Skip to main content

Posts

Showing posts from June 22, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Waziri Kombo Amuaga Balozi wa Angola

Balozi wa Angola anayemaliza muda wake, Mhe. Sandro De Oliveira amekutana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Mahmoud Thabit Kombo (Mb) kwa madhumuni ya kuaga. Katika kikao hicho kilichofanyika jijini Dar es Salaam Juni 21, 2025, Mhe. Balozi Sandro De Oliveira alitumia muda huo kuishukuru Wizara na Serikali kwa ujumla kwa kumpa ushirikiano uliomuwezesha kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi katika kipindi chote cha uwakilishi nchini. Viongozi hao pia walijadili masuala mbalimbali ya kisekta kuhusu ushirikiano kati ya nchi ya Tanzania na Angola, ikiwemo sekta ya Gesi na Mafuta, Madini, Uchumi wa Buluu, usafirishaji kwa njia ya reli na Ushoroba wa Lobito.

Mkoa wa Mara Watoa Mafunzo Kwa Wachimbaji Wadogo wa Madini

 Na Ada Ouko, GMTV SERIKALI mkoani Mara kwa kushirikiana na Uongozi wa Mgodi wa dhahabu wa Barrick North Mara uliopo Nyamongo Wilayani Tarime wamefungua mafunzo maalumu kwa wachimbaji wadogo yatakayowawezesha kuendesha shughuli zao kwa tija na kwa mafanikio makubwa. Akizungumza kwa niaba ya mkuu wa mkoa huo, wakati akifungua mafunzo hayo Juni 20, 2025 Mkuu wa Wilaya ya Musoma Juma Chikoka alisema mpango wa mafunzo hayo ni utekelezaji wa ahadi ya Waziri wa madini Antony Mavunde aliyefanya ziara mwezi May mwaka huu mkoani humo. " May mwaka huu Waziri wa madini alikuja hapa Nyamongo kwa ajili ya kuwakabidhi leseni vikundi vya vijana, ambapo jumla ya vikundi 48, na vijana 1736 walikabidhiwa leseni za uchimbaji kwa lengo la kuwawezesha kunufaika na rasilimali zitokanazo na sekta ya madini"Alisema Chikoka. Aidha aliwataka vijana na wanawake wanaonufaika na mradi huo kujitokeza kwa wingi kushiriki mafunzo hayo , Sambamba na hilo alitoa rai kwa Taasisi zinazohusika kusimamia vikundi...