Skip to main content

Posts

Showing posts from July 16, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

KATIBU MKUU CCM AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA NORWAY NCHINI TANZANIA

Katibu Mkuu Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Dkt. Asha-Rose Migiro, amefanya mazungumzo na Balozi wa Norway nchini Tanzania, Mhe. Tone Tinnes, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, Dar es Salaam. Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika Julai 15,2026, viongozi hao walijadiliana kuhusu uhusiano na ushirikiano mzuri uliopo kati ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na Ufalme wa Norway, pamoja na maeneo ya ushirikiano yanayohusu maendeleo ya kidemokrasia, utawala bora, ujenzi wa taasisi na maendeleo endelevu.

JKCI NA ALMC WAIMARISHA HUDUMA ZA MOYO ARUSHA KUPITIA TEKNOLOJIA ZA KISASA

Na Mwandishi Wetu, Arusha Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), imezindua mfumo wa kidijitali wa usajili wa wagonjwa na teknolojia mpya ya kisasa ya Dozee ya kufuatilia hali ya mgonjwa hata kiwa nyumbani. Uzinduzi huo ulifanyika jana jijini Arushwa ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini,Paul Makonda. Alisema uwekezaji huo unaifanya Tanzania kuwa miongoni mwa nchi zinazoendelea kupiga hatua barani Afrika katika matumizi ya ubunifu wa kidijitali kuboresha huduma za matibabu na kutekeleza malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 Makonda alisema matumizi ya teknolojia katika usajili wa wagonjwa, utunzaji wa kumbukumbu za kitabibu na ufuatiliaji wa wagonjwa baada ya matibabu ni sehemu ya maono ya Serikali ya kujenga taifa lenye uchumi unaotegemea maarifa, sayansi na teknolojia. Katika kambi hiyo, Taasisi ya Moyo Mfumo wa teknolojia unaojulikana kitaalamu kama Dozee, una uwezo wa kufuatilia hali ya mgonjwa kwa wa...

MAKAMU WA RAIS DKT. NCHIMBI ASHIRIKI MKUTANO WA NNE WA KUENZI NA KUENDELEZA URITHI WA HAYATI BENJAMIN MKAPA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amesema unapotafakariwa mustakabali wa utoaji huduma za afya nchini, hakuna budi kutoa kipaumbele kwa vijana kama Hayati Benjamini Mkapa alivyoamini, ikiwemo kubuni programu zitakazowaandaa vijana kukabiliana na changamoto za siku zijazo kwa kujiamini. Makamu wa Rais amesema hayo, wakati alipomwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Nne wa kuenzi na kuendeleza Urithi wa Hayati Benjamin William Mkapa na Maadhimisho ya Miaka 20 ya Taasisi ya Benjamin Mkapa (BMF), uliyofanyika katika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam. Amesema Vijana ndiyo viongozi wa sekta ya afya wa kesho, watumishi wa afya na watafiti wajao. Makamu wa Rais amesema Maisha na uongozi wa Hayati Benjamin Mkapa unatoa mafunzo mengi hususani katika usimamizi na uendelezaji wa sekta ya afya nchini kwa kuwa alitambua nafasi ya afya bor...

KATIBU MKUU CCM AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA NORWAY NCHINI TANZANIA

 Katibu Mkuu Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Dkt. Asha-Rose Migiro, amefanya mazungumzo na Balozi wa Norway nchini Tanzania, Mhe. Tone Tinnes, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, Dar es Salaam. Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika Julai 15,2026, viongozi hao walijadiliana kuhusu uhusiano na ushirikiano mzuri uliopo kati ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na Ufalme wa Norway, pamoja na maeneo ya ushirikiano yanayohusu maendeleo ya kidemokrasia, utawala bora, ujenzi wa taasisi na maendeleo endelevu.

RAIS SAMIA AONGOZA KIKAO CHA BARAZA LA MAWAZIRI IKULU CHAMWINO

 RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameongoza Kikao cha Baraza la Mawaziri kilichofanyika Ikulu Chamwino, mkoani Dodoma, tarehe 16 Julai 2026. Kikao hicho kimewakutanisha Mawaziri wa Serikali kwa ajili ya kujadili na kufanya maamuzi kuhusu masuala mbalimbali ya kitaifa yanayolenga kuimarisha utoaji wa huduma kwa wananchi na kuendeleza utekelezaji wa vipaumbele vya maendeleo nchini.

WAZIRI MAVUNDE KUWA MGENI RASMI JUKWAA LA LCCF 2026 MWANZA

📍MWANZA  Waziri wa Madini, Mheshimiwa Anthony Mavunde, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Jukwaa la Tano la Utekelezaji wa Ushirikishwaji wa Watanzania katika Sekta ya Madini (Local Content Compliance Forum – LCCF 2026), litakalofanyika kuanzia Julai 22 hadi 24, 2026, katika Ukumbi wa Malaika Beach Resort jijini Mwanza. Jukwaa hilo, linaloandaliwa na Tume ya Madini, linatarajiwa kuwakutanisha wadau mbalimbali wa Sekta ya Madini, wakiwemo makampuni ya uchimbaji wa madini, watoa huduma migodini, wafanyabiashara wa madini, taasisi za Serikali, wawekezaji pamoja na wananchi wenye shauku ya kushiriki katika maendeleo ya sekta hiyo. Kwa mujibu wa Tume ya Madini, Jukwaa litatoa fursa kwa washiriki kujifunza kupitia mawasilisho ya kitaalam, midahalo, mafunzo na maonesho yatakayolenga kuimarisha ushiriki wa Watanzania katika shughuli za uchumi zinazotokana na Sekta ya Madini. Aidha, jukwaa hilo litakuwa sehemu muhimu ya kujenga ushirikiano kati ya wadau, kubadilishana uzoefu, kujadili fu...

JAB YAPOKEA OMBI LA KUTOA MAFUNZO KWA BLOGGERS ZAIDI YA 200

 Na Mwandishi Wetu, JAB Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imepokea ombi kutoka Mtandao wa Mabloga Tanzania (TBN) la kutoa mafunzo kwa wanachama wake zaidi ya 200 kuhusu Sheria ya Huduma za Habari, Maadili ya Uandishi wa Habari na umuhimu wa kupata ithibati. Ombi hilo limetolewa leo, tarehe 16 Julai, 2026, na Mwenyekiti wa Mtandao wa Mabloga Tanzania, Bw. Beda Msimbe, alipokutana na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa JAB, Wakili Patrick Kipangula, katika mazungumzo yaliyofanyika katika ofisi za Bodi jijini Dar es Salaam. Akizungumza baada ya mazungumzo hayo, Wakili Kipangula amesema Bodi imepokea ombi hilo na iko tayari kushirikiana na Mtandao huo katika kuwawezesha bloga kupata uelewa wa kina kuhusu Sheria ya Huduma za Habari, maadili ya taaluma pamoja na umuhimu wa kupata ithibati. Amesema mafunzo hayo yataanza kutolewa kwa bloggers wenye ithibati ili kuimarisha weledi na uelewa wao wa majukumu ya kitaaluma, kabla ya kuendelea kuwafikia wale ambao bado hawajapata ithibati. "Wal...