Skip to main content

Posts

Showing posts from October 29, 2024

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Wafanyabiashara dodoma wamshukuru Rais Samia kwa ujenzi wa machinga complex

▪️Jiji kujenga sakafu kupunguza nguvu ▪️Mbunge Mavunde awachangia 10m kutunisha mfuko wa Soko ▪️Awataka Mgambo wa Jiji kuacha kutumia mabavu ▪️Aahidi kuwaunganisha na Taasisi za fedha kwa ajili ya mitaji ▪️DC Shekimweri aahidi kusimamia utatuzi wa kero sokoni 𝐃𝐨𝐝𝐨𝐦𝐚 Wafanyabiashara wadogo wa Soko la Machinga Complex Jijini Dodoma wameishukuru serikali ya awamu ya sita chini ya Mh. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa namna ilivyowahamisha kutoka barabarani na kuwajengea soko maalum maarufu kama Machinga Complex. Akizungumza katika mkutano mkuu wa soko Kaimu Mwenyekiti wa Machinga Complex Ndg. Lucas Kingamkono ameishukuru serikali kwa uwepo wa soko la Machinga ambalo limerahisisha ufanyaji wa biashara kwa wafanyabiashara hao wadogo ambao awali walikuwa maeneo ambayo hayakuwa rasmi na hivyo kufanya biashara kwa mashaka. Akizungumza katika mkutano huo,Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini *lMh. Anthony Mavunde ameupongeza uongozi wa soko Kwa kuandaa mkutano wa kusikiliza kero za wafanyabiash...

Mariam mwinyi apongeza jitihada za wake wa marais afrika

 Mke wa Rais wa Zanzibar, Msarifu na Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini ya Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation Mhe. Mama Mariam Mwinyi ameeleza kufurahishwa na mchango mkubwa wa wake wa Marais wa Afrika, hasa katika kutoa ufadhili wa masomo kwa fursa 2,080 kwa madaktari chipukizi kutoka nchi 52 za Afrika kwenye taaluma 44 muhimu zinazohitajika, kama vile “oncology,” utaalamu wa afya ya uzazi kwa kina mama, tiba ya kisukari, na magonjwa mengine. Mama Mariam Mwinyi, ameyasema hayo leo tarehe 29 Oktoba 2024 alipozungumza katika Mkutano wa 11 wa “Merck Foundation Africa Asia Luminary” uliofanyika katika hoteli ya Johari Rotana, jijini Dar es Salaam, uliowakutanisha wake wa Marais wa Afrika kutoka nchi 15. Aidha Mama Mariam Mwinyi ametumia fursa hiyo kuipongeza “Merck Foundation” kwa kutimiza miaka 12 ya utekelezaji wa miradi yake ya maendeleo kwa nchi za Afrika na Asia, pamoja na miaka saba tangu kuanzishwa kwa taasisi hiyo. Halikadhalika, Mama Mariam Mwinyi amepongeza jitihada za ...

Biteko kuongoza maafisa wa ngazi ya juu Jwtz,Maafisa wa kati, askari na watanzania kuaga mwili wa Jenerali mstaafu Musuguri lugalo 01.11.2024

 

Shule ya msingi twibhoki bagamoyo yang'ara matokeo ya darasa la saba 2024

 

Mkuu wa jeshi la kujenga taifa awapa pole viongozi na wachezaji wa Jkt tanzania fc

 Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Generali Rajabu Mabele amekutana ns kusalimiana na baadhi ya viongozi wa JKT Tanzania FC na wachezaji alipowatembelea kwa ajili ya kuwapa Pole. Meja Jenerali Mabele ambae amepokelewa na viongozi wa JKT Tanzania FC baada kuwasili katika kambi ya wachezaji, Mbweni, Dar Es salaam kuwajulia hali kutokana na ajali waliyoipata 27 October 2024 baada ya basi lao walilokuwa wakisafiria kuacha njia na kuanguka eneo la Mbweni, wakitokea Dodoma kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Dodoma Jiji. Mkuu huyo wa JKT amepata nafasi ya kuzungumza na kuwapa Pole viongozi navwachezaji hao wa JKT Tanzania FC.

Mkuu wa majeshi nchini atangaza rasmi kifo cha Jenerali mstaafu David Musuguri

 

Waziri mkuu Majaliwa kufungua kongamano la kujadili bima ya afya kwa wote Jijini Arusha

TANZANIA imeitisha kongamano kubwa kwa ajili ya kujadili Mpango wa Bima ya Afya kwa Wote, sambamba na Mdahalo wa Kitaifa kuhusu Mpango wa Ufadhili wa Sekta ya Afya kwa kuhusisha wataalam wa sekta ya afya wa ndani na nje ya nchi. Kongamano hilo na mdahalo huo wa kitaifa unatarajia kufunguliwa na waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Kassim Majaliwa oktoba 30 katika kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha jijini Arusha. Tayari wadau hao wa sekta ya afya wameanza kongamano lao leo  tarehe 29 na kutegejea kumalizika kwa matukio hayo mawili 01 Novemba 2024.  Wataalamu hao kutoka sekta mbalimbali wa ndani na nje ya nchi watajadili mikakati inayofaa kutumiwa na nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kuboresha huduma za afya kwa wote. Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na wabia wa maendeleo imeshiriki uratibu wa maandalizi ya matukio hayo muhimu ambapo Mdahalo wa Kitaifa kuhusu...

Rais Mwinyi akutana na waziri wa nishati wa qatar

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein Ali Mwinyi leo katika siku ya kwanza ya ziara yake nchini Qatar . Mapema asubuhi alikutana na Waziri wa nchi wa Qatar anayeshughulikia masuala ya Nishati Mheshimiwa  Saad bin Sherida Al- Kaabi. Mazungumzo hayo yametoa nuru kwa Qatar kuiuzia Tanzania mbolea aina ya Urea kwa gharama nafuu. Mazungumzo hayo alihudhuriwa pia na Balozi wa Tanzania nchini Qatar Mheshimiwa Habib Awesi Mohammed pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mbolea ( TFC ) Samwel Ahadi Mshote.  Kesho akimaliza ziara yake nchini Qatar Rais Dk. Hussein Ali Mwinyi anatarajiwa kushiriki mkutano mkubwa wa Kimataifa wa  kutimiza miaka 30 ya Familia Duniani utakaofanyika jijini Doha. Halikadhalika Mkutano huo unafuatia Azimio la mwaka 1994 la Umoja wa Mataifa la Mwaka wa Kimataifa wa Familia ( IYF ) lililopitishwa rasmi na Baraza la Umoja wa Mataifa likizingatia thamani na umuhimu uliopo wa kuzilinda na kuzisaidia familia kupitia sheria za K...