Skip to main content

Posts

Showing posts from January 16, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Vijiji Vinane Misungwi Kunufaika na Mpango wa Matumizi bora ya Ardhi

 Wananchi waupokea kwa furaha Mpango wa kitaifa wa matumizi bora ya Ardhi unaotekelezwa katika Vijiji 8 vya Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Mkoani Mwanza . Serikali kupitia Wizara ya Ardhi, na Maendeleo ya Makazi pamoja na Timu ya Wawezeshaji wa masuala ya Ardhi kutoka Tume ya Taifa ya Mipango na Matumizi bora ya Ardhi mapema wiki hii imetambulisha mpango huo wa matumzi bora Ardhi katika Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi utakaotekelezwa katika Vijiji 8 kati ya Vijiji 115 vya Wilaya hiyo kwa kutenga maeneo rasmi kisheria kwa matumizi ya huduma za kijamii sambamba na kutoa hati za kimila. Akizungumza katika Mikutano ya Hadhara na Viongozi wa Serikali za Vijiji katika Kijiji cha Gulumungu na Lukanga Afisa wa Tume ya Mipango ya matumizi ya Ardhi Bw. Bwahama Bagenyi ameeleza kwamba Serikali inaendelea kuboresha na kuweka mipango ya upimaji wa maeneo ya Vijiji kwa ushirikiano na Wananchi pamoja na Viongozi, waweze kutenga maeneo yao kwa ajili makazi, Kilimo, malisho, Makaburi, taasisi ...

Meja Jenerali Gaguti Afunga rasmi zoezi la Medani Msata

Mkuu wa Utumishi wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania Meja Jenerali Marco Gaguti amefunga rasmi zoezi la Medani la EX- MALIZA lililofanywa na Kuruti wa Kundi la 44/25 katika eneo la Msata tarehe 16 Januari 2026.  Akizungumza baada ya kukamilika kwa zoezi hilo, Meja Jenerali Gaguti amewataka Kuruti hao wanaotarajia kuhitimu mafunzo ya awali ya kijeshi hivi karibuni kuwa waadilifu, kujituma na kuwa watiifu kwa nchi yao. Kuruti walioshiriki zoezi, wametakiwa kuzingatia mafunzo ya nadharia na vitendo kama shambulio la kunuia, shambulio la kushtukiza na somo la doria huku akionyesha wazi kuwa zoezi limefanikiwa.  Dhamira ya Jeshi la ulinzi la Wananchi wa Tanzania ni kuona kuruti wote wanahitimu na kwenda katika maeneo mbalimbali watakayopangiwa kushiriki  kulilinda taifa. Meja Jenerali Gaguti aliongeza kuwa Mafunzo na Mazoezi mbalimbali ya medani ndio msingi wa JWTZ kwani Jeshi imara linatokana na uwepo wa mazoezi ya medani. Kuruti wanaotarajiwa kuhitimu kozi ya mafunzo ...

Kanali Mtambi Awapa Somo Vijana Tarime

  Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Kanali Evans Alfred Mtambi leo tarehe 16 Januari, 2026 amekuwa mgeni rasmi katika kikao cha vijana wa Wilaya ya Tarime kilichoandaliwa na Chifu wa Wakurya Koo ya Wakenye Mhe. Christopher Gachuma ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (MNEC) kutoka Mkoa wa Mara. Akizungumza katika kikao hicho, Kanali Mtambi amewataka vijana wa Wilaya ya Tarime kubadilika kifikra na matendo ili kuweza kufaidi fursa mbalimbali zilizopo katika Wilaya ya Tarime na Mkoa wa Mara kwa jumla.  Mhe. Mtambi amesema Mji wa Tarime na Mkoa wa Mara unafursa nyingi na kusipokuwa na amani na utulivu fursa hizo zitawafaidisha watu waliopo katika Mikoa mingine.  Mhe. Mtambi pia amewasikiliza vijana na kupokea kero, changamoto na mapendekezo yao kuhusiana na utatuzi wa changamoto zinazowakabili.  Kikao hicho kimehudhuriwa pia na Chifu wa Watimbaru Ndugu Peter Zakaria na viongozi wengine katika jamii na kimefanyika katika ukumbi wa Hoteli ya CMG, Tarime.

Dkt. Mwigulu Aongoza Kikao Cha Kujadili Changamoto za Kibiashara Kati ya Tanzania na Zambia

Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba leo Januari 16, 2026 ameongoza kikao cha kimkakati na Mawaziri, Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu wa kisekta, Ofisini kwake, Mlimwa Jijini Dodoma. Katika kikao hicho, viongozi hao wamejadili kuhusu changamoto za biashara kati ya Tanzania na Zambia  Wizara zilizohudhuria kikao hicho ni pamoja na Ofisi ya Waziri Mkuu ( Sera Bunge na Uratibu), Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Wizara ya Fedha, Wizara ya Nishati, Wizara ya Uchukuzi, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,  Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Pia, kikao hicho kilihudhuriwa na Wakuu wa Mikoa ya Mbeya, Songwe na Rukwa.

Makamu wa Rais Azindua Jengo La Viongozi Mashuhuri Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amesema Serikali imejizatiti kuhakikisha Sekta ya Uchukuzi inaimarika ili kuliweka Taifa kwenye nafasi nzuri ya ushindani wa kibiashara, kuongeza mapato ya fedha za kigeni na kukuza mchango wa sekta hiyo katika pato la Taifa. Makamu wa Rais amesema hayo wakati wa uzinduzi wa Jengo la Viongozi Mashuhuri katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam. Amesema pamoja na ujenzi wa jengo hilo, Serikali ya Awamu ya Sita imejipanga kikamilifu kuendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya kisekta kama ilivyoainishwa katika Dira ya Maendeleo ya Taifa ya Mwaka 2050, Mpango wa Miaka Mitano wa Maendeleo ya Taifa na Ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (2025). Makamu wa Rais amesisitiza kwamba, Serikali itaendelea kuboresha miundombinu na huduma mbalimbali katika Viwanja vya Ndege, huduma za usafiri wa barabara, usafiri majini na usafiri kwa njia ya reli. Halikadhalika amesema, Serikali it...