Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda amefunga rasmi Mafunzo ya Askari wapya katika hafla iliyofanyika katika viwanja vya Shule ya Mafunzo ya Awali ya Kijeshi (RTS) Kihangaiko Msata Mkoani Pwani leo tarehe 31 Januari 2025. Jenerali Mkunda amewataka askari wapya kukiishi na kuzingatia kiapo cha utii wakati wote watakapokuwa wakitekeleza majukumu yao sehemu mbalimbali watakayopangiwa, huku akisisitiza kuchukuliwa hatua kwa askari watakaokwenda kinyume na kiapo chao. Askari wapya wameaswa kutotenda mambo ambayo ni kinyume na taratibu za kijeshi ikiwemo kutojihusisha na siasa, matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii, matumizi ya madawa ya kulevya, michezo ya kamari na kuepuka madeni yasiyo na tija. Mkuu wa Majeshi amewataka Askari hao kutunza Afya zao na kuzingatia lishe bora wakati wote wanapotekeleza majukumu yao. Aidha, wasijihusisha na uhalifu wa aina yoyote kwani watakuwa wamekwenda kinyume na sheria na taratibu za kijeshi hivyo watachukuliwa hatua za kinidhamu. Je...
Marato tv - Sauti ya Jamii