Skip to main content

Posts

Showing posts from June 20, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Wazalishaji Umeme Mkoani Njombe Watakiwa Kushirikiana

_📌Washauriwa kuunda umoja wa kusaidiana na kubadilishana uzoefu_ Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Mhe. Balozi Meja Jenerali Mstaafu, Jacob Kingu ametoa wito kwa waendelezaji wa miradi ya Nishati Jadidifu Mkoani Njombe kufanya kazi kwa kushirikiana ili kuongeza tija kwenye shughuli zao na kuwa mfano bora kwa waendelezaji wa miradi katika mikoa mingine. Ametoa wito huo Juni 20, 2025 akiwa katika ziara ya kukagua mradi wa kuzalisha umeme kwa kutumia maporomoko ya maji uliopo katika Kijiji cha Masisiwe, Kata ya Ukwama, Wilaya ya Makete Mkoani Njombe unaomilikiwa na Dayosisi ya Kusini Kati ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri  Tanzania (KKKT)kupitia Kituo cha Udiakonia Tandala. "Kwa wingi wa rasilimali ya maji iliyopo Mkoani hapa ni dhahiri uwezo wa kuzalisha zaidi ya megawati 50 ndani ya Mkoa huu pekee upo, ni suala la nyinyi waendelezaji wa miradi kuunganisha nguvu kwa kufanya kazi kwa kushirikiana na kusaidiana," alisisitiza Mhe. Balozi Kingu. Hata hivyo alipongeza ...

Fursa za Madini Zipo Kidijitali

_Watanzania Watakiwa Kuzichangamkia_ 📍 *DODOMA, Juni 21, 2025* Sekta ya madini nchini Tanzania inaendelea kushamiri kwa kasi, ikifungua milango ya ajira, uwekezaji na maendeleo kwa wananchi na Taifa kwa ujumla. Serikali kupitia Tume ya Madini imeendelea kuweka mazingira wezeshi kwa kuhakikisha usimamizi madhubuti, uwazi, na ushirikishwaji wa wadau wote katika mnyororo mzima wa shughuli za madini. Haya yamekuwa ni matokeo ya maboresho ya sera, sheria, pamoja na mifumo ya kidijitali inayotumika katika kusimamia sekta hiyo. Akizungumza leo Juni 21, 2025 katika Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Chinangali jijini Dodoma, Afisa Ukaguzi Migodi kutoka Kurugenzi ya Ukaguzi wa Migodi na Mazingira wa Tume ya Madini, Bw. Ashen Mwambage, amesema kuwa Watanzania wengi wanapaswa kuchangamkia fursa mbalimbali zinazotolewa kupitia Sekta ya Madini. Ameeleza kuwa katika mikoa mbalimbali kama Geita, Shinyanga, Mara na Mbeya, wananchi wamehamasika kushiriki katika sh...

Balozi Nchimbi Msibani Kwa Ndugu Malima

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi akitoa pole kwa familia ya marehemu Mobutu Malima, nyumbani kwake Kishiri, Nyamagana, mkoani Mwanza, tarehe 20 Juni 2025.  Ndugu Malima, ambaye alikuwa Afisa Mwandamizi, Ofisi ya Naibu Katibu Mkuu (Bara), Makao Makuu ya CCM, Dodoma alifariki tarehe 15 Juni na anatarajiwa kuzikwa Jumapili, tarehe 22 Juni 2025, eneo la Ihayabuyaga, Magu, mkoani Mwanza.

Vyama vya UDA na CCM Vyakutana kujifunza

  CHAMA tawala nchini Tanzania, Chama cha Mapinduzi (CCM), kimeanzisha mazungumzo na United Democratic Alliance (UDA) kwa lengo la kuimarisha uhusiano kati yake na chama hicho tawala nchini Kenya. Hatua hiyo inajiri mwezi mmoja baada ya Wakenya na Watanzania kurushiana cheche za maneno kufuatia kisa ambapo wanasiasa na wanaharakati kutoka Kenya walifurushwa kutoka Tanzania huku Boniface Mwangi akizuiwa na kudai kuteswa.  Miongoni mwa waliofurushwa ni kiongozi wa chama cha People’s Liberation Party (PLP) Martha Karua na Jaji Mkuu mstaafu Willy Mutunga. Lakini mnamo Jumatano, Juni 18, 2025, Katibu Mkuu wa CCM,Dokta Emmanuel Nchimbi alifanya mazungumzo na mwenzake wa UDA, Hassan Omar Hassan jijini Nairobi. Kwenye taarifa iliyotolewa baada ya mkutano huo, viongozi hao walisema kuwa mazungumzo yao yalikita katika njia za kuimarisha ushirikiano na mahusiano kati yao. “Mazungumzo yalikita katika mbinu za kuimarisha mahusiano kati ya vyama vya CCM na UDA kwa manufaa ya watu wa nchi hi...

Mbunge Ashtakiwa Kwa Kuweka Picha yake kwenye Miradi ya Maendeleo

 WAKILI mmoja jijini Nairobi amemshtaki Mbunge wa Kajiado Kaskazini, Onesmus Ngogoyo, akimlaumu kwa kukiuka sheria kwa kuweka jina na picha yake kwenye mabango ya miradi inayofadhiliwa na serikali kupitia Hazina ya Serikali ya Kitaifa ya Maendeleo ya Maeneobunge (NG-CDF). Wakili huyo, Shadrack Wambui, anasema kuwa hatua hiyo ni kinyume na maadili ya uongozi na uadilifu, na anamtaka mbunge huyo aondoe mabango yote yenye jina lake, picha, na kauli mbiu za kisiasa kwenye shule, barabara, na miundombinu mingine ya umma katika eneo lake. Katika kesi hiyo iliyowasilishwa katika Mahakama Kuu mbele ya Jaji Christine Meoli, Bw Wambui anasema kuwa mbunge huyo amekuwa akijinufaisha kisiasa kwa kutumia miradi ya umma, baadhi ikiwa ilitekelezwa kabla ya kuchaguliwa kwake. “Mbunge huyo ameweka jina na picha yake kwenye karibu kila mradi wa maendeleo wa serikali ndani ya eneo lake, na katika hali nyingi, picha na jina lake vinachukua nafasi kubwa kupita kiasi kwenye mabango, hivyo kufunika taarif...

Maftaha Nachuma Ajiunga Act Wazalendo

Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo pa Mtwara Mjini na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha CUF Ndugu Maftaha Nachuma amekihama Chama hicho na kujiunga na Chama cha ACT Wazalendo. Maftaha amekabidhiwa kadi ya ACT Wazalendo na Makamu Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Ndugu Isihaka Mchinjita kwenye Kongamano la kumpokea lililofanyika katika Ukumbi wa Kanisa la Pentekoste Mtwara leo tarehe 19 Juni 2025.

Rais Dkt. Samia Chifu Hangaya Awa Mtemi wa Sungusungu Mikoa Mitano

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amepewa heshima na hadhi ya kuwa Mtemi wa Sungusungu, jeshi la jadi, kwa mikoa mitano ya Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Geita na Tabora. Mhe. Rais Dkt. Samia ambaye pia ni Mkuu wa Machifu nchini, akijulikana kwa jina la Chifu Hangaya, ametangazwa rasmi kuwa Mtemi wa Sungusungu kupitia risala ya utii wao kwake, wakati wa hafla ya kumpongeza kwa utekelezaji wa miradi ya kimkakati, iliyofanyika katika Uwanja wa CCM Kirumba, mkoani Mwanza, leo Ijumaa, tarehe 20 Juni 2025. “Mheshimiwa Rais (Dkt. Samia) kwa kuwa wewe ni Amiri Jeshi Mkuu, na sisi ni walinzi wako, watiifu kabisa, tunaomba upokee hadhi ya kuwa Mtemi wa Sungusungu. Nakukabidhi vifaa vya ulinzi wa jadi, ambavyo vitatolewa maelezo. Aidha, tunaomba tukutambulishe watemi na makamanda wa Sungusungu, ambao tumekuwa tukishirikiana katika mikoa hii mitano,” alisema Ndugu Richard Bundala, kiongozi wa Sungusungu hao. Mtemi wa Sung...

Mbunge Prof.Muhongo Aelezea Namna Ilani Ilivyotekelezwa Kwa Ufanisi Mkubwa

Na Shomari Binda-Musoma MBUNGE wa Jimbo la Musoma Vijijini Profesa Sospeter Muhongo ameeleza sababu za kumchagua Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwenye uchaguzi mkuu wa 2025. Sababu za kumchagua amezieleza ni pamoja na kutoa fedha nyingi zilizoweza kutekeleza miradi ya elimu,afya,maji,miundombinu na masuala ya uwezeshaji wananchi kiuchumi. Kauli hiyo ameisema leo juni 20,2025 Kijijini Murangi wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020,2025 kwenye Mkutano Mkuu wa Wilaya ya Musoma Vijijini. Amesema kuanzia kipaumbele cha kwanza cha elimu kati ya vipengele 5 serikali ya awamu ya 6 chini ya Dkt.Samia Suluhu Hassan imetoa fedha nyingi ambazo zimetekeleza miradi ya elimu kuanzia ujenzi wa shule mpya na kuongeza madarasa. Profesa Muhongo amesema wakati anashika nafasi ya ubunge 2020 Jimbo la Musoma Vijijini kulikuwa na shule za sekondari 14 na sasa zipo shule 30 za serikali zikiwemo 2 za binafsi. Amesema licha ya uwepo wa shule hizo 18 zinajengwa na ifik...

Mbunge Sagini amegawa Kompyuta na Vitabu Kwa Shule za Msingi na Sekondari

  Mwenyekiti wa Shirika lisilo la Kiserikali la Zamaless Development Foundation (ZDF) ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Butiama na Naibu Waziri Katiba na Sheria Mhe. Jumanne Sagini* amegawa jumla ya vitabu 14094, Kompyuta  9 na Printa 1 kwa Shule mpya na zenye ufaulu hafifu Msingi na Sekondari. Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo *Mhe. Sagini* amesema kuwa vitakwenda kuchochea ongezeko la ufaulu kwa wanafunzi kitaaluma na kupunguza adha kwa walimu ambao walikuwa wanaenda kuandaa mitihani nje ya shule jambo lilokuwa linasababisha uvujaji wa mitihani na ucheleweshaji. Kwa upande wake *Afisa Elimu Vifaa na Takwimu Wilaya ya Butiama Mwl. Baraka Alfred* amesema kuwa vitabu na vifaa vilivyotolewa na *Mbunge Sagini* vitasimamiwa kuhakikisha vinafanya kazi kama ilivyoelekezwa kwa walimu wakuu wa kila shule iliyopokea ili kufanikisha dhamira ya kuongeza ufaulu kwenye shule ambazo ufaulu wake upo chini na zile shule changa. Naye *Mkurugenzi wa Shirika lisilo la kiserikali la Zamaless...