• Ajira zamwagwa kwa Watanzania • Minada ya Madini kurejeshwa • Mauzo yapaa Na Vicky Kimaro, Tume ya Madini. “Serikali imefanya uwekezaji mkubwa katika Sekta ya Madini, tumenunua mitambo mikubwa, mitano imeshafika nchini, kumi ipo njiani inakuja, mitambo hii itawarahisishia wachimbaji wadogo kupata taarifa za uchimbaji na kuwaepusha na hasara,” kauli ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, aliyoitoa Oktoba 21, 2024 ambapo aliongeza, “Mitambo hii ikifika itagawanywa pote, ila nimemtaka Waziri (Mheshimiwa Anthony Mavunde) atenge mitambo miwili kwa ajili ya vijana na mmoja kwa ajili ya wanawake. Kauli hiyo ya Rais Samia ni muendelezo wa dhamira yake ya dhati ya kuhakikisha Sekta ya Madini inaendelea kuongeza mchango wake katika ukuaji wa uchumi wa nchi. Mpango wa Serikali ni kuhakikisha kuwa sekta hii inachangia asilimia 10 au zaidi katika Pato la Taifa ifikapo 2025. Ukuaji wa Sekta ya Madini umeongezeka kutoka asilimia 9.4 Mwaka 2021 hadi ku...
Marato tv - Sauti ya Jamii