📍 Mradi wagharimu zaidi ya TZS Milioni 252 Na Beatus Maganja, Rufiji, Pwani. Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) imekabidhi rasmi bweni jipya la wasichana katika Shule ya Sekondari Mchengerwa iliyopo Kata ya Ngarambe wilayani Rufiji mkoani Pwani ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuboresha mazingira ya elimu, hasa kwa mtoto wa kike. Bweni hilo ambalo ujenzi wake umegharimu zaidi ya shilingi milioni 252, limejengwa kwa ushirikiano kati ya TAWA na Shirika la Uhifadhi wa Wanyamapori (Frankfurt Zoological Society – FZS) chini ya ufadhili wa Serikali ya Ujerumani kupitia Benki ya Maendeleo ya watu wa Ujerumani (KfW), limekabidhiwa likiwa na jumla ya vitanda 40 aina ya "double decker", magodoro 80, huduma ya maji safi, pamoja na umeme unaohudumia wanafunzi wapatao 80. Mbali na bweni hilo, TAWA pia imekabidhi darasa moja la kisasa likiwa na meza 45 na viti 45 vya wanafunzi pamoja na viti vinne na meza mbili za walimu katika shule ya Sekond...
Marato tv - Sauti ya Jamii