Skip to main content

Posts

Showing posts from December 22, 2024

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Waziri Gwajima apongeza Mchango wa Shirika la Kivulini katika Mapambano dhidi ya Ukatili wa Kijinsia

  Serikali imepongeza Mchango wa shirika la kutetea haki za wanawake na watoto la Kivulini katika kuinua uchumi wa kaya na kupunguza vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto,mimba pamoja na ndoa za utotoni. Pongezi hizo zimetolewa na Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum Dkt.Dororthy Gwajima wakati wa ziara yake katika ofisi za shirika hilo zilizoko nyamhongolo Jijini Mwanza. Akizungumza na Menejimenti na wafanyakazi wa shirika la Kivulini,Dkt.Gwajima ameahidi kuwa serikali itaendelea kuunga mkono shirika hilo ikiwemo kuhakikisha linapata ufadhili zaidi ili kuongeza ufanisi kwenye shughuli za kupambana na ukatili wa kijinsia pamoja na kuinua uchumi wa kaya. ‘’Kivulini wanafanya kazi kubwa ambayo haijasimuliwa vizuri make sio watu wa kupiga kelele,Niseme natambua kwa ukubwa kazi mnayofanya,ushirikiano wenu,Tuna Jukumu moja tu la Kuisemea Kivulini ili isikike na iendelee kupata ufadhili kwa sababu kazi zake ziko kwenye Jamii huko na ni kati ya mashirik...

Tutakukumbuka Daima Ndugu yetu Rashid Msomi Bwana aka Osama

GMTV inatoa Pole nyingi kwa familia ya mzee Msomi Bwana kufuatia kifo cha kijana wao mpendwa Rashid Msomi Bwana. DAIMA tutamkumbuka ndugu yetu kwa upendo wake na ucheshi wake kwetu Tunamshuru mwenyezi Mungu kwa maisha ya ndugu yetu hapa duniani Ingawa ni muda mfupi mno lakini ametuachiabkumbukizi kubwa sisi tuliobaki. Tumwombea mwenyezi Mungu aweze umpokea na kumpa pumziko jema mbinguni

Balozi Dkt. Nchimbi ateta na Kadinali Rugambwa

*SALAAM KWA KARDINALI* Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Tabora, Mwadhama Protase Kardinali Rugambwa, akizungumza na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi.  Mazungumzo hayo yalifanyika Ijumaa, Desemba 20, 2024, wakati Balozi Nchimbi alipofika kumsalimia Kardinali Rugambwa, ofisini kwake, Uaskofuni, mjini Tabora,

Mkuu wa mkoa Sindiga akabidhi Hati na Funguo za Nyumba kwa Kaya 80

 Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Queen Cuthbert Sendiga leo Disemba 22, 2024 amegawa hati za nyumba, funguo za nyumba, majiko ya gesi pamoja na miti ya matunda Kwa kaya 89 za walioathirika wa maporomoko ya tope ya mlima Hanang kwa ambao hawakupatiwa hati wakati wa ufunguzi wa nyumba hizo. RC Sendiga, amefanya zoezi hilo ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb) , Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliyoyatoa Disemba 20, 2024 wakati wa Uzinduzi wa Makazi hayo Mapya ya waathirika wa maporomoko ya matope. Akizungumza na wanufaika wa nyumba hizo RC Sendiga amewaasa kuishi kwa upendo na amani, wanapaswa kuzitunza nyumba hizo ikiwemo kuzingatia usafi na kuboresha mazingira yanayowazunguka. Baadhi ya wanufaika wa nyumba hizo wametoa shukrani zao kwa Mhe. Samia Suluhu Hassan ,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kusema kuwa wamezifurahia huku wakiahidi kuzitunza na kutunza mazingira hayo.

Kufeli Kwa Breki Chanzo cha ajali iliyosababisha vifo vya watu 11 Kagera

Na Angela Sebastian; Bukoba  Watu 11 wamefariki dunia na wengine 16 kujeruhiwa baada ya basi ya kampuni ya Copco one yenye namba za usajili T857DHW aina ya Scania linalofanya safari zake kutoka Kigoma kwenda mjini Bukoba kufeli breki wakati limesimama kumshusha abiria na kuanza  kurudi kinyumeyume na kuacha njia kisha kupinduka. Mkuu wa mkoa wa Kagera Hajat Fatma Mwassa alieleza hayo (leo) jana wakati akiongea na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali ofisini kwakwe mjini Bukoba ambapo alisema ajali hiyo imetokea jana jumamosi Desemba 21,2024 majira ya saa nane mchana katika kijiji cha Kabukome kata Nyarubungo eneo la mlima wa pori la Kasindaga wilaya ya Biharamulo. Hajat Mwassa alisema gari lenye namba za usajili T857 DHW Scania basi mali ya Roja line travel company Ltd likiendesha na Saidi Mkenda (41) likitokea mkoani Kigoma kwenda Bukoba ambapo, dreva huyo alisimama kushusha abiria ambae alikuwa mtoto aliyepitilizwa kwenye kituo, ndipo gari lilisima ila liliashindwa kupan...