Skip to main content

Posts

Showing posts from January 5, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Dkt. Nyansaho Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Barabara Mara

kikao cha Bodi ya Barabara ya Mkoa wa Mara kilichofanyika leo tarehe 06 Januari, 2026 kimemchagua Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Rhimo Nyansaho kuwa Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Barabara ya Mkoa wa Mara.  Awali Mwenyekiti wa kikao hicho, Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Kanali Evans Alfred Mtambi aliwasilisha jina la Dkt. Nyansaho katika kikao hicho na wajumbe kwa kauli moja wakaridhia.  Kikao cha Bodi ya Barabara Mkoa wa Mara ni cha kawaida na kinapokea taarifa za utekelezaji wa matengenezo ya barabara kuanzia mwezi Aprili, 2025 hadi Septemba, 2025.

Government Reserves Key Mining Goods & Services for Tanzanians as Local Content Hits TZS 5 Trillion

📍 Dodoma | Mining Sector Reforms Highlights ✅ 20 mining goods & services officially reserved for 100% Tanzanian-owned companies 📜 Implemented through amended Local Content Regulations (2018) 💰 Mining procurement reaches TZS 5 trillion (2024) — 88% sourced locally 👷🏽‍♂️ Tanzanian employment rises to 97% across mining projects 🏭 1,331-acre Buzwagi Industrial Zone set for mining-related manufacturing 📣 Minister calls on private sector to seize supply & service opportunities The Government, through the Ministry of Minerals, has officially announced a list of 20 goods and services that must be provided to mining operations exclusively by companies that are 100% Tanzanian-owned. The move strengthens Tanzanian participation across the entire mining value chain, in line with directives from Samia Suluhu Hassan. Speaking to the media in Dodoma on January 5, 2025, the Minister for Minerals, Anthony Mavunde, said the reforms follow amendments to the 2018 Local Content Regulations, ...

𝗠𝗔𝗠𝗔 𝗠𝗔𝗥𝗜𝗔 𝗡𝗬𝗘𝗥𝗘𝗥𝗘 𝗔𝗣𝗢𝗞𝗘𝗔 𝗡𝗜𝗦𝗛𝗔𝗡𝗜 𝗬𝗔 𝗕𝗔𝗕𝗔 𝗪𝗔 𝗧𝗔𝗜𝗙𝗔

Mjane wa Baba wa Taifa na Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mama Maria Nyerere amepokea nishani ya heshima kutoka Jamhuri ya Angola ya kutambua mchango wa Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika harakati za ukombozi na upatikanaji wa amani nchini Angola. Akikabidhi nishani hiyo kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Mahmoud Thabit Kombo (Mb.), amesema kuwa Nishani ni heshima kubwa kwa Mwalimu Nyerere na nchi yetu kwa ujumla kutokana na mchango wake kwenye harakati za ukombozi ambapo ardhi ya Tanzania ilitumika kwa ajili ya kutoa hifadhi, kuandaa mipango na mikakati pamoja na mafunzo kwa wapigania uhuru wa mataifa mbalimbali, ikiwemo Angola. Naye Balozi wa Angola nchini Tanzania, Mhe. Domingos de Almeida da Silva Coelho aliyeungana na Mhe. Kombo kuikabidhi nishani hiyo kwa Mjane wa Baba wa Taifa alisema “Angola inatambua mchango mkubwa...

Naibu Meya Haji Mtete Ashiriki Mazishi ya Deus Daniel

Diwani wa Kata ya Nyasho na Naibu Meya wa Manispaa, Mheshimiwa Haji Mtete, leo ameshiriki katika msiba wa marehemu Deusi Daniel, aliyekuwa mkazi wa Mtaa wa Mlango Mmoja, Kata ya Nyasho. Marehemu alifariki dunia tarehe 31 Desemba 2025 akiwa anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Kwangwa. Akitoa salamu za rambirambi kwa familia, ndugu na jamaa wa marehemu, Mheshimiwa Haji Mtete ameeleza kusikitishwa kwake na msiba huo, akimkumbuka marehemu Deusi Daniel kama mtu aliyekuwa wa karibu na mwenye mchango mkubwa katika masuala mbalimbali ya maendeleo ndani ya Kata ya Nyasho. Mheshimiwa Mtete amesisitiza kuwa marehemu alikuwa mshiriki mzuri wa shughuli za kijamii na maendeleo, hali iliyomfanya atambulike na kuthaminiwa na wananchi pamoja na viongozi wa kata hiyo. Aidha, ametoa wito kwa wananchi wa Kata ya Nyasho kuendelea kuwa wamoja, kushikamana na kusaidiana hasa katika nyakati za majonzi, akisisitiza umuhimu wa mshikamano wa kijamii kama msingi wa maendeleo na amani. Kwa kumalizia, Mheshimiwa...

Waziri Mkuu Ampongeza Dkt. Mwinyi Kwa Mapinduzi ya Sekta ya Elimu

_Asisitiza Serikali kuendelea kuwekeza katika elimu inayojenga ujuzi na maarifa_ WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba leo Januari 05, 2026 amezindua Skuli ya Sekondari ya Chukwani na kutumia fursa hiyo kumpongeza Mheshimiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa maboresho makubwa aliyoyafanya katika sekta mbalimbali ikiwemo ya elimu. “Ninampongeza Dkt. Mwinyi kwa ujenzi wa skuli hizi za kisasa zenye vifaa bora na zilizozingatia matumizi bora ya ardhi kwa ujenzi wa skuli za ghorofa. Elimu ndio urithi sahihi, watoto someni kwa bidii na mtumie vizuri fursa hii ambayo Serikali imewapatia. Hakikisheni mnaitunza vizuri miundombinu hii.” Waziri Mkuu amezindua rasmi Skuli hiyo ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa maadhimisho ya miaka 62 ya Mapinduzi kwa vitendo, ambapo amesema kuwa wakiweka kipaumbele katika maendeleo ya sekta ya elimu vijana wa Kitanzania wataweza kujikwamua kiuchumi.   “Ujenzi wa Skuli hii ya Sekondari ya Chukwani ni mwendelezo ...

Meya wa Manispaa ya Musoma Aanza Kazi Kwa Kishindo

 MSTAHIKI Meya wa Manispaa ya Musoma, Alex Nyabiti, akiwa pamoja na Naibu Meya, Haji Mtete, wamefanya ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo ya wananchi, hususan katika sekta ya elimu, katika Shule ya Msingi Makoko iliyopo Kata ya Makoko, Manispaa ya Musoma.  Ziara hiyo imelenga kuboresha na kuharakisha utekelezaji wa miradi hiyo kabla ya kufunguliwa kwa shule. Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Meya Alex Nyabiti amesema lengo la ziara hiyo ni kuweka vipaumbele katika utekelezaji wa miradi ya elimu, sambamba na kuhakikisha watoto wanapata vyumba vya madarasa vya kutosha, ikizingatiwa kuwa shule zinatarajiwa kufunguliwa tarehe 13 Januari, 2026. “Tutafanya vizuri endapo tutakuwa na ushirikiano wa pamoja, kuheshimiana katika utendaji wa kazi na kujipima katika nafasi tulizopewa. Hizi ni kazi za serikali, si za mtu binafsi,” amesema Meya Nyabiti. Meya Nyabiti amesema Serikali ya Awamu ya Sita, chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, ilitoa fedha kiasi cha shilingi milioni 50 mw...

Serikali Yaainisha Orodha ya Bidhaa na Huduma Migodini Ambazo Hazipaswi Kufanywa na Wageni

▪️Ni utekelezaji wa maelekezo ya Mh Rais Samia juu ya ushiriki wa watanzania kwenye sekta ya madini ▪️Ni kupitia Marekebisho ya Kanuni ya Ushirikishwaji Watanzania Sekta ya Madini ▪️Manunuzi na Bidhaa Migodini  Yafikia Shilingi Trilioni 5 mwaka 2024 ▪️Waziri Mavunde ataka Sekta Binafsi kuchangamkia fursa 📍 Dodoma  Serikali kupitia Wizara ya Madini imetangaza rasmi orodha ya Huduma na Bidhaa 20 zinazopaswa kutolewa Migodini kupitia kampuni zinazomilikiwa na watanzania kwa asilimia 100 ikilenga kuongeza wigo wa ushiriki wa Watanzania katika Sekta ya Madini ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Mh. Rais Dkt. Samia S. Hassan kuhakikisha watanzania wanashiriki kikamilifu kwenye mnyororo mzimawa sekta ya madini. Hayo yamebainishwa na Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde Januari 5, 2025 jijini Dodoma wakati akizungumza na Waandishi wa Habari na kueleza kuwa, hatua hiyo   imefanyika baada ya kufanywa marekebisho ya Kanuni za Ushirikishwaji wa Watanzania kwenye Sekta ya Madini...

Rais Mstaafu Jakaya Kikwete Awasili Kisiwani Pemba

 Rais Mstaafu Awamu ya Nne wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete, akiwasili Kisiwani Pemba kwa ajili ya Sherehe ya Uzinduzi wa Jengo la Afisi ya Uhamiaji na Makaazi ya Askari,Wilaya ya Micheweni, mkoa wa Kaskazini Pemba, ambapo amepokelewa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,George Simbachawene, Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. Anna Makakala na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Mgeni Hassan Yahaya. Uzinduzi huo ni sehemu ya Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 62 ya Mapinduzi ya Zanzibar.Uzinduzi huo utafanyika leo,tarehe 4 Januari,2026.