Skip to main content

Posts

Showing posts from April 19, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Kampeni "Kiduchu Fresh Tunasonga" na uendelevu wa utoaji mikopo ya elimu

Na: Dk. Reubeni Lumbagala Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) ina jukumu la kutoa mikopo kwa waombaji ili waweze kutimiza malengo yao ya kupata elimu katika taasisi mbalimbali za elimu kama vyuo vya kati na vyuo vikuu.  Pia, HESLB inawajibika kukusanya mikopo kutoa kwa wanufaika wake ili kuwezesha waombaji wengine waweze kupata mikopo ili nao waweze kupata elimu. Kwa zaidi ya miaka 20 sasa, serikali kupitia HESLB, imewezesha vijana wengi wa Kitanzania kutimiza malengo yao ya kielimu kwa kuwakopesha mikopo ya elimu. Wengi wa vijana hao ni wale wanaotoka familia zenye changamoto za kiuchumi ambazo pengine bila kuwezeshwa mikopo, wasingeweza kumudu kupata elimu kutokana na gharama kubwa za elimu zilivyo huko vyuoni. Hii ndiyo kusema, baadhi yao wasingeweza kutimiza ndoto zao za kusoma fani na taaluma mbalimbali kama wasingepata mkopo wa elimu. Kwa kuwa tayari fedha nyingi zimewekezwa kwa kukopesha vijana wengi, HESLB inayo kazi kubwa ya kukusanya mikopo hiyo kutoka kwa...

Chatanda: Bunge Marathon Husaidia Kujenga Umoja na Afya

NA: MWANDISHI WETU - DODOMA  Mbunge wa Viti Maalum wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa (MCC), Mary Chatanda, ameshiriki msimu wa tatu wa mbio za hisani za "Bunge Marathon," zilizofanyila Aprili 18, 2026, Jijini Dodoma. Akizungumzia mbio hizo, Chatanda ameupongeza uongozi wa Bunge, wadhamini kwa kuandaa mbio hizo zenye lengo la kukuza umoja, mshikamano, kujenga afya dhidi ya magonjwa yasiyoambukiza. "Mbio za Bunge Marathon zinawaleta viongozi na wananchi pamoja, jambo linalojenga umoja na mshikamano wa Kitaifa. Tukumbuke pia mazoezi ni afya, hivyo kadri tunavyoshiriki tunajenga afya dhidi ya magonjwa yasiyoambukiza ambayo yamekuwa yakiathiri wananchi wengi," amesema Chatanda. Bunge Marathon huratibiwa na uongozi wa Bunge na huwashirikisha wabunge, viongozi, wadau  na wananchi kushiriki kukimbia umbali wa Kilometa 5, 10 na 21, huku washindi wa mbio hizo wakizawadiwa zawadi mba...

Bunge la Tanzania Laikaribisha Dunia Kwenye Ipu 153 Arusha

Naibu Spika wa Bunge la Tanzania na Mhe. Daniel Baran Sillo (Mb) amewakaribisha rasmi wawakilishi wa mabunge yote wanachama wa IPU kuhudhuria Mkutano wa 153 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) utakaofanyika Jijini Arusha kuanzia tarehe 5 hadi 9 Oktoba, 2026 Akizungumza katika sherehe za kufunga Mkutano wa 152 wa IPU jijini Istanbul, Uturuki, Mhe. Sillo ameishukuru Serikali na Bunge la Uturuki chini ya Spika *Mhe. Numan KurtulmuÅŸ* kwa ukarimu na maandalizi mazuri yaliyofanikisha mkutano huo. Mhe. Sillo amesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya uongozi wa Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kushirikiana na Bunge imejipanga kikamilifu kupokea wageni hao.  Ameeleza kuwa Tanzania ni nchi ya amani tangu uhuru 1961, yenye makabila zaidi ya 120 yanayoishi kwa umoja chini ya mwavuli wa lugha ya Kiswahili. “Tuna methali isemayo ‘Mgeni aje Mwenyeji apone’. Kwa mantiki hiyo, tumedhamiria kuhakikisha wajumbe wote wanapata VISA-FREE na VISA-ON-ARRIVAL,” amesema Mhe. Sillo. Am...

Waziri Mkuu Atoa Agizo Kwa Watendaji Serikalini

_Awataka wahakikishe miradi inasimamiwa na kuleta tija iliyokusudiwa_ WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema watendaji wa Serikali wanajukumu la kuhakikisha miradi ya maendeleo inayotokelezwa katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo ya maji, umeme, afya, miundombinu na elimu inasimamiwa ipasavyo ili Watanzania waweze kupata tija iliyokusudiwa. Waziri Mkuu amesema Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameweka jitihada kubwa katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo, hivyo ni lazima itekelezwe kama ilivyokusudiwa. Ametoa kauli hiyo leo (Jumapili, Aprili 19, 2026) wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Msanga, Chamwino mkoani Dodoma baada ya kuweka jiwe la msingi mradi wa maji akiwa katika ziara ya kikazi ya kukagua miradi ya maendeleo. Mheshimiwa Dkt. Mwigulu amesema jukumu kubwa walilonalo watendaji ni kusimamia ipasavyo miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo yao na kuhakikisha wananchi wananufaika ...

Dkt. Mwigulu Aweka Jiwe la Msingi Mradi wa Maji wa Miji 28, Chamwino Dodoma

WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba leo Aprili 19, 2026 ameweka jiwe la msingi la Mradi wa Maji wa Miji 28 katika mji wa Chamwino mkoani Dodoma. Mradi huo wa kimkakati wenye thamani ya Shilingi bilioni 17.20, unatekelezwa na Serikali kupitia Wizara ya Maji kwa kushirikiana na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) na mpaka sasa umefikia asilimia 70.2 ya utekelezaji. Kukamilika kwa Mradi huo kutawezesha kuhudumia zaidi ya wananchi 60,000 katika kata za Msanga, Buigiri, Chamwino na Mtumba, na kuongeza upatikanaji wa maji safi kutoka asilimia 91 hadi 100 pamoja na kuimarisha uzalishaji wa maji kukidhi mahitaji ya sasa na ya baadaye.  Akizungumza katika tukio hilo, Waziri Mkuu alimpongeza Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa utekelezaji wa mradi huo mkubwa ambao utanufaisha wakazi wa Wilaya ya Chamwino.

Balozi Yakubu akutana na wadau wa Tanzania France Chamber of Commerce kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi

Balozi mteule wa Tanzania nchini Ufaransa, Mheshimiwa Saidi Othman Yakubu, leo amekutana na viongozi na wanachama wa Tanzania France Chamber of Commerce katika kikao cha kujadili namna ya kuimarisha mahusiano ya biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Ufaransa, ikiwa ni sehemu ya maandalizi yake ya kuanza rasmi majukumu yake jijini Paris. Katika kikao hicho, Balozi Yakubu alipata fursa ya kupewa tathmini ya kina kuhusu uwekezaji wa Ufaransa nchini Tanzania, ambapo imeelezwa kuwa uwekezaji wa kampuni za Kifaransa umefikia takriban dola za Marekani bilioni 1.3, huku baadhi ya kampuni hizo zikiwepo nchini kwa zaidi ya miaka 30. Akizungumza katika mkutano huo, Balozi Yakubu alisisitiza dhamira ya Serikali ya Tanzania kuendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji na kuimarisha ushirikiano wa karibu na sekta binafsi ya Ufaransa. Aliahidi kushirikiana kwa karibu na wadau hao ili kuongeza mtiririko wa biashara, kuvutia uwekezaji mpya, na kuitangaza Tanzania kama lango la biashara katika ukanda ...