Hakuna Taifa Lisilokopa Duniani, Uchumi wa Dunia Umejengeka Kwa Mikopo. Kukopesheka ni Ishara ya Uchumi Imara
_Deni la Tanzania ni himilivu na lina afya kiuchumi ukilinganisha na Mataifa mengi ya Afrika na ulimwenguni._ Na Bwanku M Bwanku. Kwa siku za hivi karibuni kwenye Taifa letu kumezuka mjadala kuhusu nchi kukopa ama kutokukopa. Je kuna haja ya kukopa au kutokukopa au lipi ni lipi? Kama mwananchi nami ningependa kutoa mchango wangu kwa faida ya wote kuhusu huu mjadala. Je ni muhimu kukopa? Hatuwezi kuleta maendeleo yetu wenyewe bila kukopa? Na maeneo mengine kama hayo yanayozunguka kwenye mjadala huu. Kwa Mujibu wa Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) iliyosomwa Wiki iliyopita Alhamisi Machi 27, 2025 Deni la Taifa hadi kufikia muda huu ni Trilioni 97. Deni hili linahusisha mikopo kutoka kwenye Taasisi mbalimbali za ndani na nje ya nchi n.k ambazo fedha zote hizo zikikopwa zinaelekezwa kwenye shughuli mbalimbali za maendeleo ndani ya Taifa. Kwanza, ni muhumu ikafahamika kwamba hakuna nchi yoyote duniani inayofanya shughuli za kiuchumi kuteke...