Skip to main content

Posts

Showing posts from February 17, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Waziri Mkuu Amaliza Ziara Tanga, Aagiza Fagio Lipite Muheza

_Ahimiza Wakuu wa Wilaya wakasikilize wananchi na kutatua kero zao_ WAZIRI MKUU Dkt. Mwigulu Nchemba amemwagiza Waziri wa Nchi (OWM – TAMISEMI), Prof. Riziki Shemdoe arudi Halmashauri ya Muheza na kusafisha watumishi wote waliohusika na ubadhirifu wa fedha za mradi wa jengo la ofisi. Ametoa agizo hilo jana (Jumanne, Februari 17, 2026) wakati akizungumza na viongozi na watumishi wa Mkoa wa Tanga katika kikao cha majumuisho ya ziara yake ya siku tano mkoani humo yaliyofanyika kwenye Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA). “Muheza ndiyo wilaya iliyonidisappoint sana kwa sababu huku kwingine nimekuta upungufu bali kule Muheza ni uharibifu. Mheshimiwa Waziri kesho rudi Muheza, nenda kachukue hatua. Shirikiana na Waziri wa Utumishi, mchukue hatua,” alisisitiza. Dkt. Mwigulu amesema kuna baadhi ya vifaa vilinunuliwa lakini havikufika site (eneo la mradi). “Nondo zenye thamani ya shilingi milioni 9.2 zililipwa kwa mzabuni Saifi Store wa Tanga lakini hazikufikishwa site, maana yake zimechep...

Mtambo wa Oksijeni Waokoa Maisha ya Wananchi Lushoto

Na OWM - TAMISEMI, Lushoto Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu -TAMISEMI Mhe. Prof. Riziki Shemdoe ameshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuokoa maisha yake na wananchi wa Lushoto kwa kutoa fedha zilizowezesha kupatikana kwa mtambo wa kuzalisha hewa tiba ya oksijeni katika Hospitali ya Wilaya ya Lushoto. Prof. Shemdoe ametoa shukrani hizo leo kwa Mhe. Rais wakati alipopewa fursa na Mhe. Waziri Mkuu ya kuwasalimia wananchi wa Lushoto, mara baada ya Mhe. Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba kuzindua rasmi mtambo wa kuzalisha hewa tiba ya oksijeni katika Hospitali ya Wilaya ya Lushoto uliowekwa na Serikali ili kuboresha utoaji wa huduma za tiba kwa wananchi. “Mhe. Waziri Mkuu namshukuru sana Mheshimiwa Rais kwa kutuletea Shilingi Bilioni 5 zilizotuwezesha kupata vituo vya afya, zahanati pamoja na ununuzi wa mtambo huu wa kuzalisha hewa tiba ya oksijeni uliotuzindulia leo,” ameeleza Prof. Shemdoe. Prof. Shemdoe amemueleza Mhe. Waziri Mkuu kuwa, an...

Trc Yaanza Rasmi Usafirishaji wa Mizigo Kwa Kutumia Container Carriers Sgr

Shirika la Reli Tanzania (TRC) limeanza rasmi usafirishaji wa makasha kwa kutumia reli ya Standard Gauge, hatua inayolenga kupanua wigo wa biashara, kupunguza msongamano wa mizigo bandarini na kurahisisha usafirishaji wa mizigo kwenda mikoa ya kati ya nchi. Akizungumza wakati wa kuanza safari ya treni ya kwanza ya makasha kutoka Pugu kuelekea Ihumwa mkoani Dodoma, Kaimu Mkurugenzi wa Usafirishaji wa TRC, Focus Makoye Sahani, amesema treni hiyo inasafiri umbali wa takribani kilometa 420 kutoka Dar es Salaam. Amesema hatua hiyo ni mwanzo wa usafirishaji wa makasha baada ya TRC kuanza kusafirisha abiria pamoja na mizigo mbalimbali ikiwemo kichele kuanzia mwezi Julai, pamoja na saruji inayopakiwa Pugu. “Leo tumeongeza wigo wa biashara kwa kupakia makasha. Kama mnavyoona, treni yetu ya kwanza ya makasha kwenda Ihumwa, Dodoma, leo imeanza safari zake na tuna ofa ya kutosha kutoka kwa mteja wetu wa kwanza,” amesema Sahani. Ameeleza kuwa treni hiyo ina mabehewa 50 yanayobeba jumla ya makasha 1...

Rea yahimiza wananchi kujiunga na huduma ya umeme Tanga

📌 *Wananchi wapewa elimu ya kufanya maombi ya umeme* . 📌 *Wananchi waaswa kutumia umeme kwa tija kujiletea maendeleo* . 📍 *TANGA*  Wakala wa nishati vijijini (REA) umepiga kambi Mkoani Tanga kwa ajili ya zoezi la uhamasishaji wananchi kujiunga na huduma ya umeme. Uhamasihaji huo umefanyika katika maeneo ya pembezoni mwa wilaya ya Tanga mjini kwenye maeneo ya sokoni ,vituo vya bodaboda pamoja na mikutano ya hadhara iliyofanyika maeneo ya ofisi za kata na mitaa  lengo kubwa likiwa ni kuwapa uelewa wananchi juu ya umuhimu wa kujiunga na huduma ya umeme. Akizungumza wakati wa uhamasishaji Afisa maendeleo ya jamii kutoka REA , ndugu Abdulrazack Mkomi alisema , Lengo la wakala kufika wilayani humo ni kuwafikia wananchi na kuzungumza nao juu ya umuhimu wa kutumia fursa ya upatikanaji wa huduma ya umeme ambayo ni nafuu sana na kuwahimiza kujiunga mapema na huduma hiyo ya umeme hasa wakati ambapo mkandarasi bado yupo eneo la mradi. Aidha Mkomi amesema, utekelezaji wa miradi hii ya u...

Dkt. Mwigulu Amezindua Shule ya Amali Majulai-Mlalo

Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba leo Februari 17, 2026 amekagua na kuzindua shule mpya ya sekondari ya amali ya Majulai iliyopo katika kijiji cha Majulai, Kata ya Mwangoi, Tarafa ya Mlalo wilayani Lushoto. Shule hiyo ambayo imejengwa kwa kupitia mradi wa SEQUIP na tayari imesajiliwa, ina walimu sita na wanafunzi 89 ambao walianza masomo Januari 13, 2026.. Mradi huo ambao umegharimu sh. milioni 584.28 ulianza kutekelezwa Oktoba 23, 2024 na hadi sasa umetumia sh. milioni 581.81 na kwamba sh. milioni 2.46 zilizobakia ni za angalizo, kukamilisha ujenzi wa tenki na kulipa mafundi.

Waziri Mkuu: Mawaziri Watabaki Tanga Nikiondoka

  WAZIRI MKUU Dkt Mwigulu Nchemba amewaagiza baadhi ya mawaziri alioambatana nao wabakie mkoani Tanga ili kufuatilia masuala yaliyoibuliwa na wananchi na kuyatafutia ufumbuzi. Masuala hayo yalitokana na hoja zilizoibuliwa kwenye mikutano ya hadhara na wabunge wa mkoa wa Tanga na wananchi mbalimbali kwenye sekta za ardhi, mifugo, kilimo, maji, elimu na barabara. Ametoa agizo hilo leo (Jumanne, Februari 17, 2026) wakati akizungumza na wakazi wa Soni, Bumbuli katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye stendi ya Soni, wilayani Lushoto, mkoani Tanga. Mapema, akijibu hoja kuhusu ubovu wa barabara wilayani Lushoto, Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya alisema Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshatoa kibali cha kuanza ujenzi wa pande mbili wa barabara ya Soni - Bumbuli- Dindira hadi Old Korogwe. “Barabara hii ilishatangazwa na sasa tunakamilisha taratibu za wakandarasi. Zikiwa tayari, mmoja ataanzia Soni kwa kujenga kilometa 22 na mwingine ataanzia Old Korogwe (KwaMeta hadi ...

Wajasiriamali Jimbo la Mtumba Kukopeshwa Bilioni 2 Za Mitaji

▪️Ni kwa ushirikiano wa Ofisi ya Mbunge na CRDB FOUNDATION ▪️Zaidi ya Wananchi 3000 kunufaika na mpango huu ▪️Mbunge Mavunde awataka wanamtumbu kuchangamkia fursa ▪️Mradi mkubwa wa kilimo upo njiani Mbunge wa Jimbo la Mtumba Mh. Anthony Mavunde kwa kushirikiana ya CRDB BANK FOUNDATION kupitia programu ya Imbeju leo wameanza rasmi zoezi la kutoa mikopo ya Shiligi Bilioni 2 kwa ajili ya wajasiriamali wa Jimbo la Mtumba. Akitoa taarifa ya awali, Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB BANK FOUNDATION Bi. Tully Mwambapa amesema taasisi ya CRDB imejipanga kuhakikisha inawafikia wajasiriamali wengi nchini kwa lengo la kuwawezesha mikopo na mitaji ili kuendeleza shughuli za kiuchumi na kwamba Jimbo la Mtumba linakuwa ni moja kati ya majimbo ya mfano ambayo wajasiriamali zaidi ya 3000 kupitia vikundi vyao watapatiwa mikopo ya takribani Shilingi Bilioni 2. Naye Mbunge Mavunde ameeleza dhamira ya mpango huu ni kuunga jitihada kubwa inayofanywa na serikali chini ya uongozi wa Mh. Rais Dkt. Samia S. Hassan ya...

Serikali Yazindua Awamu ya Kwanza ya Mradi wa Kupeleka Nishati Safi Ya Kupikia Kwa Taasisi Zinazohudumia Watu Zaidi ya 100

Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Salome Makamba,  amezindua awamu ya kwanza ya mradi wa kusambaza nishati safi ya kupikia katika taasisi zinazohudumia watu zaidi ya 100, unaohusisha shule 52 za sekondari pamoja na chuo kimoja cha Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) katika mikoa 18 ya Tanzania Bara. Mradi huo ni sehemu ya mpango mkubwa wa kuunganisha miundombinu ya nishati safi ya kupikia katika taasisi 453 wenye thamani ya Shilingi bilioni 25.8, ambapo gharama zote zinagharamiwa kwa asilimia 100 na Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA).  Mhe. Salome Makamba amezindua mradi huo tarehe 17 Februari 2026 katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Kondoa, mkoani Dodoma, ambayo imekuwa taasisi ya kwanza kufungiwa mfumo wa nishati safi ya kupikia kupitia mradi husika. Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mhe. Salome amesema  kuwa mradi unahusisha usimikaji wa mifumo ya gesi ya LPG, ufungaji wa majiko banifu  pamoja na usambazaji wa mkaa mbadala katika taasisi 453. Ameeleza k...