posts

Showing posts from August 26, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

MWENGE WA UHURU KAGERA: MIRADI 54 YA SH. BILIONI 23 KUZINDULIWA NA KUKAGULIWA

 Na Angela Sebastian; Bukoba  Mwenge wa Uhuru Kuzindua na Kukagua Miradi 54 ya Sh. Bilioni 23 Kagera  Mwenge wa Uhuru mwaka huu unatarajiwa kuzindua, kufungua, kukagua na kuweka mawe ya msingi katika miradi 54 ya maendeleo yenye thamani ya Sh. bilioni 23 mkoani Kagera. Akizungumza na waandishi wa habari leo, Agosti 26, 2026, Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Kanali Yahya Kido, amesema Mwenge huo utapokelewa wilayani Muleba ukitokea mkoani Geita tarehe Agosti 30, 2026, kabla ya kuanza kukimbizwa katika halmashauri nane za mkoa huo. Kwa mujibu wa Kanali Kido, Mwenge wa Uhuru utatembea umbali wa takribani kilomita 1,230 ndani ya Kagera, huku ukiifikia miradi 54 katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo,katika miradi hiyo, 25 itawekewa mawe ya msingi, mitano itafunguliwa, 11 itazinduliwa na 13 itakaguliwa ili kujiridhisha na utekelezaji wake pamoja na manufaa yake kwa wananchi. Miradi hiyo inahusisha sekta muhimu za maendeleo, ikiwemo maji, ...

ELIMU YAHITAJIKA KUOKOA MIUNDOMBINU YA SERIKALI.

 Na Mwanamkuu Mwandoro, Tanga. Mamlaka za kiserikali zimetakiwa kutoa elimu zaidi kwa jamii ili kuepusha uharibifu wa miundombinu ya serikali ikiwemo reli,mabomba ya maji na umeme. Hayo yamesemwa na mkurungenzi wa kampuni ya Migungani company limited inayojishughulisha na ukusanyaji taka rejeleshi (chuma chakavu,oil chafu na chupa za maji) Bwana. Johannes Alexander Chacha iliyopo jijini Tanga. Chacha ametoa kauli hiyo kufuatia changamoto wanazopitia kutokana na biashara wanayofanya ya chuma chakavu,wao ambao wanafata Sheria zote na kuwa na vibali pia hujikuta wanatiwa matatizoni. "Niiombe serikali kusimamia vema sheria zilizowekwa katika biashara hii ya taka rejeleshi kwani itasaidia kuwatambua hata wale wanaofanya biashara hii kinyume cha Sheria",alisema Chacha  Aidha chacha pia ameishukuru serikali Kwa kuwaona na kuwapa kipaumbele pale inapokuja miradi ya kimkakati kama ujio wa Bomba la mafuta ghafi linaloendelea kujengwa huko chongoleani,kwani wao ni wadau wa kubwa wa mae...

MAHERA AHOJI SERIKALI: LINI VITONGOJI 109 BUTIAMA VITAPATA UMEME?

 MBUNGE wa Jimbo la Butiama, Dkt. Charles Mahera, ameitaka Serikali kueleza hatua inazochukua kuhakikisha wananchi wa vitongoji 109 katika jimbo hilo vinapatiwa huduma ya umeme. Akizungumza leo, Agosti 26, 2026, wakati wa kipindi cha maswali na majibu Bungeni jijini Dodoma, Dkt. Mahera amesema wananchi wa maeneo hayo wamekuwa wakisubiri kwa muda mrefu huduma hiyo na kutaka kujua lini Serikali itakamilisha usambazaji wa umeme. Akijibu, Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Salome Makamba, amesema Serikali inaendelea kutekeleza miradi ya usambazaji umeme nchini kwa kuzingatia ahadi za Serikali, Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) pamoja na Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050. Amesema fedha zimetengwa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi hiyo, huku akieleza kuwa Serikali inalenga kuhakikisha maeneo yote ambayo bado hayajafikiwa na huduma ya umeme yanaunganishwa kabla ya mwaka 2030. Naibu Waziri Makamba amempongeza Dkt. Mahera kwa kufuatilia maendeleo ya jimbo lake na kumtaka kuendelea kusimamia utek...

WAITARA AITAKA SERIKALI KUFUNGUA FURSA ZA UCHIMBAJI MADINI SERENGETI KWA VIJANA

 Mbunge wa Tarime Vijijini, Mhe. Mwita Waitara, ameitaka Serikali kuangalia uwezekano wa kutenga maeneo yanayodaiwa kuwa na madini katika maeneo yanayozunguka Hifadhi ya Serengeti, ili kuwawezesha vijana wa maeneo hayo kushiriki katika shughuli za uchimbaji na kunufaika kiuchumi. Waitara ametoa ombi hilo leo, Agosti 26, 2026, Bungeni jijini Dodoma wakati akiuliza swali la nyongeza kwa Naibu Waziri wa Madini, Mhe. Dkt. Steven Kiruswa, akitaka kujua ni lini Serikali itachukua hatua kuhusu maeneo hayo na kuwawezesha vijana kupata fursa za uchimbaji. Mbunge huyo amesema taarifa za kuwepo kwa madini katika maeneo hayo zimeibua matarajio kwa wananchi, hususan vijana, ambao wanahitaji fursa za ajira na shughuli za kuwawezesha kujipatia kipato. Akijibu swali hilo, Dkt. Kiruswa amesema Serikali ina utaratibu wa kisheria wa kutenga maeneo kwa ajili ya shughuli za uchimbaji madini, ikiwemo maeneo yenye matumizi mengine maalumu, endapo taratibu zote zinazotakiwa zitazingatiwa. Amesema matumizi...

BULAYA AOMBA SERIKALI KUKAMILISHA NYUMBA ZA WALIMU,MAABARA SHULENI NA KUJENGA MABWENI

MBUNGE wa Bunda Mjini, Mhe. Esther Bulaya, ameomba Serikali kuendelea kutoa fedha za kukamilisha ujenzi wa nyumba za walimu zilizoanzishwa katika halmashauri mbalimbali, pamoja na kujenga vyumba vya MAABARA na mabweni katika shule zilizo mbali na makazi ya wananchi. Mhe. Bulaya ametoa ombi hilo leo, Agosti 26, 2026, Bungeni jijini Dodoma, wakati akiuliza swali la nyongeza kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya waziri Mkuu–TAMISEMI, Prof. Riziki Shemdoe. Akizungumzia changamoto ya nyumba za walimu, Mhe. Bulaya amesema baadhi ya halmashauri zimeanza ujenzi wa nyumba hizo lakini zinakabiliwa na ukosefu wa fedha za kukamilisha miradi hiyo, hivyo kuiomba Serikali kuhakikisha inazipatia fedha ili kukamilisha majengo hayo. Pia ameitaka Serikali kuangalia changamoto ya mabweni katika shule mbalimbali, akitolea mfano baadhi ya shule zilizopo katika maeneo yenye umbali mkubwa na makazi ya wanafunzi, hali inayoweza kuwalazimisha wanafunzi kusafiri umbali mrefu kufuata elimu. Akijibu, Prof. Shemdoe amesema ...

SAMIA AONGOZA KIKAO MAALUM CHA KAMATI KUU YA CCM DAR ES SALAAM

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, akiongoza Kikao Maalum cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM kilichofanyika jijini Dar Es Salaam leo, Jumatano tarehe 26 Agosti 2026.

JWTZ YAZINDUA WIKI YA USHIRIKIANO WA KIJESHI NA KIRAIA EAC, WANANCHI KUNUFAIKA HUDUMA BURE

Wananchi katika maeneo mbalimbali nchini Tanzania wanatarajiwa kunufaika na huduma za afya bure, ukarabati wa vituo vya afya pamoja na misaada ya kijamii kupitia Wiki ya Ushirikiano wa Kijeshi na Kiraia ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) inayoendeshwa na majeshi ya nchi wanachama wa jumuiya hiyo. Wiki hiyo imezinduliwa leo jijini Dar es Salaam na Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Luteni Jenerali Salum Haji Othman, huku akisisitiza umuhimu wa ushirikiano wa kijeshi katika kuleta manufaa ya moja kwa moja kwa wananchi. Akizungumza wakati wa uzinduzi huo katika viwanja vya Golf Lugalo, Luteni Jenerali Othman amesema ushirikiano wa majeshi ya EAC si suala la ulinzi na usalama pekee, bali pia ni nyenzo ya kuimarisha mshikamano na ustawi wa wananchi wa Afrika Mashariki. Amesema kuandaliwa kwa shughuli hizo nchini Tanzania kwa mara ya pili ni ishara ya imani na uaminifu uliopo kwa Tanzania na JWTZ katika kuendeleza ushirikiano wa kikanda. Kwa upande wake, Mweny...