WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amewahakikishia Watanzania fedha zilizokusanywa katika mbio za hisani za Bunge zitakwenda kutumika kama ilivyokusudiwa. Ameyasema hayo leo (Jumamosi, Aprili 12, 2025) katika mbio za hisani za Bunge zilizolenga kuchangisha fedha za ujenzi wa Shule ya Sekondari Bunge Wavulana. Ujenzi wa shule hiyo shule hiyo itakayokuwa na uwezo wa kusajili wanafunzi wasiopungua 300 hadi 350 kwa mwaka utagharimu zaidi ya shilingi bilioni tatu. Shule hiyo ya kidato cha tano na sita itajengwa katika eneo la Kikombo, Jijini Dodoma karibu kidogo na shule ya wasichana iliyojengwa na wabunge wanawake 2020. “Ninawapongeza sana Wabunge wenzangu kwa kuweka alama na kugusa maisha ya Watanzania na watoto wetu wa kiume watakaopata fursa ya kusoma katika shule hiyo.” Amesema ujenzi wa shule hiyo ni mpango wa Bunge wa kuunga mkono juhudi za Mheshimiwa Rais Dkt. Samia suluhu Hassan katika kukuza na kuendeleza sekta ya elimu. Shule hiyo ya bweni itakuwa maabara nne za biolojia, kemia, fiziki...
Marato tv - Sauti ya Jamii