Na OWM - TAMISEMI,Mtwara Mkoa wa Mtwara umeendelea kupiga hatua katika kuboresha Sekta ya Elimu kufuatia utekelezaji wa Mradi wa Kuimarisha Elimu ya Sekondari (SEQUIP), unaosimamiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, huku ukifadhiliwa na Benki ya Dunia. Akizungumza wakati wa ziara ya ufuatiliaji wa pamoja wa utekelezaji wa mradi huo, Mratibu wa Mradi wa SEQUIP kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI, Bw. Richard Makota, alisema shule za Mkoa wa Mtwara zimeonyesha mafanikio makubwa katika utekelezaji wa mradi. “Matokeo yanaonekana wazi, hasa katika ongezeko la ufaulu wa wanafunzi kwenye masomo ya sayansi na hisabati, pamoja na matumizi ya teknolojia ya kisasa katika ufundishaji,” alisema Bw. Makota. Alisema kupitia SEQUIP, maboresho makubwa yamefanyika ikiwemo ujenzi wa miundombinu mipya ya shule, upatikanaji wa vifaa vya kisasa vya TEHAMA kama mbao janja (smart boards) na kompyuta, pamoja na utoaji wa vifaa vya maabara na kemikal...
Marato tv - Sauti ya Jamii