Skip to main content

Posts

Showing posts from September 17, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

TANZANIA'S SENIOR FEMALE MILITARY DIPLOMAT LEAVES LEGACY IN ZAMBIA

 By Prosper Makene, LUSAKA, Zambia Tanzania's senior female military diplomat, Colonel Bula Bulali, has concluded her four-year tour of duty in Zambia, leaving behind a legacy of strengthened defence ties and groundbreaking cooperation between the two historic allies. Col. Bulali, who has served as Tanzania's Defence Advisor accredited to the Republic of Zambia since 2022, officially bade farewell to Zambia's Ministry of Defence and its Services on Tuesday, 17th September 2026. According to a Press Statement issued by the Ministry of Defence, her tenure was marked by tangible achievements in defence diplomacy, military training, and joint cooperation. Reflecting on her service, Col. Bulali said Zambia and Tanzania had scored significant success in enhancing people-to-people ties and military collaboration. She singled out the signing of a landmark Memorandum of Understanding (MoU) between the Zambia National Service (ZNS) and Tanzania's Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) earl...

KIKWETE AELEZA ALIVYOPAMBANA NA SARATANI YA TEZI DUME

 Na Mwandishi Wetu RAIS mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete amewataka wanaume kujenga utamaduni wa kupima tezi dume mara kwa mara ili waweze kutibiwa mapema wanapogundulika kuwa na dalili za saratani. Alitoa wito huo jana jijini Dar es Salaam alipokuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya mwezi wa uelewa wa saratani ya tezi dume yaliyofanyika katika hospitali ya Kairuki Mikocheni. Rais Kikwete alitembelea mtambo wa kuondoa uvimbe bila upasuaji hospitalini hapo wa High Intensity Focused Ultrasound HIFU ambao unaondoa vimbe mbalimbali mwilini bila upasuaji kwa kutumia mwangwi wa sauti (Ultrasound). Alisema yeye binafsi ni mwathiriwa wa ugonjwa huo kwani baada ya kugundulika mapema mwaka 2014 alichukua hatua ya kwenda kupima vipimo vingine nchini Marekani na ilipothibitika kuwa na ugonjwa huo alikubali kufanyiwa upasuaji na mpaka sasa ni mzima wa afya. Aliwataka wanaume wasiogope kwenda kupima saratani ya tezi dume kwani teknolojia kwa sasa imekwenda mbali zaidi na ugonjwa unaweza ...

MOTSEPE: AFCON 2027 HAIONDOKI TANZANIA, KENYA NA UGANDA

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), Dkt. Patrice Motsepe, amesisitiza kuwa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027 itaendelea kufanyika Tanzania, Kenya na Uganda, akikanusha taarifa na madai yanayodai kuwa mashindano hayo yanaweza kuhamishiwa katika nchi nyingine. Dkt. Motsepe ameyasema hayo leo, Septemba 17, 2026, mara baada ya kuwasili Tanzania kwa ajili ya kukagua maendeleo ya maandalizi ya mashindano hayo, ambayo Tanzania, Kenya na Uganda zimepewa dhamana ya kuwa wenyeji. Amesema amekuwa akisikia taarifa mbalimbali zinazodai kuwa CAF inaweza kuanza kufikiria mpango mbadala wa kuhamishia AFCON 2027 katika nchi nyingine, akisisitiza kuwa hilo halitatokea. “Baadhi ya watu, kutokana na yale ambayo tayari yameripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari barani Afrika na sehemu nyingine duniani, wanasema Rais wa CAF anapaswa kuanza kufikiria mpango B na mpango C na kuiondoa AFCON Tanzania, Kenya na Uganda, hilo halitatokea,” amesema Motsepe. Aidha, Rais huyo wa CAF ...

MWANA DIPLOMASIA MWANAMKE WA JESHI LA TANZANIA AHITIMISHA UTUMISHI WA MIAKA MINNE ZAMBIA KWA MAFANIKIO MAKUBWA

 Na Prosper Makene Mshauri wa Ulinzi wa Tanzania aliyeko nchini Zambia, Kanali Bula Bulali, amehitimisha utumishi wake wa miaka minne uliogusa mafanikio makubwa ya kidiplomasia ya kijeshi. Taarifa rasmi ya Wizara ya Ulinzi ya Zambia iliyotolewa Jumanne Septemba 17, 2026 na Afisa Uhusiano Mkuu Bw. Paul Shalala, imesema Kanali Bulali ameaga rasmi Wizara hiyo na Majesi yake baada ya kuitumikia nafasi hiyo tangu 2022. Katika kipindi cha miaka minne, Kanali Bulali amewezesha kuimarika kwa ushirikiano wa mafunzo ya pamoja, kubadilishana uzoefu wa kijeshi na kuimarisha urafiki kati ya wananchi wa mataifa hayo mawili. Mafanikio makubwa aliyoyaacha ni kusainiwa kwa Hati ya Makubaliano kati ya Jeshi la Kujenga Taifa la Zambia (ZNS) na Jeshi la Kujenga Taifa la Tanzania (JKT), inayolenga uwekezaji katika biashara na kilimo. Katibu Mkuu Kaimu wa Wizara ya Ulinzi Bi. Millicent Mwenda amesema Kanali Bulali atakuwa anakumbukwa kama mjenzi wa madaraja ya urafiki. Uteuzi wa Mshauri mpya wa Ulinzi w...