WAZIRI wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi,Ajira na Mahusiono Deus Sangu amesema wakati sekta ya madini ikiendelea kung'aa kwa kuchangia takriban asilimia 10.1 ya Pato la Taifa na kuajiri maelfu ya Watanzania, kuna shujaa mmoja ambaye ni Mfuko wa Fidia Kwa wafanyakazi(WCF) anahakikisha jasho la mfanyakazi huyo haliendi bure anapopatwa na janga. Akizungumza kwenye Banda la Mfuko huo Leo Septemba 24,2024 Katika maonesho ya Tisa ya Kitaifa ya Teklojia ya Madini yanayofanyika Katika Viwanja vya Dkt.Samia Suluhu Hassan yanayofanyika Mkoa wa Geita ameeleza kwamba ndani ya miaka 10 ya WCF imejijenga kuwa mkombozi wa kweli kwa wafanyakazi wa migodini na sekta nyingine zote. Aidha ameeleza kwamba Mfuko huu unatoa fidia kwa mfanyakazi anapopata ajali kazini, anapougua ugonjwa unaotokana na kazi, au kwa wategemezi wake mwenza na watoto pindi mfanyakazi anapofariki dunia akiwa kazini. Aidha Katika kipindi Cha rais wa awamu ya sita mufuko ulikuwa na Bilioni 770 na mpaka Sasa kufikia...
Marato tv - Sauti ya Jamii