Naibu wa rais nchini Kenya Rigathi Gachagua amesema kwamba atawasili bungeni hapo kesho ili kujitetea. Naibu huyo ambaye anakabiliwa na mashtaka ya kumuondoa madarakani amesema kuwa atawasili mbele ya bunge pamoja na kundi lake la mawakili mwendo wa saa kumi na moja ili kujitetea. Akizungumza na waandishi habari nyumbani kwake huko Karen Jijini Nairobi, Kiongozi huyo amesema kwamba kabla ya yeye kuwasilisha hoja yake ya kujitetea atahitaji bunge kusikiliza maoni ya Wakenya waliomchagua. Kiongozi huyo alisema anatumai wabunge watamruhusu kujibu tuhuma zote bila kuingiliwa. Gachagua, amesema aliita kikao hicho na waandishi wa habari kutoa utetezi wake kwa Wakenya waliomchagua kabla ya kuwasili mbele ya wawakilishi hao. "Nafikiri ni haki wakati wabunge wataamua kwamba wanataka kumwondoa Naibu Rais afisini, watu waliomchagua Rigathi Gachagua kuwa Naibu Rais wasikie upande wake," akasema. Hoja ya kuondolewa mashtaka iliwasilishwa Septemba 26 na Mbunge wa Kibwezi Magharibi Mwengi M...
Marato tv - Sauti ya Jamii