Skip to main content

Posts

Showing posts from March 29, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Rais Dk. Samia amemwaga fursa nyingi kwa vijana - Mkalipa

Na: Mwandishi Wetu, Pangani Fursa nyingi za uwezeshaji vijana kiuchumi zimemwagwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan katika maeneo mbalimbali nchini ili vijana waweze kuwa na vipato vya uhakika. Hayo yamesemwa na Katibu wa Umoja wa Vijana Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), wilaya ya Pangani, Nasri Mkalipa katika ziara ya kiutendaji aliyoifanya Machi 29, 2026, katika Kata za Bweni na Ubangaa wilayani Pangani. Mkalipa amesema ni dhamira ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kuwafanya vijana kuwa na uchumi imara ndiyo maana ameboresha sekta za elimu, utoaji mikopo ya elimu, fursa za ajira ili vijana wawe na maisha mazuri. "Rais wetu Dk. Samia Suluhu Hassan ni Rais wa aina yake. Ameongeza fursa nyingi za uwezeshaji uchumi kwa vijana na wanawake ili wawe na uchumi imara. Miradi mingi ya maendeleo inayotekelezwa inawagusa vijana, hivyo ni jukumu letu vijana kutumia fursa hizo kuboresha maisha yetu," amesema Mkalipa. Sambamba na hilo, Mkalipa amewaasa Vijana kujiepusha na makundi hatarishi bali wa...

Mfumo utabiri kiasi cha maji nyenzo ya takwimu sahihi za maji

Na: Dk. Reubeni Lumbagala Maji ni raslimali ya asili ambayo inatumika katika maeneo mengi muhimu yanayochagiza maendeleo. Upo umuhimu wa wananchi kuelimishwa ili kuielewa sekta ya maji kwa mapana badala ya kuona maji kama huduma ya kijamii pekee kwa shughuli za nyumbani kama kupikia, kufulia na kuogea.  Maji ni zaidi ya matumizi hayo yaliyozoeleka kwa baadhi ya watu. Kwa nchi yetu yenye vyanzo vingi vya maji lakini wakati huo huo ina idadi kubwa ya watu na shughuli nyingi za kijamii na kiuchumi zinazohitaji maji, takwimu sahihi za maji zinapaswa kuwepo ili tusiwe watu wa kubahatisha kuelewa kiasi cha maji tulichonacho nchini na mahitaji halisi ya maji kufanikisha mipango na shughuli mbalimbali za maendeleo. Bila takwimu sahihi tutakwama na hatutakuwa na uhakika wa kufanikisha mambo yetu kama nchi. Katika masuala ambayo Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amesisitiza kuyasimamia kikamilifu na kuyapa kipaumbele ni pamoja na matumizi ya teknolojia za kisasa katika shughuli mbalimbali za maji ...

Dmdp II Yaleta Mapinduzi ya Miundombinu Manispaa ya Temeke

‎Dar es Salaam ‎Mradi wa Uendelezaji Jiji la Dar es Salaam Awamu ya Pili (DMDP II) unatekeleza ujenzi wa barabara zenye urefu wa Kilomita 51.2 kwa kiwango cha lami na zege katika Kata zaidi ya nane (8) na mitaa isiyopungua 20 katika halmashauri ya Manispaa ya Temeke.  ‎Hayo yamebainishwa na Meneja wa TARURA wilaya ya Temeke, Mhandisi Paul Mhere ambapo ameeleza kuwa wameingia mikataba ya ujenzi wa barabara kwa gharama ya shilingi Bilioni 97.176. ‎"TARURA wilaya ya Temeke tuna mtandao wa barabara Kilomita 648.45, tuna majimbo matatu (3) ambayo ni Temeke, Chamazi na Mbagala na kote miradi inaendelea utekelezaji wake upo zaidi ya asilimia 75 isipokuwa Mbagala na Yombo mikataba ilisainiwa mwezi wa Aprili 2025 utekelezaji wake upo asilimia 32", amesema. ‎Ameongeza kuwa zaidi ya Kilomita 166 za barabara wilayani humo ni lami na zege, barabara za zege zinahimili uzito wa aina yoyote na zinadumu muda mrefu huku zikipunguza matengenezo ya mara kwa mara na kuondolea gharama serikali. ‎...

Waziri Mkuu: Coco Beach Haiuzwi, ni ya Wananchi

Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, ametoa ufafanuzi rasmi kuhusu hatma ya eneo la Coco Beach, akisisitiza kuwa halitauzwa kwa mwekezaji yeyote bali maboresho yatafanyika kwa manufaa ya wananchi waliopo katika eneo hilo. Amesema hayo leo, Machi 29, 2026, alipotembelea eneo la Coco Beach jijini Dar es Salaam, ambapo alizungumza na wajasiriamali wadogo wanaofanya shughuli zao katika eneo hilo na kusikiliza kero zao mbalimbali. “Coco Beach haiuzwi. La kwanza niwaondolee hofu—hapauzwi, wala hakuna mwekezaji mwingine zaidi yenu nyinyi wenyewe. Hakuna atakayekuja kutoa maelekezo zaidi ya yale yaliyotolewa na Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan. Hapa hapauzwi,” amesisitiza. Aidha, Dkt. Mwigulu amesema Serikali itaendelea kutekeleza maelekezo ya Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa lengo la kuhakikisha Watanzania wananufaika na maboresho yanayofanyika katika eneo hilo. “Sisi wasaidizi wa Mheshimiwa Rais tutaendelea kuhakikisha Watanzania wanapata lile tabasamu la Mama ambalo ame...

Serikali Yahimiza Matumizi ya Vyakula vya Asili Kuimarisha Afya

Na,Saleh Lujuo-DODOMA MKURUGENZI wa Huduma za Uhamasishaji wa Afya (Elimu ya Afya kwa Umma), Dkt. Rahma Ahmed Hingora, amewahimiza Watanzania kurejea katika matumizi ya vyakula vya asili kama sehemu muhimu ya kujenga afya bora, kuzuia magonjwa, na kusaidia matibabu kwa njia salama na endelevu. Dkt. Hingora ametoa msisitizo huo kwa Watanzania leo Jijini Dodoma ambapo amesema vyakula vya asili vina mchango mkubwa katika kuimarisha afya ya mwili na vinaweza kutumika kama sehemu ya kinga na tiba iwapo vitatumika kwa usahihi. “Tunapaswa kurudisha utamaduni wa kula vyakula vya asili kama maboga, ubuyu na vyakula vingine vinavyopatikana katika mazingira yetu. Hivi ni vyakula vyenye virutubishi muhimu vinavyosaidia kuimarisha kinga ya mwili na afya kwa ujumla,” amesema Dkt. Hingora. Amebainisha kuwa kumekuwa na mabadiliko ya mtindo wa maisha ambapo jamii imekuwa ikipuuza vyakula vya asili na kuelekea zaidi katika matumizi ya vyakula vilivyosindikwa, ambavyo mara nyingi hupoteza virutubisho mu...

Rais Samia Akutana na Balozi wa Italia Nchini

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Italia nchini Tanzania Mhe.Giuseppe Sean Coppola, na ujumbe wake, Ikulu, Dar es Salaam tarehe 29 Machi, 2026.