Skip to main content

Posts

Showing posts from August 31, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

MASABALA MZEE MASHUHURI KAGERA ATUNUKIWA TUZO BAADA YA KUTOA ARDHI KWA AJILI YA BWENI LA WANAFUNZI-KIBETA

 Na Angela Sebastian  Mzee mashuhuri wa Mkoa wa Kagera, Joseph Masabala, amepewa hati ya shukrani na tuzo maalum baada ya kutoa sehemu ya ardhi yake kwa ajili ya ujenzi wa Bweni la wanafunzi katika Shule ya Sekondari Kibeta, Manispaa ya Bukoba, hatua inayotajwa kuwa mchango mkubwa katika kuboresha mazingira ya elimu kwa wanafunzi wa eneo hilo. Tuzo hiyo imetolewa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Wazo Michael Mwang’onda, wakati Mwenge wa Uhuru ulipotembelea na kuzindua miradi ya maendeleo katika Manispaa ya Bukoba. Mzee Masabala pamoja na mkewe, Lushaka Masabala, walipokea hati hiyo ya shukrani na tuzo kwa niaba ya familia yao. Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mwang’onda ameipongeza familia ya Mzee Masabala kwa uamuzi wao wa pamoja wa kutoa ardhi hiyo kwa ajili ya maendeleo ya elimu, akieleza kuwa hatua hiyo ni mfano wa uzalendo na kujitolea kwa jamii. Amesema ardhi hiyo haitakuwa tu sehemu ya ujenzi wa mabweni, bali itakuwa mkombozi wa elimu kwa kizazi cha sasa...

RAIS SAMIA KUSHIRIKI SHEREHE ZA UAPISHO WA RAIS HICHILEMA WA ZAMBIA

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo tarehe 01 Septemba, 2026, anaondoka nchini kuelekea Lusaka, Zambia kuhudhuria sherehe za Uapisho wa Rais Mteule wa Jamhuri ya Zambia, Mheshimiwa Hakainde Hichilema. Katika Uchaguzi Mkuu wa Zambia uliofanyika tarehe 13 Agosti, 2026, Rais Hichilema alichaguliwa kuiongoza nchi hiyo kwa muhula mwingine wa miaka mitano. Ziara ya Rais Dkt. Samia inaendeleza uhusiano wa kindugu na kihistoria kati ya Tanzania na Zambia, unaojengwa katika misingi ya umoja, mshikamano, ujirani mwema na ushirikiano wa kikanda.

DR. MWINYI SEALS NEW CHAPTER IN TANZANIA-SERBIA RELATIONS IN BELGRADE TALKS

 By Prosper Makene The President of Zanzibar and Chairman of the Revolutionary Council, Dr. Hussein Ali Mwinyi, has called for a new chapter in Tanzania-Serbia relations, urging Serbian investors to turn more than six decades of diplomatic friendship into concrete trade and investment. Speaking during a high-level meeting with the Serbian Chamber of Commerce and Industry in Belgrade on Sunday, led by Vice President Mr. Mihailo Vesović, Dr. Mwinyi said the time has come for the two countries to move beyond history and focus on economic results. Dr. Mwinyi said Tanzania is ready to deepen economic cooperation through real projects in trade, production, processing, and joint ventures between companies from both nations. He outlined major opportunities in agriculture, mining, energy, manufacturing, infrastructure, tourism, the Blue Economy, spices, and seaweed.  He noted that Tanzania has capacity in maize, sunflower, cashew nuts, and cotton, while Zanzibar offers strong potential...

>MAKAMU WA RAIS, ATEMBELEA OFISI YA MAKAMU WA RAIS MUUNGANO NA MAZINGIRA*

*>AWATAKA WATUMISHI KUACHA KUFANYA KAZI KWA MAZOEA* Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi, amewataka watumishi wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira kuongeza bidii, uwajibikaji na kuachana na utendaji wa kazi kwa mazoea ili kuhakikisha majukumu ya Serikali yanatekelezwa kwa ufanisi na kwa wakati. Makamu wa Rais ametoa wito huo leo, alipofanya ziara yake ya kwanza katika Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), iliyopo Mtumba, jijini Dodoma, ambako alipokelewa na wafanyakazi pamoja na Menejimenti ya Wizara hiyo. Amesisitiza umuhimu wa watumishi kubadili mitazamo na namna ya kufanya kazi, akitaka kila mmoja kuwa mbunifu na kuweka mipango inayolenga kuleta matokeo yanayoonekana kwa wananchi na Taifa kwa ujumla. Makamu wa Rais amewasihi watumishi kutumia nafasi zao kutoa huduma yenye thamani kwa watanzania na kutambua dhamana waliyonayo katika kuwahudumia wananchi. Pia amewataka kubadili mitazamo na namna ya kufikiri, kuwa wabuni...

WAZIRI MAVUNDE AZINDUA PROGRAMU YA KESHO ILIYO NJEMA KATIKA SEKTA YA MADINI (MBT)

▪️Azindua na Zoezi la Urushaji wa Helikopta ya Utafiti wa Madini ya Barrick  ▪️Maeneo ya Leseni za Vijana,Wanawake na Wenye Ulemavu Kufanyiwa Utafiti kwa Helikopta ▪️Rais Dkt. Samia Apongezwa kwa Maelekezo na Maono Yake Sekta ya Madini ▪️Baraza la Dhahabu Duniani Lavutiwa na Programu ya MBT ▪️Waziri Mavunde Aagiza Mitambo ya Uchorongaji ya STAMICO Kufika Mara Baada ya Utafiti Kukamilika 📍Nyamongo, Mara.  Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde, amezindua rasmi Programu ya Mining for a Brighter Tomorrow (MBT), maarufu kama “Kesho Iliyo Njema,” na kueleza kuwa programu hiyo ni hatua ya kimkakati ya Serikali katika kufungua milango mipya ya fursa na uwezeshaji kwa vijana, wanawake na watu wenye mahitaji maalum kushiriki kikamilifu katika Sekta ya Madini na kwamba programu inalenga kuwasaidia walengwa kuondokana na uchimbaji wa kubahatisha na kuelekea kwenye uchimbaji wenye tija, unaotumia maarifa, teknolojia na taarifa sahihi za kijiolojia, huku Serikali ikiendelea kuweka mazingi...

MUSWADA WA SHERIA YA MIKOPO KWA DHAMANA ZA MALI ZINAZOHAMISHIKA WAWASILISHWA BUNGENI

 Na Joseph Mahumi na Peter Haule, Dodoma Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), amewasilisha Bungeni Muswada wa Sheria ya Mikopo kwa Dhamana za Mali Zinazohamishika wa Mwaka 2026, unaolenga kuweka mfumo bora wa usimamizi wa mikopo inayotolewa kwa kutumia mali zinazohamishika kama dhamana. Akiwasilisha Muswada huo Bungeni jijini Dodoma, Mhe. Balozi Omar amesema Sheria hiyo inayopendekezwa inalenga kuongeza matumizi ya huduma za benki nchini kutoka asilimia 22 mwaka 2023 hadi asilimia 50 ifikapo mwaka 2030. Mhe. Balozi Omar amesema pia Muswada huo unalenga kuongeza uwiano wa mikopo inayotolewa kwa sekta binafsi dhidi ya Pato la Taifa kutoka asilimia 22.5 mwaka 2024 hadi asilimia 50 ifikapo mwaka 2030, sambamba na kuongeza ajira na kuchochea ukuaji wa sekta ya fedha kufikia asilimia 20 ifikapo mwaka 2030, kutoka asilimia 17.1 mwaka 2024. Alisema kuwa hatua hiyo ni muhimu katika kupanua wigo wa wananchi na wafanyabiashara kupata mikopo kwa kutumia mali zinazohamishika kam...

SUA YAWEKA MKAZO TAFITI, UBUNIFU KUTATUA CHANGAMOTO ZA JAMII

 MAKAMU Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), Prof. Raphael Chibunda, amesema chuo hicho kinaendelea kuweka mkazo katika utafiti, ubunifu, sayansi na teknolojia ili kutatua changamoto za jamii na kuchangia maendeleo ya taifa. Prof. Chibunda amesema hayo leo, Agosti 31, 2026, wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Idara ya Habari MAELEZO jijini Dodoma, akieleza kuwa SUA kwa sasa inatekeleza miradi 172 ya utafiti kwa kushirikiana na taasisi na wadau wa ndani na nje ya nchi. Amesema tafiti hizo zinagusa maeneo mbalimbali yakiwemo kilimo, mifugo, afya, uvuvi, misitu, rasilimali maji, mabadiliko ya tabianchi na masoko ya mazao, huku zikilenga kuongeza tija, kuboresha maisha ya wananchi na kutoa ushahidi wa kusaidia Serikali katika sera na mipango ya maendeleo. Katika kilimo, amesema SUA imefanya tafiti za mbegu zinazostahimili ukame, wadudu na magonjwa, pamoja na uzalishaji wa bidhaa zitokanazo na mimea, lishe na udhibiti wa visumbufu vya mazao na mifugo. Pia, chuo ...