Skip to main content

Posts

Showing posts from May 19, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Vyombo Vya Ulinzi na Usalama Msitoe Nafasi Kwa Watovu wa Adabu-Rais Samia

  Rais Samia: “Tusiwe shamba la bibi” - aonya wanaharakati wa nchi jirani kutoingilia masuala ya Tanzania Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ametoa onyo kali kwa wanaharakati kutoka nchi jirani kuacha kuingilia masuala ya ndani ya Tanzania, akisisitiza kuwa taifa hilo haliwezi kuwa “shamba la bibi” ambapo kila mtu anaingia na kufanya apendavyo. Akizungumza jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa toleo jipya la Sera ya Mambo ya Nje ya mwaka 2001 (Toleo la 2024), Rais Samia amesema kuna mwenendo unaoibuka wa baadhi ya wanaharakati kuvuka mipaka na kuingilia masuala ya ndani ya nchi, hali ambayo haiwezi kuvumiliwa. “Tusuiwe shamba la bibi kwamba kila mtu anaweza kuja na kusema anachokitaka… Tumeanza kuona mtitiriko au mwenendo wa wanaharakati ndani ya region (kanda) yetu hii, kuanza kuvamia na kuingilia mambo yetu huku,” alisema Rais Samia. Kauli hiyo inakuja siku moja baada ya wakili mashuhuri wa Kenya na aliyewahi kuwa Waziri wa Sheria, Martha Karua, pamoja na Jaji Mkuu wa zaman...

Rais Dkt. Samia Kufungua Daraja La Jp Magufuli (Kigongo - Busisi) Juni 19, 2025

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika hafla ya ufunguzi wa Daraja la JP Magufuli (Kigongo-Busisi) lenye urefu wa kilometa 3 na barabara zake unganishi zenye urefu wa kilometa 1.66 utakaofanyika tarehe 19 Juni, mwaka huu. Hayo yamesemwa na Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa leo tarehe 19 Mei, 2025 wakati alipokagua daraja hilo ambalo limekamilika kujengwa na litakuwa daraja refu zaidi katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati. "Jitayarisheni kwa wingi kumpokea kiongozi wetu mkuu atakapokuja kulifungua daraja hili Juni 19, 2025 ", amesema Waziri Mkuu Majaliwa. Kwa upande wake, Waziri wa Ujenzi Abdallah Ulega ameeleza kuwa Serikali ya Dkt. Samia Suluhu Hassan imefanikiwa kukamilisha ujenzi wa Daraja hilo linalopita juu ya maji kwa kutumia fedha za ndani ikiwa ni jambo la kihistoria kwa nchi yetu. Ameongeza kuwa zaidi ya shilingi bilioni 700 zimetumika katika ujenzi wa daraja hilo linalounganisha mji wa Kigo...

Majaliwa: Tumejizatiti Kupunguza Changamoto Katika Sekta ya Elimu

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imejizatiti katika kupunguza changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi zikiwemo za sekta ya elimu. Ameyasema hayo leo (Jumatatu, Mei 19, 2025) wakati akizungumza na wananchi katika mikutano wa hadhara iliofanyika Sengerema mjini na Buchosa wilaya ya Sengerema akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Mwanza. Waziri Mkuu amesema miongoni mwa hatua ambazo Serikali imezichukua ni pamoja na kuendelea kutoa elimu msingi bila ya ada na hivyo kuwawezesha watoto wa kitanzania wenye umri wa kwenda shule kupata elimu. Mheshimiwa Majaliwa amesema kwa sasa Serikali inaendelea na ujenzi wa shule za msingi na sekondari katika maeneo mbalimbali nchini hususani katika yale yenye msongamano mkubwa wa wanafunzi. ”Mkakati mwingine mkubwa unaoendelea kutekelezwa na Serikali ni ujenzi wa mabweni, nyumba za walimu, pamoja na kujenga shule za amali ili wanafunzi watakapomaliza shule hizi...

Rais Samia Atoa Onyo kwa 𝐖ageni 𝐖anaotumiwa 𝐊uja 𝐊uharibu 𝐀mani Nchini

Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ameitaka Wizara ya Mambo ya Nje, Wizara ya Mambo ya Ndani na Vyombo vya Ulinzi na Usalama kuchukua hatua za haraka kwa wanaotumia mitandao na teknolojia vibaya, akikemea pia wingi wa Wanaharakati kutoka nje ya nchi wanaojaribu kuingilia mambo ya ndani ya Tanzania na kutaka kuivuruga amani.  Rais Samia amesema hayo Jijini Dar es salam leo May 19, 2025 wakati akizindua Sera ya Mambo ya Nje ya Mwaka 2001 (Toleo la 2024), ambapo amesema hatotoa nafasi kwa watovu wa adabu kutoka nje ya nchi kuja kujaribu kuvuruga amani, utulivu na usalama uliopo nchini Tanzania. “Tusiwe shamba la Bibi kwamba Mtu anaweza kuja Tanzania akasema analolitaka, lipo Tanzania halipo, Watu wakajisemea tu, tumeanza kuona mwenendo wa Wanaharakati ndani ya Ukanda huu kuanza kuvamia na kuingilia mambo yetu huku, sasa kama kwao wameshadhibitiwa wasije kutuharibia, tusitoe nafasi walishavuruga kwao, nchi iliyobaki haijaharibika ni hapa kwetu, niwaombe Vyombo vya Ulinzi na Usal...

Kamati Ya Ushauri wa Kisheria Ngazi ya Mkoa na Wilaya na Kliniki ya Sheria Bila Malipo Yazinduliwa Singida

*• “Tutatoa huduma hii bure na kwa weledi mkubwa” – Mwanasheria Mkuu wa Serikali* Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida imezindua rasmi Kamati ya Ushauri wa Kisheria ngazi ya Mkoa na Wilaya na Kliniki ya Sheria bila malipo kwa Wananchi wa Mkoa wa Singida. Uzinduzi huo umefanyika tarehe 19 Mei, 2025 katika viwanja vya Stendi ya zamani Manispaa ya Singida. Akizungumza katika uzinduzi huo, Mgeni Rasmi na Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe. Halima O. Dendego ameipongeza Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa kuuchagua Mkoa wa Singida na kuja kuzindua Kamati ya Ushauri wa Kisheria ngazi ya Mkoa na Wilaya kwa kuwa ni fursa kwa wananchi wa mkoa huo kutatuliwa changamoto mbalimbali za kisheria zinazowakabili.  *“Kipekee naishukuru Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Kamati ya Ushauri wa Kisheria ngazi ya Mkoa na Wilaya kwa kunifikiria na kunipa wajibu huu mkubwa wa kuwa Mgeni Rasmi katika Halfa hii ya Uzinduzi wa Kamati na Kliniki ya ...