Skip to main content

Posts

Showing posts from February 11, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Dkt. Mwigulu Amwakilisha Rais Dkt. Samia Maadhimisho ya Miaka 30 ya Ocean Road

Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba leo Februari 12, 2026 amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan katika maadhimisho ya miaka 30 ya  Taasisi ya Saratani Ocean Road. Maadhimisho yanayofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam yanatoa fursa kwa Taasisi hiyo pamoja na wadau wengine kutafakari kwa pamoja safari ya mapambano dhidi ya saratani kwa kuangalia walipotoka, walipo na wapi  wanaelekea.

Nyamagana Gender Desk Hosts Delegation From Norway

*From: Mwanza Police Information Desk* The Gender and Children Desk of Nyamagana District, Mwanza Region, on 10 February 2026 received a delegation from Norway in collaboration with their local host organization, KIVULINI, with the aim of learning and observing the implementation of various projects carried out by the organization. The delegation comprised members of the Executive Committee from the organizations FO Innlandet and FOKUS, together with a representative of the Royal Norwegian Embassy in Tanzania, Ms. Annette Pettersen. These organizations are among the main donors supporting projects aimed at eliminating gender-based violence implemented by KIVULINI. Speaking during the visit, the Head of the Delegation, Ole Henrik Krakenes from FO, stated that they were pleased and satisfied with the level of cooperation between the Tanzania Police Force in Mwanza Region and KIVULINI, an organization engaged in preventing violence against women and children. After visiting the Nyamagana ...

Katambi Ateta Mambo Mazito na Polisi Zanzibar

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Patrobas Katambi amelipongeza Jeshi la Polisi Visiwani Zanzibar kwa kupambana na uhalifu hali iliyopelekea kupungua kwa matukio 746 ambapo matukio 3091 yaliripotiwa mwaka 2024 huku mwaka 2025 yakiripotiwa matukio 2345. Akizungumza na Uongozi wa Juu wa Jeshi la Polisi Visiwani humo Waziri Katambi alizungumzia pia kulindwa kwa watalii akikumbushia jitihada zilizofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.Samia Suluhu Hassan na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Dkt.Hussein Ali Mwinyi katika kuutangaza na kuukuza utalii. Masuala mengine aliyozungumzia ni Mauaji yanayotokana na watu kujichukulia Sheria mkononi,Makosa ya Barabarani yanayosababishwa na watumiaji wa vyombo vya moto kutofuata sheria za Usalama Barabarani.

Waziri Kikwete Awashukuru Owm-kazi,Ajira na Mahusiano Kwa Kumpatia Nishani

‎‎ ‎Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete (Mb) amewashukuru OWM-Kazi, Ajira na Mahusiano kwa kumtambua kama aliyechangia mabadiliko katika sera ya Kinga ya Jamii. ‎Mh.Kikwete amesema kuwa nishani hiyo ataipeleke kwa Mh. Samia Suluhu Hassan, Rais wa JMT kwa kumpa nafasi ya kutumika katika nchi hii chini ya Uongozi wake. ‎Amemshukuru Mh.Rais toka kwenye sakafu ya Moyo wake kwa kumteua na kumuamini siku zote. Ameendelea kuahidi kuwa atatumika kwa manufaa na ujenzi wa nchi. ‎#KaziNaUtu #TunasongaMbele ‎

Kamati ya Bunge Yaipongeza Tarura Kwa Kuimarisha Barabara, Kuokoa Maisha ya Wananchi

Na OWM - TAMISEMI, Dodoma Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu Mhe. Selemani Kakoso ameipongeza Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) kwa kujenga miundombinu ya barabara iliyookoa maisha ya wananchi katika maeneo mbalimbali ambayo awali kuharibika kwa miundombinu hiyo kulisababisha vifo vya wananchi. Mhe. Kakoso amesema hayo leo Februari 11, 2026 wakati wa kikao cha mafunzo kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, yaliyohusu uboreshaji wa Mtandao wa Barabara za Wilaya, Mikakati, Changamoto na Fursa kwa Maendeleo ya Taifa yaliyofanyika katika Ukumbi wa Anne Makinda Bungeni Jijini Dodoma. Mhe. Kakoso amesema kuwa, katika jimbo lake kuna eneo ambalo TARURA imejenga daraja ambapo kila mwaka wananchi walikuwa wakipoteza maisha kutokana na kukosekana kwa daraja la uhakika, lakini tangu daraja hilo lijengwe hakuna taarifa za vifo tena. “Katika Jimbo langu kuna sehemu amba...

Siku 100 Za Raia Samia Ikulu Zilivyoleta Neema Kwa Vijana

Na Mwandishi Wetu WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais, Maendeleo ya Vijana, Joel Nanauka, ametaja mafanikio makubwa ambayo Rais Samia Suluhu Hassan ameyafanya ndani ya siku 100 madarakani ikiwemo kuwawezesha vijana. Akizungumzia siku 100 za Rais Samia IKULU, Waziri Nanauka, Waziri Nanauka alisema Rais Samia amefanikiwa kutekeleza ahadi zake hasa kusaidia vijana wa makundi mbalimbali ambao wengi wamepata mafunzo ya ujasiriamali na kupata mikopo. Akizungumzia siku 100 za Rais Samia IKULU, Waziri Nanauka,  alisema kwa utekelezaji wa ahadi zake ndani ya siku 100 IKULU, Rais Samia amevunja rekodi ya watangulizi wake. “Siku 100 za Rais Samia IKULU zimekuwa na mafanikio makubwa sana na pengine naweza kusema ni kati ya siku 100 zenye matokeo ya haraka kuliko na hii inatokana na dhamira yake,, aliahidi bilioni 200 kwa wafanyabishara wadogo, wakati na wa kampuni changa na amezitoa,” alisema Waziri Nanauka alisema kati ya ahadi 13 alizotoa Rais Samia kuwa atazitekeleza ndani ya siku 100, ahadi sita ...

Waziri Mkenda Asisitiza Uwekezaji wa Wanawake na Wasichana Katika Masomo ya Sayansi

 DODOMA. WAZIRI wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda amesema Serikali itaendelea kuwekeza katika Sayansi nchini ili kuendana na hitaji la Soko la Sayansi kwakuwa na Wanasayansi bora na wakutosha katika Sekta zote kutokana na kukua kwa teknolojia Ulimwenguni. Profesa Mkenda ameyaeleza hayo leo Februari11 Jijini Dodoma wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake na Wasichana katika sayansi Mwaka 2026. Amesema takwimu zinaonesha wanawake wanasayansi duniani ni takribani asilimia 36 tu, hali inayoashiria kuwa bado kuna haja kubwa ya kuwawezesha wanawake kushiriki kikamilifu katika sekta ya sayansi. ‎“Nchini Tanzania wanawake ni wengi kuliko wanaume. Kimsingi, tungewekeza vya kutosha katika kuwaendeleza wasichana kwenye masomo ya sayansi, tungekuwa na idadi kubwa zaidi ya wanasayansi wanawake,” amesema Waziri Mkenda. Aidha,Prof. Mkenda amewataka wanafunzi, hususan wasichana, kujitokeza kwa wingi kusoma masomo ya sayansi ili kuongeza idadi ya wataalamu na kuhar...