ESAP MINING SERVICES YAIBUKA KINARA MAONESHO YA 9 YA TEKNOLOJIA YA MADINI GEITA, YATWAA TUZO TATU KWA MPIGO
KAMPUNI ya Esap Mining Services Limited imetwaa tuzo tatu katika Maonyesho ya Tisa ya Teknolojia ya Madini yaliyofanyika mkoani Geita, hatua inayotajwa kuwa chachu ya kuongeza ubunifu, matumizi ya teknolojia za kisasa na ufanisi katika shughuli za uchimbaji madini nchini. Katika ushindi huo mkubwa, kampuni hiyo imejinyakulia tuzo za Mthamini Mkuu wa Maonyesho, Kampuni Bora ya Uchorongaji Miamba (Drilling) na mshindi wa pili katika kipengele cha Kampuni Bora ya Uchimbaji Madini. Akizungumza baada ya kupokea tuzo hizo Leo Oktoba 2,2026 wakati wa Maonesho ya Tisa ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea Katika Viwanja vya Dkt.Samia Suluhu Hassan Mkoani Geita, Afisa Utawala na Mawasiliano wa Esap Mining Services Limited,ShabaniMitenenko Sadiki, alisema mafanikio hayo ni hamasa kwa kampuni kuendelea kuboresha huduma zake na kuongeza juhudi katika utekelezaji wa shughuli zake za uchimbaji madini. Alisema kutambuliwa katika vipengele hivyo kunawapa ari ya kuendelea kutumia teknolojia za kisasa n...