Skip to main content

Posts

Showing posts from March 7, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Prof. Kabudi Awahimiza Diaspora Kuwekeza Nchini Tanzania

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Kazi Maalum), Prof. Palamagamba Kabudi, amewahimiza Watanzania wanaoishi nje ya nchi (Diaspora) kuendelea kuwekeza nchini na kushiriki kikamilifu katika juhudi za maendeleo ya taifa. Amesema Watanzania walioko ughaibuni wana nafasi kubwa ya kuchangia ukuaji wa uchumi wa nchi kupitia mitaji, utaalamu na uzoefu walioupata nje ya nchi. Prof. Kabudi ameyasema hayo wakati wa mkutano na Watanzania wanaoishi jijini London, Uingereza, ambapo aliwasilisha salamu za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, pamoja na ujumbe wa serikali kwa Watanzania waishio ughaibuni. Amesema serikali inaendelea na juhudi za kurekebisha, kujenga upya na kufanya maboresho katika sekta mbalimbali. Aidha, Profesa Kabudi amewataka Watanzania wanaoishi nje ya nchi kununua hisa katika miradi ya maendeleo inayotekelezwa nchini, kushiriki katika uwekezaji wa pamoja na kutumia utaalamu wao kwa kushirikiana na wataalamu waliopo Tanzania kusaidia maendeleo ya sekta m...

Dkt. Mwigulu Asisitiza Maadili na Umoja

*Ni katika mashindano ya kuhifadhi Qur’an wilayani Kondoa WAZIRI MKUU Dkt. Mwigulu Nchemba amesema ni muhimu wa kuendeleza maadili, elimu ya dini na mshikamano wa jamii kupitia mashindano ya kuhifadhi Qur’an tukufu. Ameyasema hayo leo (Jumamosi, Machi 7, 2026) wakati akizungumza na wananchi waliohudhuria mashindano hayo yaliyofanyika uwanja wa Kambi ya Fisi kwenye kijiji cha Bukulu, kata ya Soera, wilayani Kondoa, mkoani Dodoma. Amesema mashindano ya aina hiyo yana mchango mkubwa katika kukuza malezi bora kwa vijana pamoja na kuimarisha misingi ya maadili mema katika jamii. “Serikali inaunga mkono juhudi za taasisi za dini katika kuimarisha elimu ya kiroho na maadili kwa vijana. Malezi ya kidini yana nafasi muhimu katika kujenga jamii yenye amani, uvumilivu na mshikamano,” amesema Waziri Mkuu ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mashindano hayo. Akielezea umuhimu wa mashindano hayo, Waziri Mkuu amesema katika Qur’an sura ya pili aya ya 185, imeelezwa kuwa Qur’an imeshushwa ndani ya mwezi ...

Waziri Kabudi Afanya Mazungunzo na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola

  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Kazi Maalum), Prof. Palamagamba Kabudi, amefanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola, Mhe. Shirley Botchwey, yaliyolenga kuimarisha ushirikiano katika masuala ya utawala bora, demokrasia na maendeleo ya pamoja. Katika mazungumzo hayo, pamoja na mambo mengine, Prof. Kabudi amebainisha kuwa Tanzania inaendelea kuthamini nafasi na mchango wa Jumuiya ya Madola katika kukuza ushirikiano wa kimataifa na kuimarisha taasisi za kidemokrasia.  Kwa upande wake, Mhe. Botchwey amepongeza ushiriki na mchango wa Tanzania katika shughuli za Jumuiya ya Madola na kuahidi kuendeleza ushirikiano na nchi wanachama. Mazungumzo hayo yamefanyika jijini London, ambako Prof. Kabudi yuko kwa ziara ya kikazi kushiriki mikutano ya Jumuiya ya Madola inayojumuisha nchi wanachama 56, ikiwemo Kikao cha 72 cha Kamati ya Mawaziri wa Jumuiya ya Madola (CMAG) kitakachofanyika Machi 7, 2026 na Mkutano wa 26 wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi wanachama wa Jumuiya hiyo ut...

Mbunge Agness Awafikia Wanawake Wa Kikristo Kwa Kuwashika Mkono

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mara, Mheshimiwa Agnes Marwa, ameungana na wanawake wa mashirika ya Kikristo katika Musoma kuadhimisha International Women's Day kwa shangwe na mshikamano mkubwa. Katika maadhimisho hayo yaliyowakutanisha wanawake wa Christian Council of Tanzania (CCT) pamoja na WAWATA wa Manispaa ya Musoma, Mheshimiwa Mbunge alitoa pongezi kwa wanawake kwa mchango wao mkubwa katika kuimarisha maadili ya jamii, familia na maendeleo ya Taifa. Akizungumza katika sherehe hizo, Mheshimiwa Agnes Marwa aliwahimiza wanawake kuendelea kushikamana, kujiamini na kutumia fursa mbalimbali za maendeleo ili kujiletea ustawi wao na jamii kwa ujumla. Katika kuonesha dhamira yake ya dhati ya kuunga mkono shughuli za wanawake na taasisi za kijamii, Mheshimiwa Mbunge alitoa mchango wa shilingi milioni 2 na laki 4 (Tsh 2,400,000) kwa ajili ya ununuzi wa tent, hatua itakayosaidia kuimarisha uendeshaji wa shughuli mbalimbali za kijamii na kiroho katika Manispaa ya Musoma. Wanawake walioshir...

SADC Yahimiza Mtangamano Wenye Matokeo Chanya Katika Kikanda

Mkutano wa Kamati ya Makatibu Wakuu wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) umeanza jijini Pretoria, Afrika Kusini Machi 07, 2026, chini ya Uenyekiti wa Balozi Tebogo Seokolo ambaye ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uhusiano wa Kimataifa na Ushirikiano ya Afrika Kusini.  Katika hotuba ya ufunguzi Balozi Seokolo alihimiza Nchi Wanachama kuchukua hatua za kukuza zaidi mtangamano wa Kikanda kwa kuongeza kiwango cha Biashara baina ya Nchi za SADC kutoka kiwango cha sasa cha asilimia 23.   Kwenye hotuba hiyo alihimiza umuhimu wa Nchi Wanachama kuimarisha sekta za Viwanda, kwa kuzingatia kwamba sekta hiyo inakua kwa kasi na inachangia asilimia 11 ya pato la ndani (GDP) la nchi za SADC.  Aidha, alisisitiza umuhimu wa kuboresha miundombinu haswa barabara ili kurahisisha mwingiliano na mtangamano wa watu na biashara ndani ya Kanda; na usalama wa chakula na lishe, haswa ikizingatiwa kuwa watu milioni 58 katika kanda ya SADC wana changamoto ya usalama wa chakula. Kiong...