Skip to main content

Posts

Showing posts from February 19, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Dkt. Mwigulu Akagua Ujenzi wa Barabara ya Spencon-Mabogini-kahe-Chekereni.

_Aagiza ijengwe na TANROADS ili iwe bypass ya kupunguza msongamano mjini._ Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba leo Februari 20, 2026 amekagua ujenzi wa barabara ya Spencon-Mabogini-Kahe-Chekereni yenye urefu wa kilomita 31.25. Akizungumza na Wananchi wa Mabogini, Wilaya Moshi Mkoani Kilimanjaro, Dkt. Mwigulu ameelekeza barabara hiyo ihamishwe kutoka TARURA, na kwenda TANROADS ili ijengwe kwa kiwango cha lami kwa kuwa ni Bypass hivyo itasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza msongamano katikati ya mji wa Moshi.

Rais Mwinyi Ashiriki Futari Iliyoandaliwa na Rais Samia Ikulu Tunguu-ZBR

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi amejumuika kwenye Futari iliyoandaliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa Viongozi wa Serikali, Vyombo vya ulinzi na Usalama, Siasa , Dini  na Wananchi mbalimbali katika Viwanja vya Ikulu ndogo ya Tunguu, Mkoa wa Kusini Unguja leo tarehe 19 Februari 2026.

Nyansaho Foundation Yaongeza Tabasamu Kwa Jeshi La Polisi Wilayani Serengeti

TAASISI ya Nyansaho Foundation imetoa msaada wa viti 50 pamoja na runinga (TV) ya kisasa ya inchi 65 kwa Jeshi la Polisi, kwa ajili ya matumizi ya askari katika Kituo Kikuu cha Polisi Mugumu, wilayani Serengeti mkoani Mara. Msaada huo umekabidhiwa rasmi kwa uongozi wa jeshi hilo kama sehemu ya mchango wa taasisi hiyo katika kuunga mkono taasisi za umma zinazotoa huduma kwa wananchi. Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, mwakilishi wa Nyansaho Foundation alisema kuwa taasisi hiyo inaamini katika ushirikiano wa karibu na Serikali ili kuboresha mazingira ya kazi kwa watumishi wa umma, wakiwemo askari wa Jeshi la Polisi ambao wana jukumu kubwa la kulinda usalama wa raia na mali zao. Alisema kuwa utoaji wa viti hivyo utasaidia kuboresha mazingira ya kazi na mapokezi kwa wananchi wanaofika kituoni hapo kupata huduma, huku runinga hiyo ikitarajiwa kusaidia katika utoaji wa elimu, taarifa pamoja na burudani kwa askari waliopo kazini. Kwa upande wake, kiongozi wa Jeshi la Polisi wilayani Ser...

Waziri Wa Tamisemi Aelekeza Kusimamishwa Kazi Watumishi 14 Wilayani Muheza

Na OWM - TAMISEMI, Muheza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu -TAMISEMI Mhe. Prof. Riziki Shemdoe, Kwa mujibu wa Kanuni ya 37(1) ya Kanuni za Utumishi wa Umma za mwaka 2022, amemuelekeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza akisimamiwa na RAS kuwapumzisha kutekeleza majukumu yao watumishi 14 wa Halmashauri hiyo ambao wanatuhumiwa kusababisha changamoto zilizokwamisha ujenzi wa jengo la utawala.  Prof. Shemdoe amewataja watumishi hao wanaosimamishwa kazi ili kupisha uchunguzi ni Afisa Hesabu Mwandamizi Rajabu Diamond Mushi, Mhandisi wa Kilimo Mkuu Abdallah Mohamed Jaha, Afisa Ugavi Msaidizi Shukuru Elias Marandu, Afisa Rasilimali watu Jesca Francis Luvigo, Mhandisi Careen Dustan Meela, Mkuu wa Idara ya Manunuzi Mwangaza Rajabu Kusenge, Mkuu wa Idara ya Elimu Msingi Pilly Maximilian Sindanguru na Kaimu Mkuu wa Idara ya Huduma za Sheria Angela Jabe Mwapachu. Amewataja wengine kuwa, ni Mkuu wa Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Edward Sempindu Mgaya, Mkuu wa Kitengo cha Michezo...

Kilimanjaro Hifadhi ya Pili Kwa Mapato Nchini

Na. Sixmund Begashe, Rombo Wananchi wanaoishi kuzunguka Hifadhi ya Taifa Kilimanjaro wamatakiwa kuendeleza uhifadhi na kutunza mazingira kwani hali hiyo imesaidia hifadhi hiyo kuwa ya pili Kitaifa kwa kuingiza mapato mengi hatua itakayochochea maendeleo kutokana na fedha zinazotokana na Utalii pamoja na uhifadhi.  Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) ameyasema hayo katika mkutano wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba na wananchi wa Wilaya ya  Rombo, Mkoani Kilimanjaro na kubainisha kuwa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ndio inayoshika nafasi ya kwanza kwa kuingiza fedha nyingi za kigeni na mapato makubwa kwa ujumla.  Dkt. Kijaji amefafanua kuwa kazi kubwa inayofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kutangaza Utalii na uhifadhi endelevu, sambamba na kuboresha miundo mbinu katika hifadhi za Taifa imepelekea  Hifadhi hiyo kuingiza shilingi bilioni 364,733,948,036 katika ...

Rea ni zaidi ya huduma kwa wananchi mkoani Tanga

📌 *Wananchi wahimizwa kujiunga mapema na huduma ya umeme* . 📌 *Wananchi waaswa kutumia huduma ya umeme kwa tija* . 📍 *MKINGA*  Wakala wa Nishati Vijijini (REA) unaendelea kufanyia vitendo nia yake ya kujali na kuthamini wananchi kwa kusaidia inafikisha huduma nafuu ya umeme kwenye kila kijiji na kijiji mkoani Tanga ili huduma hiyo isaidie kuboresha maisha ya wananchi mkoani humo. Kauli hiyo imetolewa na Afisa maendeleo ya jamii kutoka REA, ndugu Abdulrazack Mko wakati wa ziara ya kuhamasisha wananchi kujiunga na huduma ya umeme wilayani Mkinga mkoani Tanga. Aidha Mkomi, amewasisitiza wananchi kuwa waangalifu wakati wa kufanya malipo ya kujiunga na huduma ya umeme, akieleza kuwa gharama ya kuunganisha umeme vijijini ni shilingi 27,000 kwa makazi na shilingi 139,000 kwa Mitambo na mashine au viwanda na malipo yote yanalipwa kwa kutumia kumbukumbu inayotumwa moja kwa moja kutoka TANESCO kwa njia ya meseji na si vinginevyo. Aidha, uhamasishaji huo ulijikita zaidi katika kutoa elimu ...