Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mara, Mheshimiwa Agness Marwa, amekabidhi matofali 1,000 na mifuko 30 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa uzio unaozunguka wodi ya wazazi katika Kituo cha Afya Nyasho, Manispaa ya Musoma, hatua inayolenga kulinda faragha za mama wajawazito wakati wa kupata huduma za uzazi. Akizungumza wakati wa kutembelea kituo hicho, Mhe. Agnes Marwa amesema ameamua kutoa mchango huo kwa hiari yake baada ya kubaini changamoto inayowakabili kinamama wanaojifungua, akisisitiza kuwa hataki kusubiri wananchi wamfuate kumuomba msaada, bali ana wajibu wa kufuatilia na kutambua mahitaji yao mwenyewe. Pia amekishukuru Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kuwapa wabunge nafasi pana ya kutekeleza majukumu yao, huku akimpongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwataka wabunge kutoka na kuwafuata wananchi ili kutatua changamoto zinazowakabili. Mhe. Marwa amesema kama ilivyo kwa jukumu la malezi, yeye kama mama ana wajibu wa kufahamu changamoto zinazowakabili wananchi, hususan wa...
Marato tv - Sauti ya Jamii