🔹️ *_Biashara kufanyika kidijitali kupitia Soko la Bidhaa Tanzania-TMX_* 🔹️ *_Waziri Mavunde kuwa Mgeni Rasmi Hafla ya Mnada_* 🔹️ *Wanawake wahamasishwa kuchangamkia fursa za biashara katika mnyororo wa madini_* 📍 *Mirerani- Manyara* Wafanyabiashara wa Madini nchini Tanzania wameelezea matumaini yao makubwa kuhusu hatua ya kurejeshwa kwa Minada ya Madini katika eneo Mirerani, Mkoa wa Manyara na kueleza kuwa kurejea kwa minada hiyo kutasaidia kuleta mchango mkubwa katika kuongeza thamani ya madini, hususan Tanzanite, ambayo ni madini adimu yanayopatikana nchini Tanzania pekee. Hayo yameelezwa kwa nyakati tofauti na baadhi ya wafanyabiashara wakati wakizungumza na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Madini leo Desemba 13, 2024 kuelekea Siku ya Mnada wa Madini ya Vito Mirerani 2024 inayotarajiwa kufanyika Desemba 14, 2024. Wafanyabiashara hao wameitaka Serikali kuendelea kushirikiana na wadau ili kuhakikisha kuwa minada inafanyika mara kwa mara, kwa uwazi, na kwa misingi ya h...
Marato tv - Sauti ya Jamii