Skip to main content

Posts

Showing posts from September 27, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Majaliwa Ashiriki Mbio za Hisani za Saifee

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa leo Septemba 28, ameshiriki katika mbio za hisani za Saifee Marathon zilizoanzia na kuishia katika viwanja vya green park Oysterbay, jijini Dar es Salaam. Lengo la marathon hizo ni kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa kuchukua hatua za kujikinga na magonjwa ya moyo na mishipa ya damu kwa kutoa elimu ya afya kwa wananchi kuhusu mtindo bora wa maisha. Lengo lingine ni kuimarisha uchunguzi wa mapema wa magonjwa yasiyoambukiza, pamoja na kuhimiza ushirikiano wa wadau mbalimbali katika mapambano dhidi ya magonjwa yasiyoambukiza. 

Mgombea Urais kupitia CUF ahamasisha Watanzania wakapige kura

📌 Asema maandamano ni njia ya kuvuruga Amani ya nchi.  Na MASHAKA MHANDO, Tanga  MGOMBEA urais kupitia Chama Cha Wananchi (CUF) Gombo Semandito Gombo amewataka watanzania kutosusia uchaguzi mkuu kwani mabadiliko ya kweli yanatoka katika sanduku la kura. Kauli hiyo ameitoa wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari mkoani Tanga kuhusu tathimini ya awamu ya kwanza ya kampeni za ugombea urais, ubunge na udiwani alizotembelea katika mikoa 14 aliyopita hapa nchini. Amesema ni muhimu wapuuzie watu ambao wanafanya ushawishi wa kususia uchaguzi na kufanya maandamano ambayo yatasababisha kuvuruga amani iliyopo wakati amani iliyopo imeundwa na waasisi wa Taifa. "Niwaombe watanzania jitokezeni kushiriki kwenye uchaguzi mkuu October 29 mwaka huu, kwenda kupiga kura ni haki yako ya msingi na ya kikatiba, sisi wapinzani tunatakiwa kushinda uchaguzi kwa njia ya amani na utulivu, nendeni mkapige kura," amesema Mgombea huyo Urais. Alisema kuwa katika tathimini hiyo ya mikoa 14 aliyotembel...

MSD yawadai Bil. 6.2 watoa huduma za afya

Na MASHAKA MHANDO, Korogwe BOHARI ya dawa nchini (MSD) Kanda ya Tanga, imesema inakabiliwa na changamoto ya ufanisi wa kazi kutokana na madeni inayowadai vituo vya kutoa huduma ya afya ya zaidi ya Sh. 6,242,077,935.35 katika kanda hiyo. Akitoa  salamu kwenye kikao baina ya MSD na wadau wake, Kaimu Meneja wa bohari hiyo Kanda ya Tanga, Granty Mwapwele alisema fedha hizo zinatokana na kusambaza bidhaa za afya kwenye vituo vyote 568 vinavyohudumiwa na MSD Kanda ya Tanga katika mwaka wa fedha wa 2024-2025. "Bohari ya dawa Kanda ya Tanga imekumbwa na changamoto ya kwa baadhi ya vituo vyote vya kutolea huduma kuwa na madeni makubwa hali hii inaathiri kiasi kikubwa huduma zetu," alisema. Alisema MSD Kanda ya Tanga inahudumia jumla ya Halmashauri 12 zenye jumla ya vituo vya kutolea huduma za afya 568 kwa kusambaza bidhaa za afya mara sita kwa mwaka pale wanapohitaji. Alitaja vituo wanavyovihudumia kuwa ni pamoja na hospitali ya rufaa Bombo, hospital ya magonjwa maalum, hospitali za w...

Balozi Nchimbi Kuzisaka Kura za Ccm Ndani ya Jiji la Dar es Saalam

 Mgombea Mwenza wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt Emmanuel John Nchimbi, leo Septemba 28,2025 anaendelea na Mikutano yake ya Kampeni za Urais ndani ya Jiji la Dar es Salaam, ili kusaka Kura za Ushindi wa Chama hicho Tawala. Dkt Nchimbi katika Ratiba yake anaanzia Wilaya ya Kigamboni, kisha ataelekea Mbagala kwa mkutano utakaofanyika katika eneo la Maturubai–Polisi. Baadaye, atahitimisha siku kwa mkutano mkubwa wa hadhara utakaofanyika Temeke, katika uwanja wa Mwembe Yanga. Mikutano ya Dkt Emmanuel John Nchimbi inalenga kuwasilisha sera na ahadi za CCM kwa wananchi, pamoja na kuhamasisha mshikamano na ushiriki wao katika uchaguzi mkuu ujao.

Tanzania Yapata Medali ya Dhahabu Apimondia 2025

Copenhagen, Denmark, 27 Septemba 2025 — Tanzania imepata heshima kubwa ya kimataifa baada ya kutunukiwa Medali ya Dhahabu katika Kongresi ya 49 ya Apimondia iliyofanyika katika ukanda wa Scandinavia (Sweden, Denmark na Norway). Tuzo hiyo ilitangazwa Septemba 27, 2025 ambapo banda la Tanzania lilishinda katika kipengele cha Large Stand (zaidi ya mita 36 za mraba) kutokana na ubunifu na ubora wa maonesho ya mazao ya nyuki yaliyovutia wageni kutoka mataifa mbalimbali duniani. Cheti cha ushindi kimetolewa na Rais wa Shirikisho la Apimondia, Jeff Pettis, kwa kutambua mchango wa Tanzania katika kukuza tasnia ya nyuki kimataifa. Akizungumza mara baada ya kupokea cheti hicho, Kamishna Msaidizi anayesimamia Rasilimali za Nyuki, Hussein Msuya, alisema ushindi huo ni ishara kuwa Tanzania imeanza kuthibitisha nafasi yake kama kitovu cha uzalishaji na usindikaji wa mazao ya nyuki barani Afrika na duniani. “Ushindi huu unatarajia kuongeza thamani ya bidhaa za nyuki za Tanzania sokoni, hususan asali,...

Wasira: Dk. Samia Dereva Mzoefu Mpeni Usukani Atufikishe Pazuri

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Stephen Wasira amesema kwa miaka minne, Rais Dk,. Samia Suluhu Hassan amefanya mambo makubwa hivyo Watanzania wanapaswa kumrudisha madarakani aendelee kuleta maendeleo mengi. Wasira amesema hayo leo Septemba 27, 2025 alipokuwa akizungumza na viongozi na wanachama wa CCM wa Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro, mjini Moshi. "Hapa Moshi kwa muda wa miaka minne amejenga shule mpya nne za msingi, sio kilimanjaro ni hapa hapa Moshi, amejenga madarasa mapya kwa sababu ya watoto kuongezeka 40, mjini hapa na nyinyi hamkuchangishwa. "Kwenye afya amejenga zahanati tisa mjini Moshi, amejenga vituo vipya vya afya vitatu na amerekebisha hospitali na kuweka vifaa katika vituo vya afya na hospitali. Vituo vya afya vilivyojengwa chini ya Mama Samia ni kama hospitali tu, ukienda utakuta vifaa vyote vya hospitali viko mule. "Kwa kufanya alivyofanya vifo vya mama wajawazito vimepungua kutoka 500 kwa vizazi 100,000 mpaka 100. Huyo ndiye Sam...

Dkt.Biteko aelezea miaka 10 ya mapinduzi Bukombe

📌 Ataja sababu za kumchagua Dkt. Samia kwa kura nyingi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Bukombe kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Doto Mashaka Biteko amesema kuwa kwa Serikali ya CCM inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan imefanya jitihada kubwa ya kuwaletea maendeleo wananchi wa Wilaya ya Bukombe ikiwa ni pamoja na kutoa fursa za kukuza uchumi wa Wilaya hiyo. Dkt. Biteko amesema hayo Septemba 27, 2025 wakati wa mkutano wa kampeni katika Kata ya Katente wilayani Bukombe mkoani Geita ikiwa ni sehemu Kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani utakaofanyika Oktoba 29, mwaka huu. Amesema mwaka 2015 Kata ya Katente, Igulwa na Kata zote zilizopo maeneo ya mjini zilikuwa na kiwango duni sana cha maendeleo ikilinganishwa na maendeleo yaliyofikiwa sasa.  Amesema Wilaya ya Bukombe ilikuwa na shule moja ya kidato cha tano na sita, hospitali moja, zahanati nne huku umeme ukiwa katika vijiji saba pekee. Amesema Serikali ya CCM imekuwa ikifanya jitihada kubwa ya  kuteke...