*📌 Amwakilisha Rais Samia hafla ya kutabaruku kanisa SDA- Magomeni* *📌 Ataka watu kutengenezeana furaha badala ya kuumizana* *📌 Ahimiza Mshikamano wa Taifa ili kuleta maendeleo* *Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati* Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewataka Watanzania kujenga misingi ya kusaidiana kuheshimiana na kuvumiliana ili kufanikisha malengo wanayojiwekea kimaendeleo. Dkt. Biteko ametoa rai hiyo leo Desemba 15, 2024 Jijini Dar es Salaam alipomwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa mgeni maalum katika Hafla ya Kutabaruku Jengo la Kanisa la Waasventista Wasabato, Magomeni. Amewahimiza waumini na Watanzania kwa ujumla kuboresha huduma za jamii na kuwekeza katika mipango itakayowezesha kukidhi mahitaji na kupata Taifa endelevu. “ Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan siku zote amekuwa akisisitiza maridhiano, uhimilivu, mabadiliko na kuimarisha amani yetu il...
Marato tv - Sauti ya Jamii